Entertainment

Waandaaji wa Tamasha la Asake na Gabzy Washtakiwa kwa Uzembe

Waandaaji wa Tamasha la Asake na Gabzy Washtakiwa kwa Uzembe

Familia ya marehemu Karen Lojore imewasilisha rasmi kesi mahakamani ikidai fidia ya Shilingi milioni 100 za Kenya kufuatia kifo cha binti huyo kilichotokea katika tamasha la muziki lililofanyika Uwanjani Nyayo mwezi Disemba mwaka jana.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizowasilishwa mahakamani, Karen alipoteza maisha baada ya kutokea msongamano mkubwa wa watu (crowd surge) wakati wa tamasha lililowahusisha wasanii Asake na Gabzy. Familia inadai tukio hilo lingeweza kuzuilika iwapo hatua stahiki za usalama zingechukuliwa.

Katika kesi hiyo, waandaaji wa tamasha hilo, Tukutane Entertainment, wametajwa kama wadaiwa wakuu, wakituhumiwa kushindwa kuhakikisha usalama wa kutosha kwa mashabiki waliohudhuria hafla hiyo. Familia ya marehemu inaeleza kuwa uzembe katika maandalizi na udhibiti wa umati wa watu ndio uliopelekea kupotea kwa maisha ya Karen.

Familia sasa inaitaka mahakama kutoa haki kwa marehemu kwa kuwalazimisha wahusika kuwajibika, huku wakisisitiza kuwa fidia wanayodai ni kwa ajili ya madhara makubwa ya kihisia, kiakili na kifamilia waliyopata kutokana na kumpoteza mpendwa wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *