WILLY PAUL AMSHAMBULIA BAHATI, ADAI ANANUNUA VIEWS YOUTUBE
Staa wa muziki nchini Willy Paul amemshambulia mke wa Bahati, Diana B kwa madai ya kununua views Youtube. Kupitia ukurasa wake wa instagram Willy Paul amemsuta vikali Diana B kwa hatua ya wimbo wake uitwao “Hatutaachana” kufikisha zaidi ya views millioni moja ndani ya siku nne kitu ambacho hakijakuwa kikifanyika kwa nyimbo za wasanii nchini. Aidha amedai amemtolea uvivu Diana B kwa kusema hana kipaji cha muziki na hivyo hakuna namna wimbo wake ungefikisha idadi hiyo ya views wakati mashabiki wamekuwa wakimkejeli kwenye mitandao ya kijamii. Hata hivyo himaker huyo wa Heartbreak amemtaka DianaB akome kumzungumzia vibaya na badala yake ashindane na msanii wake mpya Queen P kwani yeye yupo kwenye level tofauti. Kauli ya Willy Paul imekuja mara baada ya Diana B kunukuliwa kwenye moja ya interview akisema Willy Paul anamchukia kwa sababu amemshinda kwa idadi ya views kwenye mtandao wa youtube.
Read More