Kenya Kusimamia Mpira wa Kikapu kwa Ukumbi wa Kisasa

Kenya Kusimamia Mpira wa Kikapu kwa Ukumbi wa Kisasa

Serikali ya Kenya imeingia makubaliano na Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Kitaifa (NBA) kujenga ukumbi wa kisasa wa kimataifa humu nchini. Uamuzi huu ulifikiwa katika mazungumzo kati ya Waziri wa Michezo, Salim Mvurya, na maafisa wakuu wa NBA wakiongozwa na Clare Akamanzi, afisa mkuu wa eneo la Bara Afrika. Ukumbi huu utakaojengwa kwa kasi unatarajiwa kuwa na uwezo wa kuandaa mashindano ya mpira wa kikapu ya kimataifa, jambo litakalowawezesha wanamichezo wa Kenya kupata fursa kubwa zaidi za kuonyesha vipaji vyao na kushindana na wachezaji kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Serikali imeahidi kutoa eneo maalum kwa ajili ya ujenzi huo kama sehemu ya mikakati yake ya kukuza na kuendeleza talanta za michezo nchini. Kwa upande wake, NBA itachangia kwa kiasi kikubwa katika fedha za ujenzi na itahakikisha ukumbi huo unakuwa mahali pa kisasa na lenye kuvutia, si tu kwa ajili ya michezo bali pia kwa ajili ya shughuli zingine za burudani. Mradi huu unatarajiwa pia kutoa ajira na kuongeza fursa za kiuchumi kwa wanamichezo pamoja na jamii kwa ujumla.

Read More
 Khaligraph Ageuza Kejeli Kuwa Faida Kupitia OG Omollo Sweatpants

Khaligraph Ageuza Kejeli Kuwa Faida Kupitia OG Omollo Sweatpants

Msanii wa Hip Hop nchini Kenya, Khaligraph Jones, ameonyesha ubunifu na ujasiri kwa kugeuza kejeli alizopokea kutoka kwa rapa Octopizzo kuwa fursa ya biashara. Kupitia mitandao yake ya kijamii, Khaligraph alizindua Limited Edition OG Omollo Custom Sweatpants, hatua iliyowaacha mashabiki wake wakimpongeza kwa uamuzi wa kipekee. Khaligraph ambaye anafanya vizuri na single yake mpya “Confuse” amehitimisha ujumbe wake kwa kutumia hashtag maarufu #respecttheogs, ishara ya kuendeleza msimamo wake wa kudumisha heshima na ushawishi katika anga ya muziki wa rap nchini humo. Uamuzi huo ulionekana kama jibu la moja kwa moja kwa kejeli kutoka kwa rapa mwenzake, Octopizzo, ambaye alinukuliwa akisema “Kuna rapper flani huvaa sweatpants from January to December na timber ya yellow.” Badala ya kuchukua maneno hayo kwa njia hasi, Khaligraph aliuchukua mtindo huo na kuubadilisha kuwa bidhaa ya kibiashara, hatua iliyotafsiriwa na mashabiki kama “clap back” ya kishujaa. Mashabiki wengi walimsifu kwa ubunifu huo, wakisema ni mfano bora wa jinsi msanii anaweza kutumia ukosoaji kujinufaisha.

Read More
 VJ Patello Amchana Diana B Baada ya Madai ya Chain Feki

VJ Patello Amchana Diana B Baada ya Madai ya Chain Feki

Mzozo kati ya VJ Patello na Influencer aligeukia muziki Diana B umeendelea kuchukua sura mpya baada ya Patello kujibu vikali madai ya kwamba mikufu yake ya dhahabu ni bandia. Kupitia Instagram, Patello alimshutumu Diana na mumewe Bahati kwa kushindwa kulipa shilingi milioni moja kwa Harambee Stars, akiongeza kuwa wawili hao hawana uhalali wa kuzungumzia vitu vya thamani. Ugomvi huo ulianza baada ya Patello kukosoa wimbo mpya wa Diana B uitwao Bibi ya Tajiri, ambapo Diana alisikika akijinadi kuwa ndiye rapa bora nchini Kenya huku akionekana kwenye video akirarua picha za marapa maarufu kama Khaligraph Jones na Nyashinski. Kitendo hicho kilimkera Patello ambaye alimtolea uvivu kwa kudai kuwa hana heshima kwa wasanii halisi wa hiphop, akamtaka aendelee na masuala ya content creation kwa sababu hajui kurap. Diana B hakusita kujibu mashambulizi hayo kwa kumdharau Patello, akisema kwa kejeli kwamba ni ajabu mtu mwenye mikufu bandia anathubutu kukosoa kazi ya “Bibi ya Tajiri”

Read More
 Instagram Yazindua App Rasmi kwa Watumiaji wa iPad

Instagram Yazindua App Rasmi kwa Watumiaji wa iPad

Instagram imetangaza rasmi kuanzisha programu maalum kwa watumiaji wa iPad, hatua inayokuja baada ya zaidi ya miaka 15 ya huduma hiyo kupatikana kwa watumiaji wa simu pekee. Tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2010, Instagram haijawahi kuwa na toleo rasmi kwa iPad, hali iliyowalazimu watumiaji kutumia app ya iPhone ambayo haikuwa na muonekano unaoendana na skrini kubwa ya iPad. Katika toleo hili jipya, Instagram imefanya mabadiliko kadhaa ya kimtindo na kimuundo. Ukurasa wa mwanzo wa app ya iPad umejikita zaidi kwenye maudhui ya video fupi (Reels) badala ya picha na machapisho ya kawaida (Feeds), tofauti na ilivyo kwenye toleo la simu. Aidha, sehemu ya maoni sasa inaweza kusomwa bila kuvuruga uonyeshaji wa video, na watumiaji wataweza kufungua ujumbe wa moja kwa moja huku wakiendelea kuona orodha ya mazungumzo yao upande mwingine wa skrini. Ripoti za hivi karibuni zinaonesha kuwa watoto na vijana wengi hutumia iPad kwa matumizi ya burudani, hasa kupitia TikTok, ambayo tayari imewekeza katika matumizi ya iPad na Smart TV. Hatua ya Instagram kuzindua toleo hili inatazamwa kama njia ya kuingia rasmi kwenye ushindani wa jukwaa la maudhui ya video, likiwa linalenga kuvutia kundi hilo la watumiaji na kuongeza muda wa matumizi kwenye jukwaa hilo.

Read More
 Mwimbaji wa Rwanda, Gloriose Musabyimana ‘Gogo’ Afariki Dunia Uganda

Mwimbaji wa Rwanda, Gloriose Musabyimana ‘Gogo’ Afariki Dunia Uganda

Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Rwanda, Gloriose Musabyimana maarufu kama Gogo, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 36. Taarifa zinaeleza kuwa Gogo alifariki usiku wa Septemba 3, 2025 nchini Uganda baada ya kuugua kwa muda mfupi. Kifo chake kimewashtua mashabiki na wadau wa muziki, ambapo wengi wameeleza masikitiko yao kupitia mitandao ya kijamii. Gogo alipata umaarufu kupitia nyimbo zake za injili mtandaoni, hususan wimbo wake “Blood of Jesus Christ”, uliomuwezesha kupata mashabiki wengi wa muziki wa injili. Nyimbo zake za kuinua roho zilimfungulia milango ya kutumbuiza katika mataifa mbalimbali, ikiwemo Uganda ambako aliwahi kushiriki katika Mega Gospel Concerts. Hivi karibuni, aliwahi kufanya onyesho mjini Mbarara, na wakati wa kifo chake alikuwa bado jijini Kampala, Uganda. Ingawa chanzo halisi cha kifo chake bado hakijabainika, taarifa zinaashiria kuwa alikumbwa na changamoto kadhaa za kiafya kabla ya mauti. Msanii Bruno K, ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa Gogo, amethibitisha taarifa za kifo chake kupitia mtandao wa kijamii leo asubuhi kwa huzuni kubwa. “Ni habari za kusikitisha kweli,” aliandika. “Nilipigiwa simu leo asubuhi kuarifiwa kuhusu kifo cha Gogo. Ni kweli ameenda kukutana na Bwana; meneja wake ndiye aliyenithibitishia.” Kifo cha Gogo kimeacha pengo kubwa katika muziki wa injili, huku mashabiki na wenzake wakimkumbuka kwa sauti yake yenye nguvu na ujumbe wa matumaini aliouacha kupitia muziki.

Read More
 Instagram Kuja na Mfumo Mpya wa Picture-in-Picture (PIP) kwa Reels

Instagram Kuja na Mfumo Mpya wa Picture-in-Picture (PIP) kwa Reels

Instagram imeanza kujaribu mfumo mpya wa Picture-in-Picture (PIP), ambao utawawezesha watumiaji wake kuendelea kutazama video za Reels hata baada ya kufunga app ya Instagram. Kwa kutumia teknolojia hii, watumiaji wataweza kufanya shughuli nyingine kwenye simu zao huku bado video ikiendelea kuonekana kwenye kona ya skrini. Kwa mfano, unaweza kutazama Reel huku ukiandika ujumbe kwenye WhatsApp, kusoma meseji, kutumia browser au hata ukiwa kwenye home-screen ya simu yako. Hii ni hatua kubwa kwa Instagram katika kuongeza urahisi wa kutumia app na kuwapa watumiaji wake uwezo wa multitasking bila kukatizwa na hitaji la kubaki ndani ya app muda wote. Kwa sasa, hii ni huduma ya majaribio na inapatikana kwa watumiaji wachache tu. Hata hivyo, Instagram imethibitisha kuwa mfumo huu mpya utaanza kupatikana kwa watumiaji wote hivi karibuni. Maboresho haya yanaashiria mwelekeo mpya wa Instagram wa kufanya matumizi ya video kuwa rahisi zaidi na kuendana na mahitaji ya watumiaji wa kisasa wanaotaka kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.

Read More
 Diana B Atangaza Ujio Mpya Kwenye Muziki Baada ya Ukimya wa Miaka 2

Diana B Atangaza Ujio Mpya Kwenye Muziki Baada ya Ukimya wa Miaka 2

Mwanamitandao aliyegeukia muziki,Diana B, ametangaza rasmi kurejea kwenye muziki baada ya ukimya wa miaka miwili wa kutoachia wimbo wowote. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diana B amedokeza kuwa leo atawazawadia mashabiki wimbo mpya unaoitwa “Bibi Ya Tajiri”. Akiwa mwenye bashasha, ameeleza kuwa kipindi chote cha miaka miwili hakukuwa cha kupumzika bali cha kufanya kazi kwa bidii ili kujijenga. Diana ambaye amekuwa akijulikana kwa kuonyesha maisha yake ya kifahari pamoja na mume wake msanii Bahati, amejinasibu kuwa jitihada zake zimezaa matunda na kwamba kwa sasa anajivunia kuwa tajiri, kauli ambayo pia ndiyo jina la single yake mpya. Ujumbe huo umewasha moto wa shauku miongoni mwa mashabiki wake, wengi wakimpongeza kwa kurudi kwenye muziki na wengine wakingojea kuona kama wimbo huo utadhihirisha hadhi ya kifahari na mafanikio anayojigamba nayo. Mashabiki na wadau wa muziki sasa wanasubiri kwa hamu ujio wa “Bibi Ya Tajiri”, ambao unatarajiwa kuwa mwanzo mpya wa safari ya Diana katika tasnia ya burudani.

Read More
 Mungai Eve Akanusha Taarifa za Kujutia Kuachana na Director Trevor

Mungai Eve Akanusha Taarifa za Kujutia Kuachana na Director Trevor

Content creator maarufu wa mtandaoni, Mungai Eve, amekanusha vikali madai yanayosambaa mtandaoni kuwa anajutia uamuzi wake wa kuachana na mpenzi wake wa zamani, Director Trevor. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mungai Eve amesema taarifa hizo ni za uongo na hazina ukweli wowote. Alibainisha kuwa hajawahi kutoa kauli yoyote inayodai kuwa anapitia msongo wa mawazo au kuhisi upweke kufuatia kuvunjika kwa uhusiano huo. Kauli yake imekuja baada ya mitandao ya kijamii, hususan X (zamani Twitter), kusheheni madai kwamba Mungai Eve amekuwa akikosa amani ya moyo na kujuta kuachana na Trevor, ambaye kwa muda mrefu walikuwa pamoja kama wapenzi na washirika wa kazi za uundaji maudhui. Mungai Eve kwa sasa anaendelea na shughuli zake za kimaudhui mtandaoni, huku akiwataka mashabiki wake kupuuza habari za kupotosha zinazolenga kudhoofisha taswira yake.

Read More
 Cardi B Aondolewa Mashtaka ya Shambulio na Ubaguzi

Cardi B Aondolewa Mashtaka ya Shambulio na Ubaguzi

Rapa maarufu wa Marekani, Cardi B, amekutwa hana hatia katika kesi ya madai yaliyofunguliwa na mlinzi wake wa zamani wa usalama, Emani Ellis. Ellis alikuwa amemshataki Cardi B kwa madai ya kumshambulia kwenye ofisi ya daktari wa wanawake huko Beverly Hills mwaka 2018. Mlinzi huyo alidai Cardi alimshambulia, kumtemea mate, na kumtolea maneno ya ubaguzi wa rangi, na kuomba fidia ya $24 milioni (takriban Ksh bilioni 3.1). Hata hivyo, ushahidi uliotolewa na mashahidi waliokuwa kliniki hiyo ulikanusha madai ya Ellis. Majaji wakachunguza ushahidi huu na hatimaye wakamua kusimama na Cardi B, wakimkuta hana hatia. Akizungumza nje ya mahakama, Cardi B amesema kuwa atapambana na mtu yeyote atakayefungua shauri la uongo dhidi yake, akionya kuwa safari hii mhusika atalazimika kugharamia uharibifu wowote atakaomsababisha. Cardi B pia alisisitiza kuwa kesi hii ilikuwa njama ya kutaka pesa, na alieleza kuwa hana hofu ya kudai haki yake mbele ya sheria. Uamuzi huu unamruhusu Cardi B kuendelea na maisha yake bila kuingiliwa na masuala ya kisheria yanayohusiana na tukio hilo la zamani, huku akiwakilisha mfano wa kushikilia haki binafsi na usalama wa heshima.

Read More
 Cardi B Amwaga Hasira kwa Paparazzi Mbele ya Kamera

Cardi B Amwaga Hasira kwa Paparazzi Mbele ya Kamera

Rapa maarufu wa Marekani, Cardi B, amekumbana na hali ya kutoelewana na paparazzi jana, akiwa nje ya Mahakama ya Alhambra, California. Paparazzi huyo aliuliza swali lisilo na adabu linalohusiana na uhusiano wake na mchezaji wa NFL, Stefon Diggs, mpenzi wake wa sasa, na pia aliyekuwa mume wake, Offset, ambaye hivi karibuni alionekana kujigamba kuhusu ujauzito wa mtoto wao wa nne. Cardi B, akiwa ameshtuka na kushikwa na hasira, alionyesha kukerwa kwake kwa kumnyanganya shabiki kalamu na kisha kumrushia paparazzi huyo. Rapa huyo aliweka wazi kuwa paparazzi wanapaswa kuwa na adabu na kumheshimu, akisisitiza kuwa wanawake wanastahili heshima wanapoulizwa maswali yenye hofu kama hayo. Hali hii imeonesha mara nyingine tena jinsi Cardi B anavyolinda maisha yake binafsi na jinsi anavyoshughulikia maswali yasiyo na heshima kutoka kwa waandishi wa habari.

Read More
 Morocco na Misri Karibu na Tiketi ya Kombe la Dunia

Morocco na Misri Karibu na Tiketi ya Kombe la Dunia

Morocco na Misri zina nafasi kubwa ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026, kufuatia mwenendo wao mzuri katika mechi za kufuzu zinazoendelea barani Afrika. Mashindano haya ya kufuzu, yaliyoanza mwezi Novemba 2023, yanatarajiwa kukamilika mwezi ujao, huku raundi nne muhimu zikiwa zimebaki. Katika mfumo wa kufuzu wa Afrika, ni washindi wa makundi tisa pekee watakaopata nafasi ya moja kwa moja ya kushiriki fainali hizo zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico. Timu nyingine nne bora zitakazomaliza katika nafasi ya pili zitapata nafasi ya pili kupitia mchujo wa mabara unaotarajiwa kuchezwa Novemba mwaka huu. Misri na Morocco, ambazo zimekuwa na kampeni imara hadi sasa, huenda zikajikatia tiketi zao moja kwa moja kabla ya raundi ya mwisho, iwapo zitapata ushindi katika mechi zao za wiki hii. Ushindi huo utazifanya ziendelee kuongoza makundi yao kwa tofauti ya alama isiyoweza kufikiwa na wapinzani wao katika mechi zilizobaki. Timu nyingine kama Cape Verde, Comoro na Sudan bado zina nafasi ya kufuzu, japo zinahitaji ushindi katika mechi zao zilizosalia. Kwa upande mwingine, Nigeria, ambayo ni moja ya mataifa yaliyotarajiwa kufanya vizuri, inakumbwa na presha kubwa na huenda ikaondolewa mapema ikiwa haitarejea kwenye mstari wa ushindi.

Read More
 Dyana Cods Atetea Wasanii Kuhusu Malipo Kutoka Serikalini

Dyana Cods Atetea Wasanii Kuhusu Malipo Kutoka Serikalini

Mwanamuziki wa Kenya, Dyana Cods, amejibu lawama zinazowakumba wasanii wanaofanya maonyesho kwenye hafla za serikali na kulipwa kwa kazi zao. Kundi la wakosoaji limekuwa likidai kwamba hatua ya wasanii kushiriki katika hafla hizo ni sawa na kuunga mkono serikali ya Rais William Ruto, hali ambayo imewafanya baadhi ya wananchi kuwataka wasanii wasipokee malipo hayo. Kwa mujibu wa Dyana Cods, mtazamo huo ni wa kupotosha kwani sanaa ni taaluma kama nyingine, na msanii anayelipwa na serikali hastahili kuhusishwa moja kwa moja na masuala ya kisiasa. Hitmaker huyo wa Set It, amesisitiza kuwa walimu, madaktari na kazi nyingine pia hulipwa na serikali bila kulaumiwa, hivyo ni upotoshaji kuona malipo ya wasanii yakigeuzwa kuwa ajenda ya kisiasa. Aidha, amesema wasanii wanachangia pakubwa katika burudani, kukuza utamaduni na kuimarisha taswira ya taifa, hivyo hawapaswi kubezwa wala kuhusishwa moja kwa moja na siasa kwa sababu ya kazi yao. Kauli yake imekuja wakati ambapo kumekuwa na maoni tofauti kuhusu nafasi ya wasanii kwenye hafla za kitaifa. Wapo wanaoamini kuwa fedha za umma zinapaswa kuelekezwa zaidi kwenye sekta za kijamii, huku wengine wakisisitiza kuwa wasanii pia ni wataalamu wanaostahili kulipwa kwa kazi zao kama walivyo wataalamu wengine.

Read More