Sports news

Arsenal Yatinga Fainali ya Carabao Cup Baada ya Ushindi Dhidi ya Chelsea

Arsenal Yatinga Fainali ya Carabao Cup Baada ya Ushindi Dhidi ya Chelsea

Klabu ya Arsenal imefuzu kwa fainali ya Carabao Cup baada ya kuibwaga Chelsea kwa bao 1–0 katika mchezo wa marudiano uliopigwa kwenye Uwanja wa Emirates.

Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Kai Havertz katika dakika ya 96, akimalizia ushindi wa jumla wa mabao 4–2 kwa Gunners katika hatua ya nusu fainali ya mikondo miwili. Havertz, ambaye aliwahi kuichezea Chelsea, alihakikisha Arsenal inasonga mbele kwa kuipa timu yake goli la ushindi wa dakika za mwisho.

Kwa matokeo haya, Arsenal sasa itasubiri mshindi kati ya Manchester City na Newcastle United ili kukutana naye katika fainali itakayochezwa Wembley mnamo Machi 22, 2026.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, alisifu nidhamu na ari ya wachezaji wake, akisema kuwa kufuzu kwa fainali ni ushahidi wa maendeleo ya timu msimu huu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *