WILLY PAUL ATANGAZA KUMUUNGA MKONO RAILA ODINGA KWENYE UCHAGUZI MKUU WA AGOSTI 9 NCHINI KENYA

WILLY PAUL ATANGAZA KUMUUNGA MKONO RAILA ODINGA KWENYE UCHAGUZI MKUU WA AGOSTI 9 NCHINI KENYA

Msanii nyota nchini Willy Paul amezua mjadala mzito kwenye mtandao wa kijamii baada ya kumtawaza kinara odm Raila Odinga kuwa rais wa tano wa Kenya kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu. Kupitia ukurasa wa Instagram Willy Paul ameweka wazi msimamo wake wa kisiasa bila uwoga kwa kuchapisha bango la kiongozi huyo wa Chama cha ODM, jambo linalotafsiriwa moja kwa moja kuwa hitmaker huyo wa Toto amejiunga rasmi na muungano wa Azimio la Umoja ambao unampigia debe Raila Odinga kutua uongozi wa nchi ya Kenya kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu     . Kauli hiyo ya Willy Paul imeibua hisia mseto miongoni mwa wakenya kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi wameonekana kukerwa na hatua ya msanii huyo kujihusisha na masuala ya kisiasa huku wengine wakimtaka aelekeze nguvu zake kwenye ishu ya kutoa muziki. Utakumbuka Willy Paul ambaye anamezea kiti cha ubunge eneo la Mathare Kaskazini juzi kati aliweka wazi kuwa yupo tayari kumenyana na wagombea wenzake kutoka eneo la mathare kaskazini kwenye uchaguzi wa mchujo wa chama cha ODM Aprili 17 mwaka huu wa 2022.

Read More
 WILLY PAUL AKANUSHA TAARIFA ZA KUIUA CAREER YA MWANAMUZIKI WA BONGOFLEVA DIAMOND PLATINUMZ

WILLY PAUL AKANUSHA TAARIFA ZA KUIUA CAREER YA MWANAMUZIKI WA BONGOFLEVA DIAMOND PLATINUMZ

Baada ya Kurasa moja ya udaku nchini kwenye mtandao wa Instagram kuchapisha taarifa kuwa Willy Paul ana mpango wa kuimaliza career ya msanii wa Bongofleva Diamond Platinumz tarehe 17 mwezi Aprili mwaka huu, msanii huyo ameibuka na kukanusha taarifa hizo. Kupitia uwanja wa comment ya post hiyo Willy Paul amesema madai hayo hayana msingi wowote kwani post yake ilitafsiriwa vibaya. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Toto” amesema post yake kwenye mtandao wa instagram ililenga kutangaza jambo lake ambalo litafanyika April 17 mwaka huu ingawa hakuweka wazi kama ni project ya wimbo au show. Utakumbuka Willy Paul kupitia Instagram Page yake aliandika ujumbe unaosomeka “Nimetangaza rasmi vita. Nizuie kama una uwezo, Aprili 17 nitazika mtu. Mimi sio Simba. Jina langu ni Willy Paul almaarufu Black Panther.” Ujumbe huo ulitafsiriwa moja kwa moja kumlenga Diamond platinumz ambaye amekuwa akijiita Simba.

Read More
 STAA MUZIKI NCHINI KENYA WILLY PAUL ADOKEZA UJIO WA NGOMA MPYA

STAA MUZIKI NCHINI KENYA WILLY PAUL ADOKEZA UJIO WA NGOMA MPYA

Mafanikio ya wimbo wa ‘Toto’ yanaonekana yanampa Staa wa muziki nchini Willy Paul jeuri ya kufikiria kuachia  wimbo mwingine mpya. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Willy Paul  amewaachia mashabiki zake swali iwapo aachie wimbo mpya mara baada ya wimbo wake wa Toto kufikisha zaidi ya views millioni moja kwenye mtandao wa youtube. Hata hivyo mashabiki zake wameonekana kuitikia wito wake wa kuachia wimbo mpya, hivyo huenda mtu mzima Willy Paul akawabariki na singo mpya muda wowote kuanzia sasa. Utakumbuka Toto ni wimbo unaopatikana kwenye album yake ya pili African Experience ambayo pia inafanya poa kwenye mtandao wa Boomplay Kenya ikizingatiwa kuwa mpaka sasa ina zaidi ya streams millioni moja.

