Harmonize Aibua Maswali kwa Kuficha Sura ya Mpenzi Mpya

Harmonize Aibua Maswali kwa Kuficha Sura ya Mpenzi Mpya

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Harmonize, ameibua gumzo mitandaoni baada ya kuonyesha dalili za kuwa kwenye uhusiano mpya wa kimapenzi. Kupitia Insta Story yake, Harmonize amepost picha na video zikimuonesha akiwa na mrembo anayesemekana kuwa mpenzi wake mpya huku akificha sura yake. Hatua hiyo imezua minong’ono miongoni mwa mashabiki ambao wamekuwa wakijiuliza ni nani haswa mpenzi huyo mpya wa mkali huyo wa Best Couple. Tetesi hizo zimezidi kushika kasi baada ya video nyingine kusambaa, ikimuonesha Harmonize akiwa amelala pembezoni mwa mrembo huyo. Tukio hilo limeibua mjadala kuhusu ni kwa nini staa huyo anaamua kuficha sura ya mchumba wake mpya ilhali tayari kumekuwepo na ushahidi wa video kuvuja.

Read More
 Jaketi la Khaligraph Lapigwa Mnada kwa Dola 100

Jaketi la Khaligraph Lapigwa Mnada kwa Dola 100

Jamaa mmoja nchini Kenya ameibua gumzo mitandaoni baada ya kudai kuwa anauza jaketi alilopewa na Rapa Khaligraph Jones, wakati wa onyesho lililofanyika Machakos. Kwa mujibu wa jamaa huyo, jaketi hilo ni zawadi ya moja kwa moja kutoka kwa Papa Jones. Hata hivyo, amesema sasa amelazimika kuliuza kwa bei ya dola 100 (takribani KSh 13,000) akieleza kuwa ana mahitaji ya kifedha. Taarifa hiyo imezua maoni tofauti mitandaoni. Baadhi ya mashabiki wameshangazwa na uamuzi wa kuuza zawadi ya msanii mkubwa kama Khaligraph, huku wengine wakisisitiza kuwa mara tu zawadi inapotolewa, mwenye kupokea ana uhuru wa kuamua atalifanyia nini. Mpaka sasa, Khaligraph Jones hajaweka wazi msimamo wake kuhusu suala hilo, na kuacha mashabiki wakijiuliza kama kweli jaketi hilo ni la ukweli au ni mbinu ya kutafuta kiki.

Read More
 VJ Patelo Apuuzilia Uvumi wa Kuibiwa Dandora

VJ Patelo Apuuzilia Uvumi wa Kuibiwa Dandora

Msanii kutoka Kenya VJ Patelo amekanusha vikali tetesi zilizokuwa zikisambazwa mitandaoni kwamba alivamiwa na kuibiwa Chains zake za dhahabu katika eneo la Dandora, Nairobi. Akijibu madai hayo, Patelo amesema anashangazwa na watu wanaobuni stori za uongo ili kutafuta umaarufu na kufuata vichwa vya habari. Ametoa msimamo wake kwamba hajawahi kuibiwa wala kushambuliwa Dandora, na kwamba ukimya wake mtandaoni ni wa kawaida kutokana na ratiba zake binafsi. Aidha, amewataka wafuasi wake kupuuza taarifa zisizo na msingi na kuendelea kumuunga mkono katika kazi zake za sanaa. Uvumi huo ulianza baada ya jamaa mmoja kudai kuwa Patelo alinyang’anywa mali zake, jambo ambalo limepelekea mashabiki wengi kuhoji ni kwa nini hakuwa akiposti kwenye mitandao ya kijamii kwa siku mbili zilizopita.

Read More
 Kenya Yatamba KGL Millennium Half Marathon, Accra

Kenya Yatamba KGL Millennium Half Marathon, Accra

Wanariadha wa Kenya walifagia medali zote katika mbio za mwaka huu za nusu marathoni za KGL Millennium mjini Accra, Ghana, na kuweka rekodi mpya katika mbio za wanaume na wanawake. Katika mbio za wanaume, Gilbert Kiprotich alinyakua taji ya mwaka huu kwa kutumia muda mpya wa saa 1 na sekunde 59, akifuatwa na Alfred Cherono kwa saa 1 dakika 01 na sekunde 04 na Paul Eyanae kwa saa 1 dakika 02 na sekunde 12. Muda huo wa Kiprotich ulivunja rekodi ya awali ya mbio hizo na hivyo akajipatia tuzo ya 900,000 shillings. Shindano la wanawake lilitawaliwa na Hympha Kiteta mwenye umri wa miaka 20, ambaye alimaliza mbio hizo kwa saa 1 dakika 07 na sekunde 42. Lucy Ndambuki na Eunice Muchiri wakafuatia katika nafasi ya pili na ya tatu na hivyo kuipa Kenya nishani zote za mbio hizo.

Read More
 Cardi B Atinga Mitaani New York Kutangaza Albamu Yake Mpya

Cardi B Atinga Mitaani New York Kutangaza Albamu Yake Mpya

Msanii wa muziki wa hip-hop nchini Marekani, Cardi B, amewashangaza mashabiki na wachambuzi wa muziki baada ya kuonekana akizunguka mtaani ya New York akitangaza kwa mikono yake mwenyewe albamu yake mpya “Am I The Drama.” Tukio hilo lililoshuhudiwa na wapita njia na mashabiki wake limeibua mitazamo tofauti. Wapo wanaoona hatua hiyo kama mkakati wa kibunifu wa kumfanya msanii huyo aendelee kuwa karibu na mashabiki wake na kuonesha unyenyekevu katika tasnia ambayo mara nyingi hutegemea matangazo makubwa ya kibiashara. Hata hivyo, upande wa pili wa maoni unasema ni dalili za kukata tamaa na ishara kwamba mradi huo huenda unakumbwa na changamoto za kupenya sokoni kabla hata ya kutoka rasmi. Kwenye mitandao ya kijamii, mjadala umechacha. Wafuasi wake wanamsifu kwa ujasiri wa kwenda mitaani na kujibebea jukumu la kutangaza kazi yake badala ya kutegemea matangazo ya kibiashara pekee. Lakini wakosoaji wanadai hatua hiyo inadhihirisha presha anayokabiliana nayo, hasa katika soko la muziki lenye ushindani mkali ambapo wasanii wapya na wakongwe huachia miradi kila mara.

Read More
 Sugu Awakosoa Mastaa Tanzania kwa Kudharau Harakati za Kudai Haki

Sugu Awakosoa Mastaa Tanzania kwa Kudharau Harakati za Kudai Haki

Mwanasiasa ambaye pia ni msanii wa hip hop, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, amewatolea uvivu mastaa wa muziki Diamond Platnumz, Ommy Dimpoz, Jux na Marioo kwa kauli zao za kuwataka wananchi kuacha kulalamikia Serikali na badala yake wafanye kazi. Sugu, ambaye kwa sasa ni mwanachama wa chama cha upinzani nchini Tanzania, alicharuka mitandaoni akiwataka wasanii hao kuacha kudharau wale wanaopigania haki na badala yake kujiunga katika harakati za kudai mabadiliko ya kisiasa na kijamii. Kupitia Instagram, amedai kuwa baadhi ya wasanii waliofanikiwa kimaisha wameanza kuwasihi wananchi “kutafuta kazi” badala ya kulalamika kuhusu changamoto zinazotokana na serikali. Kauli hizo, kwa mujibu wa SUGU, zinaonyesha dharau kwa wafuasi wa mageuzi. Akitumia maneno makali, SUGU amesisitiza kuwa yeye na kizazi chake wamekuwa wakipiga muziki na kujipatia mamilioni tangu miaka ya 1998, lakini bado wamekuwa mstari wa mbele kudai haki na ustawi wa taifa. Ameongeza kuwa mafanikio binafsi hayapaswi kuzuia mtu kushiriki katika mapambano ya kijamii na kisiasa.

Read More
 Msanii wa Uganda Bruno K Aanzisha Kampeini ya Kuchangia Mazishi ya Gogo Gloriose

Msanii wa Uganda Bruno K Aanzisha Kampeini ya Kuchangia Mazishi ya Gogo Gloriose

Mwanamuziki kutoka Uganda, Bruno K, ameanzisha kampeni ya kuchangisha fedha kusaidia mazishi ya msanii wa injili wa Rwanda, Gogo Gloriose, aliyefariki dunia nchini Uganda tarehe 4 Septemba baada ya kuugua kwa muda mfupi. Kupitia TikTok Live akiwa na meneja wa marehemu, Bruno K ameeleza kuwa kuna uhitaji wa dharura wa msaada wa kifedha ili kulipa bili ya hospitali na kuandaa usafirishaji wa mwili wa Gogo kurudi Rwanda kwa mazishi. Amesisitiza kuwa Gogo hakuja Uganda kwa shughuli za kibiashara bali alikuwa akihudumu, hivyo ni jukumu la mashabiki na makanisa aliyowahi kuhudumu kushirikiana kumpa heshima ya mwisho. Hata hivyo amebainisha pia kuwa mchango huo unahitajika kwa ajili ya kulipa bili ya hospitali, kununua jeneza na kugharamia gharama za usafirishaji wa mwili wake kuelekea Rwanda. Marehemu, kwa jina halisi Gloriose Musabyimanna, alikuwa amesafiri Uganda kuhudhuria ibada ya injili alipougua ghafla na kulazwa hospitalini Kyengera ambako alifariki dunia.

Read More
 Mbosso Apata Views Nyingi Kenya Kuliko Tanzania Kwenye YouTube

Mbosso Apata Views Nyingi Kenya Kuliko Tanzania Kwenye YouTube

Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Mbosso, ameibua mjadala baada ya takwimu kuonyesha kuwa muziki wake unasikilizwa zaidi nchini Kenya kuliko nyumbani kwao Tanzania. Kwa mujibu wa ripoti ya takwimu za YouTube, nyimbo za Mbosso zimeangaliwa zaidi ya mara milioni 102 kutoka Kenya, ikilinganishwa na mara milioni 47 kutoka Tanzania. Hii inamaanisha kwamba takribani asilimia 68.5 ya watazamaji wake kutoka Kenya na Tanzania wanatoka Kenya pekee. Ufanisi huu unaonyesha namna Mbosso alivyojijengea mashabiki wakubwa nchini Kenya, huku muziki wake ukiendelea kushika nafasi kwenye redio, majukwaa ya kidijitali na mitoko ya burudani. Wachambuzi wa muziki wanasema hali hii inathibitisha nguvu ya soko la Kenya kwa wasanii wa Afrika Mashariki, na kwa Mbosso, inaweza kufungua milango ya ushirikiano zaidi na wasanii wa Kenya pamoja na kuongeza idadi ya shoo katika nchi hiyo.

Read More
 Nyashinski Atangaza Tarehe Rasmi ya Albamu Mpya “Yariasu”

Nyashinski Atangaza Tarehe Rasmi ya Albamu Mpya “Yariasu”

Mwanamuziki nguli wa Kenya, Nyashinski, amethibitisha kuwa albamu yake mpya itajulikana kwa jina “Yariasu” na itaingia sokoni tarehe 19 Septemba 2025. Albamu hiyo inabeba jumla ya nyimbo 13, ambazo msanii huyo amezitaja kuwa za moto na zimeandaliwa kwa ubora wa kimataifa. Kupitia mitandao ya kijamii, Nyashinski amewataka mashabiki wake kufanya pre-order ya albamu hiyo mtandaoni ili kuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuisikiliza mara tu itakapotoka. Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wake wameonekana kutaka zaidi, wakimhimiza kuachia albamu yote kwa pamoja badala ya kutoa ngoma moja moja. Licha ya maoni hayo, tayari Nyashinski ameachia nyimbo mbili kutoka kwenye albamu hiyo, ambazo ni “Tai Chi” na “P.i.c”, zilizopokelewa kwa shangwe na mashabiki wake. Albamu ya “Yariasu” inatarajiwa kuwa miongoni mwa matoleo makubwa zaidi ya mwaka huu, ikidumisha nafasi ya Nyashinski kama mmoja wa wasanii wakubwa na wabunifu zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Read More
 Thee Pluto Apokea YouTube Gold Play Button Kwa Subscribers Milioni Moja

Thee Pluto Apokea YouTube Gold Play Button Kwa Subscribers Milioni Moja

Mwanamitandao maarufu Thee Pluto ameendelea kuandika historia katika tasnia ya maudhui ya kidijitali baada ya kipindi chake cha Thee Pluto Show kufikisha zaidi ya subscribers milioni moja kwenye mtandao wa YouTube. Hatua hiyo imemfanya kutunukiwa tuzo ya heshima ya YouTube Gold Play Button, ikiwatambua waundaji wa maudhui wanaofikisha idadi hiyo kubwa ya subscribers. Thee Pluto, anayefahamika zaidi kwa vipindi vyake vya loyalty test ambavyo vimejipatia mashabiki wengi hususan vijana, alisherehekea mafanikio haya makubwa akiwa likizoni katika kisiwa cha Bali, Indonesia. Aliwashukuru mashabiki wake kwa mchango wao mkubwa katika safari yake, akisema bila wao mafanikio hayo yasingewezekana. Kwa mujibu wa takwimu za akaunti yake, Thee Pluto alijiunga na YouTube mnamo Januari 5, 2018, na kufikia sasa ameshapakia zaidi ya video 1,288, ambazo kwa pamoja zimeangaliwa zaidi ya mara 273 milioni. Hii ni ishara ya ushawishi wake mkubwa na nafasi yake katika soko la burudani mtandaoni. Kwa kutunukiwa Gold Play Button, Thee Pluto amejiunga na kundi dogo la waundaji maudhui wa Kenya waliovuka mipaka ya ndani na kuonyesha kuwa bidii, ubunifu na uthabiti vinaweza kufanikisha safari ya kimataifa kupitia jukwaa la YouTube.

Read More
 YY Amtema Mpenzi Baada ya Kukosa Kutandika Kitanda

YY Amtema Mpenzi Baada ya Kukosa Kutandika Kitanda

Mchekeshaji maarufu wa Kenya, YY Comedian, amefichua kisa cha kushangaza kuhusu maisha yake ya mapenzi ya zamani. Akizungumza katika kipindi cha Feast with Friends kinachoendeshwa na Shiksha Arora, YY alieleza kuwa aliwahi kumtema mwanamke mara baada ya mkutano wao wa kwanza kwa sababu alishindwa kutandika kitanda. Kwa mujibu wa msanii huyo, tukio hilo lilimfanya atathmini mitazamo na maadili ya mpenzi wake, jambo lililomsukuma kufikia uamuzi wa haraka wa kumaliza uhusiano. YY alisema kwake nidhamu na mpangilio ni mambo ya msingi katika maisha ya kila siku, na kushindwa kwa mwanamke huyo kutandika kitanda kulionekana kama ishara ya kutopenda usafi na kutojali mambo madogo. Kisa hicho kimezua mijadala mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakiona sababu hiyo kuwa ndogo mno kupelekea kuvunja uhusiano, huku wengine wakimtetea wakisema kila mtu ana haki ya kuweka viwango vyake vya maisha binafsi. YY Comedian amejulikana kwa ucheshi wake wa kipekee na mara nyingi hutumia matukio ya maisha binafsi kama chanzo cha vichekesho, jambo linalomfanya kuendelea kuwa miongoni mwa wakali wa tasnia ya ucheshi nchini Kenya.

Read More
 Trevor Amkingia Kifua Diana B Baada ya Ukosoaji wa “Bibi Ya Tajiri”

Trevor Amkingia Kifua Diana B Baada ya Ukosoaji wa “Bibi Ya Tajiri”

CEO wa Chama cha Content Creators nchini Kenya, Director Trevor amejitokeza na kumkingia kifua Diana B baada ya kupata ukosoaji mkali kutokana na wimbo wake mpya Bibi ya Tajiri ambao una zaidi ya views laki tano youtube ndani ya siku tatu. Hii ni baada ya baadhi ya mashabiki na wakosoaji wa muziki kudai kuwa Diana hana kipaji cha uimbaji na uandishi wa muziki. Akizungumza, Trevor amewataka Wakenya kumuunga mkono Diana badala ya kumbeza, akisisitiza kuwa kila msanii anastahili nafasi ya kujaribu na kukuza sanaa yake. Aidha, amewataka wasanii wa Kenya kushirikiana naye ili kuendeleza muziki wa ndani badala ya kumpuuza. Trevor, hata hivyo, amesisitiza kuwa huu ni mwanzo wa safari ya Diana katika muziki na kwamba anastahili nafasi ya kuthibitisha kipaji chake. Ukosoaji huo ulianza baada ya mashabiki kudai kuwa Bibi ya Tajiri ilikuwa sampled kutoka wimbo maarufu wa marehemu E-Sir, Sare Sare. Haikuishia hapo, baadhi walimlaumu Diana kwa kuchana picha za marapa wakubwa nchini kama Khaligraph Jones na Nyashinski kwenye video yake, wakisema kitendo hicho ni kukosea heshima muziki wa hip hop.

Read More