Mke wa Guardian Angel, Esther Musila amewajibu vikali wakosoaji waliodai ndoa yao haitafika mbali kuelekea maadhimisho ya miaka minne ya ndoa na miaka sita tangu waanze kuwa pamoja.
Akizungumza kupitia mitandao ya kijamii, Esther amesema kuwa yeye na Guardian Angel bado wapo imara na hawana mpango wa kuachana hivi karibuni, licha ya shinikizo kutoka kwa jamii kuhusu suala la kupata mtoto pamoja na tofauti yao kiumri.
Mwanamama huyo wa miaka 55, amesema walimwengu wanapaswa kuwazoea kuwaona pamoja, akisisitiza kuwa ndoa yao haiendeshwi na maoni ya watu bali misingi ya mapenzi, heshima na uamuzi wao binafsi.
Hata hivyo amesema kuwa tarehe 4 Januari itakuwa siku maalum sana kwa familia yao, kwani watakuwa wakiadhimisha miaka minne ya ndoa na pia kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Guardian Angel. Ameahidi kuwa kutakuwa na jambo kubwa litakalowashangaza wengi na kuwanyamazisha wanaowabeza na kuwashambulia mitandaoni.