Read More
 WILLY PAUL ACHUKIZWA NA JINA LA MKUNAJI, ATAKA MASHABIKI WAACHE KUMUITA JINA HILO

WILLY PAUL ACHUKIZWA NA JINA LA MKUNAJI, ATAKA MASHABIKI WAACHE KUMUITA JINA HILO

Mwanamuziki maarufu nchini Willy paul amewataka mashabiki zake kuacha kumuita jina la utani la Mkunaji. Kupitia instagram Willy paul amesema jina hilo ni la kishetani na lina mikosi mingi, hivyo hataki kuhusishwa nalo. Hitmaker huyo wa “My Woman” amesema tangu aanze kutumia jina la mkunaji amejipata kwenye kashfa nyingi ambazo amedai zimemuaharibia chapa au brand yake ya muziki. Hata hivyo amewaomba mashabiki zake kuacha kumuita mkunaji huku akisema kuwa imelazimika kuairisha suala la kuachia video ya wimbo wake wa toto kwa ajili ya kuhakikisha jina hilo linaondolewa kwenye video ya wimbo huo. “Morning fam, would like to take this opportunity to let everyone know that from today hence forth I will not be using the name ” MKUNAJI ” it’s evil and I don’t want to be associated with it! Ever since I embraced the name I’ve had too much problems. So if you’re truly a fan of Willy Paul, Willy Pozze. Stop calling him ” MKUNAJI ” We’re postponing the release of #TOTO video just to do away with this name, to make sure that it’s nowhere. You’ll notice afew changes when the #toto video drops. 2022 is not a year of problems!”..ameandika willy paul kupitia instagram page yake.

Read More
 WILLY PAUL AOMBA RADHI FAMILIA YA BAHATI KUFUATIA TUHUMA ZA KUTOKA KIMAPENZI NA DIANA MARUA

WILLY PAUL AOMBA RADHI FAMILIA YA BAHATI KUFUATIA TUHUMA ZA KUTOKA KIMAPENZI NA DIANA MARUA

Staa wa muziki nchini Willy Paul hatimaye ameiomba radhi familia ya Bahati baada ya kupewa makataa ya saa 24 kufanya hivyo la sivyo atafunguliwa mashtaka kwa madai ya kutoa matamshi ya chuki dhidi ya Diana Marua. Willy Paul awali alidai kuwa miaka kadhaa iliyopita alitoka  kimapenzi na mke wa Bahati japo hakubaka kama namna ambavyo Diana Marua alimtuhumu. Sasa kupitia screenshot ya ujumbe unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii willy paul ameonekana akimlilia Bahati amsamehe kutokana na kile kinachoendelea mtandao. Sanjari na hilo Willy Paul amemtumia Bahati Barua akisema kwamba madai yake ya kutoka kimapenzi na mke wake Diana Marua sio ya kweli kwani kiki tu,  hivyo Bahati anapaswa kuelewa kwani ni sehemu ya matukio ambayo utokea kwenye tasnia ya muziki. Hata hivyo haIjabainika kama kuna ukweli wowote kuhusiana na hilo ikizingatiwa kuwa Willy Paul wala Bahati hajatoa tamko lolote. Utakumbuka Januari 13 mwaka huu kuna barua ilikuwa inasambaa mitandaoni ikidaiwa kuwa ni ya wakili wa Diana Marua ambapo kwenye barua Willy Paul alipewa makataa ya saa 24 aombe msamaha la sivyo afungulie kesi mahakamani kwa madai ya kumharibia jina diana marua kuwa aliwahi toka nae kimapenzi.

Read More
 WILLY PAUL AKANUSHA KUIBA IDEA YA WIMBO WAKE MPYA KUTOKA KWA RINGTONE

WILLY PAUL AKANUSHA KUIBA IDEA YA WIMBO WAKE MPYA KUTOKA KWA RINGTONE

Nyota wa muziki nchini Willy Paul amekanusha madai ya kuiba idea ya wimbo wake mpya uitwao “Atoti Jaber” kutoka kwa msanii mwenzake Ringtone Apoko. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Willy Paul amemtaka Ringtone akome kueneza taarifa za uongo kwamba alimuibia wimbo wa “Atoti Jaber” huku akisema madai hayo hayana msingi wowote ikizingatiwa kuwa wimbo huo aliomshirikisha Klons Melody na Jakadalla sio wimbo wa injili. Those of you that know Ringtone know the kind of person he is.. My brother please stop telling your friends that I stole the song atotijaber from you. It has never been a gospel song, enough with your clout chasing bro. It’s 2022, new beginnings. I love and respect you as a big brother who came to this industry before me. To all my fans, keep supporting the song #atotijaber x @klons_melody x @musajakadalla_ ameandika Willy Paul kupitia Instagram yake Hitmaker huyo wa “My Woman” amesema amechoshwa na sarakasi za Ringtone ambapo ameenda mbali na kumtaka msanii huyo aelekeze nguvu zake kwenye ishu ya kutangaza kazi zake za muziki badala ya kutengeneza mitukio ili azungumziwe na vyombo vya habari nchini. Hata hivyo amesema anamheshimu Ringtone kama mmoja wa wasanii waliomtangulia kwenye tasnia ya muziki huku akiwataka mashabiki waendelee kusapoti wimbo wake wa “Atoti Jaber” kwenye digital platflorms mbali mbali za muziki.

Read More
 DIANA MARUA AFUTA VIDEO YA TUHUMA ZA UBAKAJI DHIDI YA WILLY PAUL YOUTUBE

DIANA MARUA AFUTA VIDEO YA TUHUMA ZA UBAKAJI DHIDI YA WILLY PAUL YOUTUBE

Mwanamitandao aliyegeukia muziki  Diana Marua amefuta video aliyotengeneza akidai kuwa staa wa muziki nchini Willy Paul alijaribu kumbaka. Hii ni baada ya  mahakama ya Milimani kutoa amri  ikimtaka Diana Marua kufuta video ambayo alipakia YouTube mnamo Desemba 9  yenye jina la ‘My Untold Story, Willy Paul tried to rape me’ ikielezwa kuwa madai yake yameathiri kazi na afya ya Willy Paul . “Inaamriwa kuwa video ya mshtakiwa/mlalamikiwa na chapisho la mitandao ya kijamii lililochapishwa kwenye chaneli yake ya YouTube yenye jina la ‘My Untold Story, Willy Paul tried to rape me’, lfutwe ikusubiriwa kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi yake kwa vile linamuathiri mlalamishi, kumfanya apoteze fursa za biashara na kumfanya ateseke kiafya” Karatasi ya amri za mahakama iliyotiwa saini na hakimu mkuu mwandamizi D.W Mburu ilisomeka. Mahakama pia ilimtahadharisha Diana na washirika wake dhidi ya kumharibia jina Willy Paul ikisubiriwa kusikilizwa kwa kesi aliyowasilisha mahakamani. Onyo kali imetolewa kwa yeyote atakayekaidi amri hiyo ya mahakama ambayo ilitolewa tarehe 29 Desemba.

Read More
 MAHAKAMA YAMUAMURU DIANA MARUA KUFUTA VIDEO YA TUHUMA ZA UBAKAJI DHIDI YA WILLY PAUL

MAHAKAMA YAMUAMURU DIANA MARUA KUFUTA VIDEO YA TUHUMA ZA UBAKAJI DHIDI YA WILLY PAUL

Mahakama ya Milimani nchini Kenya imemuamuru Diana Marua kufuta video aliyotengeneza akidai kuwa mwanamuziki Willy Paul alijaribu kumbaka. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Willy Paul alichapisha picha ya karatasi ya amri za mahakama iliyotiwa saini na hakimu mkuu mwandamizi D.W Mburu. Amri hiyo ya mahakama inamtaka Diana Marua kufuta video ambayo alipakia YouTube mnamo Desemba 9 ikielezwa kuwa madai yake yameathiri kazi na afya ya Willy Paul. “Inaamriwa kuwa video ya mshtakiwa/mlalamikiwa na chapisho la mitandao ya kijamii lililochapishwa kwenye chaneli yake ya YouTube yenye jina la ‘My Untold Story, Willy Paul tried to rape me’, lfutwe ikusubiriwa kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi yake kwa vile linamuathiri mlalamishi, kumfanya apoteze fursa za biashara na kumfanya ateseke kiafya” Karatasi hiyo ilisomeka. Mahakama pia imemtahadharisha Diana na washirika wake dhidi ya kumharibia jina Willy Paul ikisubiriwa kusikilizwa kwa kesi aliyowasilisha mahakamani. Onyo kali imetolewa kwa yeyote atakayekaidi amri hiyo ya mahakama ambayo ilitolewa tarehe 29 Desemba.

