Gossip

Eric Omondi Atangaza Rasmi Kuwania Ubunge Lang’ata

Eric Omondi Atangaza Rasmi Kuwania Ubunge Lang’ata

Mchekeshaji na mwanaharakati, Eric Omondi, ametangaza rasmi nia yake ya kuwania kiti cha Ubunge wa Lang’ata katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027.

Akizungumza na waandishi wa habari, Omondi amesema azma yake kubwa ni kuongoza kampeni kabambe ya kuhamasisha vijana kujisajili kama wapiga kura, akisisitiza kuwa mabadiliko ya kweli ya uongozi yatawezekana tu iwapo vijana watajitokeza kwa wingi kushiriki katika mchakato wa kidemokrasia.

Omondi pia amedai kuwa ifikapo mwaka 2027, wabunge wa wazee wataregeshwa nyumbani ili kupisha viongozi vijana wenye nguvu, mawazo mapya na uelewa wa changamoto za kizazi cha sasa. Kwa mujibu wake, wakati umefika kwa vijana kuchukua usukani wa uongozi na kushiriki kikamilifu katika maamuzi ya kitaifa.

Hatua ya Eric kuingia rasmi kwenye siasa za Lang’ata imezua maswali kuhusu uhusiano wake na Phelix Odiwour maarufu Jalang’o, mbunge wa sasa wa eneo hilo. Wawili hao waliwahi kuwa marafiki wa karibu na washirika katika tasnia ya burudani, lakini dalili zinaonyesha kuwa huenda mahusiano yao si mazuri kwa sasa, hasa ikizingatiwa msimamo wa Eric wa kutaka mabadiliko ya uongozi katika eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *