Mume wa mfanyabiashara na staa wa mitandao ya kijamii Zari Hassan, Shakib Cham, ametangaza nia ya kutaka kupambana tena ulingoni na msanii Rickman Manrick kufuatia pambano lao la ngumi lililomalizika kwa ushindi wa Rickman kwa knockout ya kutisha.
Licha ya kushindwa vibaya, Shakib Cham ameweka wazi kuwa hana hofu wala nia ya kujiondoa kwenye ndondi. Kupitia kauli zake, amesema kuwa bado anaamini ana uwezo wa kumshinda Rickman endapo atapewa nafasi nyingine, akisisitiza kuwa pambano la kwanza halikuwa mwisho wa safari yake ulingoni.
Katika pambano la kwanza lililovuta hisia za mashabiki wengi, Shakib alijikuta akinyeshewa mvua ya makonde mazito kutoka kwa Rickman Manrick, hali iliyomfanya apoteze fahamu na kuanguka chini ya ulingo.
Waamuzi walilazimika kusitisha pambano hilo mara moja kwa sababu za kiusalama hasa baada ya Zari Hassan kushindwa kujizuia na kumwaga machozi hadharani aliposhuhudia mume wake akizirai kutokana na kipigo hicho