Read More
 RINGTONE APINGA AZMA YA WILLY PAUL KUJITOSA KWENYE ULINGO WA SIASA MWAKA 2022

RINGTONE APINGA AZMA YA WILLY PAUL KUJITOSA KWENYE ULINGO WA SIASA MWAKA 2022

Baada ya Willy Paul kutangaza azma ya kujiunga na siasa mwaka wa 2022, msanii wa nyimbo za injili nchini Ringtone ameonekana kutofautiana kimawazo na Hitmaker huyo wa “Lenga”. Akipiga stori na Mungai Eve kwenye mtandao wa Youtube Ringtone amesema watu wasichukulie kauli ya Willy Paul kwa uzito kwani msanii huyo anajaribu kushinda na msanii mwenzake Bahati ambaye kipindi cha nyuma alitia nia ya kuwania ubunge wa Mathare. Hitmaker huyo wa “Pamela” amemshauri Willy Paul aachane na siasa na badala yake awekeze nguvu zake kwenye muziki kwani ni mmoja wa wasanii ambao wana kipaji cha kipekee nchini. Sanjari na hilo Ringtone amedokeza kwamba mwaka wa 2022 ataweka wazi azma yake ya kujiunga na siasa kwani amekuwa akipata shinikizo za kuwania ubunge Dagorreti kaskazini kutoka kwa watu wake wa karibu. Ikumbukwe mwaka wa 2011 Ringtine aliwania ubunge katika uchaguzi mdogo wa Kitutu Masaba kupitia chama cha Vijana Progressive Party ambapo aliibuka wanane kwa kupata kura 467.

Read More
 WILLY PAUL ASHANGAZWA NA VIEWS ZAKE KUSHUKA YOUTUBE

WILLY PAUL ASHANGAZWA NA VIEWS ZAKE KUSHUKA YOUTUBE

Staa wa muziki nchini Willy Paul amefunguka na kuzungumzia ishu ya kupungua kwa idadi ya viewers wanaotazama video za nyimbo zake kwenye mtandao wa Youtube. Kupitia  Youtube live Willy Paul amedai kuwa kuna mchezo mchafu ambao unaendelea kwenye channel yake ya YouTube  ambapo amelalamika kuwa views za video za nyimbo zake zinapanda na kushuka. Hitmaker huyo wa “My Woman” amesema kuna msanii ameamua kusambaratisha harakati zake za kuupeleka muziki wake kimataifa kwa kununua baadhi ya watu ambao amedai wameweka kizuizi kwenye channeli yake ya Youtube ili watazamaji wa nyimbo zake wazipande. Hata hivyo ametoa onyo kwa msanii huyo ambaye hajamtaja jina kuacha tabia hiyo la sivyo atamwaanika ikizingatiwa kuwa ana idhibati inaonyesha kuwa amekuwa akinunua views youtube. Kauli hiyo ya Willy Paul imetafsiriwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii  kuwa ina mlenga moja kwa moja msanii mwenzake Bahati na mkewe Diana Marua ambao katika siku za hivi karibu hajakuwa na maelewano mazuri naye.

Read More
 WILLY PAUL ATANGAZA KUWANIA UBUNGE MATHARE MWAKA 2022

WILLY PAUL ATANGAZA KUWANIA UBUNGE MATHARE MWAKA 2022

Mwanamuziki nyota nchini Willy Paul ametia nia ya kugombea kiti cha ubunge eneo la Mathare  kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022. Hitmaker huyo “My Woman” ameweka wazi hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwwa kuandika ujumbe unaosomeka “Are you ready Mathare? Lets bring that change #Levels, ujumbe unaowataka wakaazi wa Mathare kumuunga mkono kwenye azma yake ya kuleta mabadiliko katika eneo hilo. Willy Paul hajaweka wazi  kama atawania wadhfa huo kama mgombea huru ama atatumia chamaa cha kisiasa kufanikisha azma yake hiyo ila ni jambo la kusbiriwa. Tangazo hilo la Willy Paul limeibua hisia mbali mbali miongoni mwa wakenya kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi wameonekana kutilia shaka uwezo wa Willy Paul kujiunga na siasa huku wengine wakiwataka msanii huyo ajitenge na  siasa na badala yake awekeze nguvu zake kwenye kutoa muziki mzuri. Iwapo Willy Paul atafanikisha mpango wake wa kuwania ubunge wa Mathare mwaka wa 2022 atajiunga na wasani wenzake kama Rufftone, Jalang’o, Frasha, Gabu, na Prezzo.

Read More
 WILLY PAUL AWEKA REKODI BOOMPLAY KUPITIA THE AFRICAN EXPERIENCE ALBUM

WILLY PAUL AWEKA REKODI BOOMPLAY KUPITIA THE AFRICAN EXPERIENCE ALBUM

Nyota wa muziki nchini Willy Paul anazidi kufanya vizuri kupitia mauzo ya mtandaoni na Albamu yake ya “The African Experience” ambayo tayari ina takriban mwezi mmoja tangu itoke rasmi. Album ya “The African Experience” ambayo ndio albamu ya pili kwa   Willy Paul tangu aanze muziki imefanikiwa kufikisha  zaidi ya Streams millioni moja kwenye mtandao wa kusikiliza na kupakua muziki wa Boomplay. Ikumbukwe album ya “The African Experience” kutoka kwa mtu mzima Willy Paul iliachiwa rasmi Oktoba 21 mwaka huu ikiwa na jumla ya mikwaju 17 ya moto huku  ikiwa na kolabo 9 pekee.

Read More