Twitter imeweka utaratibu mpya wa kuzuia ku-post picha ya mtu bila ruhusa yake. Twitter imesema ni marufuku kutuma au ku-post picha binafsi ya mtu bila ruhusa yake. Ku-tweet picha au video ya mtu ni kosa na inaweza kupelekea kufungiwa akaunti yako.
Endapo mtu akipost picha ya mtu bila ruhusa yake, mtu huyo anaweza kuripoti picha hiyo na twitter itaifuta na kutoa adhabu kwa mtu aliyepost bila ruhusa. Kiutaratibu kabla ya kupost video ya mtu unatakiwa mpatia Consent Form inayothibitisha huyo mtu amekupa ruhusa.
Kanuni hii ina mapungufu yake, haigusi watu maarufu kwa sababu inaweza kuwa ni habari. Hivyo kama ni picha au video ya mtu maarufu au vyombo binafsi vya habari, hakuna tatizo kupost.
Pia ni marufuku ku-post taarifa za namba za simu za mtu, address yake, majina yake, namba zake za ID, vitambulisho au taarifa ambazo sio zako