Lulu Diva Akanusha Tuhuma za Kutelekezwa na Kevin, Ex wa Hamisa Mobetto

Lulu Diva Akanusha Tuhuma za Kutelekezwa na Kevin, Ex wa Hamisa Mobetto

Msanii wa Bongo Fleva, Lulu Diva, ameibuka na kufafanua kuhusu madai ya mitandaoni yanayodai kuwa ametekelezwa kimapenzi na mfanyabiashara wa Togo, Kevin Sowax, ambaye pia ni ex wa mwanamitindo Hamisa Mobetto. Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti, Lulu Diva alisema hajawahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Kevin, wala kusafiri kwenda China kama inavyodaiwa. Alisema taarifa hizo zimemshangaza kwani hazina ukweli wowote na ni kama hadithi anazosikia kuhusu maisha yake, ambazo hata yeye huzisikia kutoka kwa watu. “Yaani hii ndiyo ile hali ya kusikia habari zako ikiwa hata wewe huzijui. Nimesikia minong’ono mingi kuhusu kutelekezwa sijui China. Mimi sijawahi kusema Kevin ni mpenzi wangu, wala sijawahi kwenda China. Hakuna kitu kama hicho bwana,” alisema Lulu Diva. Kuhusu kuwahi kuonekana hadharani akiwa na Kevin, Lulu Diva alisema hawezi kukataa kuwa waliwahi kuonekana pamoja, lakini hilo halimaanishi walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi. “Sikatai kama nimeonekana na Kevin pamoja, lakini hiyo si sababu ya kuhusishwa moja kwa moja na uhusiano. Sitaki hata kulizungumzia hilo kwa undani. Cha kuelewa ni kwamba siwezi kutelekezwa,” alisema kwa msisitizo. Msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya ‘Kipenseli’, alisema angetamani mashabiki wake waelekeze nguvu kwenye kazi zake za sanaa badala ya kushiriki kusambaza taarifa zisizo na msingi. “Naombeni mniache niko bize na Kipenseli. Naombeni sapoti ya kazi yangu,” aliongeza. Kwa miezi ya hivi karibuni, Lulu Diva amekuwa akitajwa mara kwa mara kwenye tuhuma za kimapenzi mitandaoni, hasa baada ya ripoti kuibuka kwamba anahusiana na Kevin, miezi michache baada ya mfanyabiashara huyo kuachana rasmi na Hamisa Mobetto mnamo Aprili mwaka huu.

Read More
 Jovial Afunguka Sababu ya Kutoanika Mtoto Wake Mitandaoni

Jovial Afunguka Sababu ya Kutoanika Mtoto Wake Mitandaoni

Mwanamuziki maarufu wa Kenya, Jovial, amefunguka kuhusu uamuzi wake wa kutoweka sura au jina la mtoto wake kwenye mitandao ya kijamii. Kupitia ukurasa wake wa Instastori, Jovial alisema kuwa hatua hiyo ni njia yake ya kumlinda mtoto wake dhidi ya madhara ya maneno na mitazamo hasi inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii. Alisisitiza kuwa, kama mzazi, jukumu lake la kwanza ni kuhakikisha usalama na utulivu wa mtoto wake. Kauli yake ilikuja baada ya shabiki mmoja kumuuliza kwa nini hadi sasa hajawahi kushirikisha mashabiki taarifa zozote kumhusu mtoto wake, tofauti na mastaa wengine ambao huanika familia zao hadharani. Jovial ameungana na orodha ya wasanii na watu mashuhuri ambao huchagua kutokuweka wazi maisha ya watoto wao, wakiamini kuwa faragha ni kinga muhimu katika ulimwengu wa kidijitali wenye changamoto nyingi.

Read More
 Shalikido Afafanua Sababu za Kutoridhishwa na Ushauri wa Terence Creative

Shalikido Afafanua Sababu za Kutoridhishwa na Ushauri wa Terence Creative

Msanii wa Gengetone, Shalikido, amemkashifu mchekeshaji maarufu Terence Creative kwa kutoa ushauri kwa wasanii kuwekeza miradi mingine kando na muziki wakati anapitia changamoto kubwa za kifedha. Shalikido, ambaye hivi karibuni alijitokeza hadharani kuomba msaada wa kifedha, alisema ushauri wa Terence ulitolewa wakati usiofaa na haukuzingatia hali halisi ya matatizo aliyokuwa akikumbwa nayo. Alisisitiza kuwa mtu anapokumbwa na changamoto za kifedha, si rahisi kupokea ushauri wa namna hiyo bila kuelewa muktadha wa maisha yake na changamoto anazokabiliana nazo. Shalikido ameonyesha wazi kuwa badala ya kutoa maelekezo au ushauri usioeleweka, ni vyema kutoa msaada wa moja kwa moja au kuelewa hali ya mtu kabla ya kutoa mapendekezo. Kauli ya Shalikido imekuja siku chache baada ya Terence Creative kuwahimiza wasanii kupanga mikakati ya baadaye kwa kuwekeza katika miradi tofauti, akisisitiza kuwa maisha ya kuwa msanii si ya kudumu milele na kuwa kuna wakati uwezo wao wa kung’ara jukwaani utaisha.

Read More
 Geoffrey Mosiria Atoa Wito wa Msamaha Kati ya Director Trevor na Eve Mungai

Geoffrey Mosiria Atoa Wito wa Msamaha Kati ya Director Trevor na Eve Mungai

Mchambuzi wa masuala ya mitandaoni, Geoffrey Mosiria, ametoa rai kwa Director Trevor kumsaamehe na kumsaidia aliyekuwa mpenzi wake, Eve Mungai, akisisitiza kuwa wawili hao wanapaswa kuzingatia maisha ya sasa na mipango ya baadaye, badala ya kuzidi kushikilia yaliyopita Kupitia mitandao yake ya kijamii, Mosiria amesema kuwa lawama na kejeli zinazotokana na habari za uongo mitandaoni haziwezi kusaidia chochote, bali ni busara wawili hao waweke kando tofauti zao na kuendelea mbele. Kwa kutoa wito wake, Mosiria amesema mashabiki wanapaswa kutambua kuwa maisha binafsi ya wasanii na wanaburudishaji ni sehemu ya safari zao, na kwamba ni vyema kuunga mkono badala ya kuongeza shinikizo kupitia habari zisizo sahihi. Mosiria alitoa kauli hiyo baada ya posti mbili feki kusambaa mitandaoni na kuibua mjadala kuhusu uhusiano wa wawili hao. Katika moja ya posti hizo bandia, ilidaiwa kuwa Mungai amemuomba radhi Trevor na kutaka warudiane, huku nyingine ikimnukuu akijutia uamuzi wa kuachana naye na kuwaonya mashabiki dhidi ya ushauri mbaya wa mtandaoni.

Read More
 Mulamwah Atambulisha Emillianah Mwikali Kama Mpenzi Wake Mpya

Mulamwah Atambulisha Emillianah Mwikali Kama Mpenzi Wake Mpya

Mchekeshaji na msanii wa Kenya, Mulamwah, ametambulisha rasmi Emillianah Mwikali, maarufu kama Instagram model, kama mpenzi wake mpya. Hii inajiri takribani miezi minne tu baada ya kutangaza kuachana na aliyekuwa mchumba wake, Ruth K. Kupitia mitandao ya kijamii, Mulamwah alichapisha picha zikimuonesha akiwa na Mwikali ndani ya Mercedes Benz S-Class yake ya thamani ya takribani KSh milioni 8. Aidha, alionyesha picha ya karibu ya mkono wake uliochorwa tattoo yenye maandishi “Blessed,” ambayo mashabiki waliitambua mara moja kama alama ya Mwikali. Hatua ya Mulamwah imeibua mjadala miongoni mwa mashabiki, wengine wakimpongeza kwa kurudi kwenye maisha ya mapenzi huku wengine wakionyesha mshangao kutokana na hatua yake ya haraka kuanza ukurasa mpya. Hadi sasa, wawili hao hawajatoa maelezo zaidi kuhusu safari yao ya kimapenzi, lakini picha na ujumbe wa Mulamwah umeonekana kuthibitisha rasmi uhusiano wao.

Read More
 Zuchu Akanusha Madai ya Kupuuzwa Kasarani Wakati wa Fainali za CHAN

Zuchu Akanusha Madai ya Kupuuzwa Kasarani Wakati wa Fainali za CHAN

Msanii kutoka Tanzania, Zuchu, amejitokeza na kukanusha vikali madai kwamba alipuuziwa na mashabiki wakati wa onyesho lake katika Uwanja wa Kasarani, wakati wa fainali za mashindano ya CHAN kati ya Morocco na Madagascar. Ripoti zilizosambaa mitandaoni zilisema kuwa baadhi ya mashabiki waliokuwepo uwanjani walionekana kuimba wimbo wa taifa la Kenya wakati Zuchu alipokuwa akiendelea na maonesho jukwaani, hali iliyotafsiriwa na baadhi ya watumiaji wa mitandao kama ishara ya kutompa usikivu au heshima anayostahili. Kupitia mitandao ya kijamii, hususan Instagram, Zuchu alikanusha madai hayo akisisitiza kuwa video zilizozagaa mtandaoni zimehaririwa kwa nia ovu ya kueneza taarifa potofu. Alieleza kuwa onyesho hilo lilirushwa moja kwa moja (live) na linapatikana kwa ukamilifu kwenye YouTube, hivyo kama tukio hilo lingetokea kweli, lingeonekana bayana kwenye rekodi ya moja kwa moja. Hitmaker huyo wa Amanda ameendelea kusisitiza kuwa mafanikio ya kazi yake hayawezi kutikiswa na kauli za watu wachache mitandaoni, kwani chapa yake inasimamiwa na juhudi, maombi, na mashabiki wake wa kweli walioko ndani na nje ya Tanzania. Tukio hilo, ambalo lilidaiwa kutokea wakati wa mechi kubwa ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), limezua mjadala mitandaoni huku baadhi ya mashabiki wakimtetea vikali Zuchu, wakisema alitoa burudani ya hali ya juu licha ya kelele za mtandaoni.

Read More
 Oga Obinna Amuinua Shalikido Kwa Msaada wa Kifedha na Ajira Mpya

Oga Obinna Amuinua Shalikido Kwa Msaada wa Kifedha na Ajira Mpya

Mtangazaji maarufu na mchekeshaji Oga Obinna, amejiunga na orodha ya mastaa ambao wameamua kumsaidia msanii wa muziki wa Gengetone, Shalikido, ambaye hivi karibuni aliomba umma imsaidie kutokana na maisha kumuendea vibaya. Katika hatua ya kuonyesha upendo na mshikamano kwa wasanii wachanga, Oga Obinna ameamua kumpa Shalikido kazi ya mwaka mmoja kama mshawishi wa mitandaoni (influencer), akimwahidi nafasi ya kukuza kipato chake kupitia majukwaa ya kidijitali. Obinna pia ametoa zawadi za vifaa vya nyumbani kwa Shalikido ikiwemo sofa, godoro na zulia, hatua iliyochukuliwa kama ishara ya kumuwezesha kuanza maisha mapya kwa ustawi na heshima. Zaidi ya hayo, kupitia kipindi chake cha moja kwa moja (live show) kwenye YouTube, Oga Obinna alifanikiwa kuchangisha kiasi cha KSh 62,000 kwa ajili ya kumsaidia msanii huyo kijana. Michango hiyo ilitoka kwa wafuasi wake walioguswa na hali ya Shalikido na waliotaka kuona maisha yake yakibadilika. Hatua hii ya Oga Obinna imepongezwa na wengi kama mfano bora wa usaidizi wa kijamii na kuinua vipaji vya vijana, hasa wale wanaokumbwa na changamoto za kiuchumi. Hatua hii ya Obinna inakuja siku chache tu baada ya mchekeshaji mwingine maarufu, Eric Omondi, kumsaidia Shalikido kwa kumpatia pikipiki mpya na mahitaji mengine muhimu ya nyumbani. Msaada huo ulitolewa baada ya Shalikido kufunguka hadharani kuhusu hali ngumu ya maisha aliyokuwa akipitia, hali iliyomlazimu kushindwa hata kumudu mahitaji ya msingi ya familia yake.

Read More
 Instagram Yazindua Kipengele Kipya cha Folders Katika DM

Instagram Yazindua Kipengele Kipya cha Folders Katika DM

Instagram imeanza kuweka sehemu mpya inayowezesha watumiaji kuongeza folders katika upande wa ujumbe wa moja kwa moja (DM). Hatua hii inalenga kurahisisha upangaji na upatikanaji wa ujumbe, hasa kwa wale wanaopokea jumbe nyingi kila siku. Kupitia maboresho haya, watumiaji sasa wanaweza kutenganisha jumbe kwa urahisi kulingana na makundi tofauti. Mfano, mtu anaweza kutenganisha jumbe za waliyojibu kupitia Instagram Stories, kuweka tofauti kati ya jumbe kutoka kwa Followers na wale ambao si Followers, kutenga jumbe za kibiashara, pamoja na jumbe kutoka kwa akaunti zilizo na alama ya kuthibitishwa (verified). Kipengele hiki kinatarajiwa kuwasaidia sana wafanyabiashara, wabunifu wa maudhui na watumiaji wenye ufuasi mkubwa ambao mara nyingi hukumbwa na changamoto ya kusimamia mawasiliano mengi kwa wakati mmoja. Kwa sasa Instagram inalisambaza kipengele hiki hatua kwa hatua, na katika muda mfupi ujao watumiaji wote duniani wataweza kufurahia urahisi huu mpya wa kusimamia ujumbe wao.

Read More
 Ryan Ogam Ajiunga na Wolfsberger AC ya Austria

Ryan Ogam Ajiunga na Wolfsberger AC ya Austria

Mshambulizi wa Harambee Stars Ryan Ogam amekamilisha uhamisho wake kujiunga na kilabu cha Wolfsberger AC cha Austria kutoka kilabu cha Tusker FC kinachoshiriki katika ligi kuu ya FKF. Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 20, ambaye alijipatia umaarufu kwa kufunga mabao mawili kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024, atajiunga na wachezaji wenzake wapya baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa. Ogam alikuwa mmoja wa wachezaji bora wa Ligi Kuu ya FKF msimu uliopita, ambapo alifunga mabao 15 katika mechi 17 pekee za Tusker FC. Wolfsberger, ambayo ilimaliza katika nafasi ya nne katika ligi ya Bundesliga ya Austria msimu uliopita, imemsajili mshambulizi huyo ili kuboresha safu yao ya ushambulizi. Uhamisho wake unaashiria sura mpya katika taaluma yake ya soka, na kumpa jukwaa jipya la kujipima nguvu katika soka la bara Ulaya.

Read More
 Wimbo wa “Chinje” wa Toxic Lyrikali Waweka Historia Youtube

Wimbo wa “Chinje” wa Toxic Lyrikali Waweka Historia Youtube

Rapa anayekuja kwa kasi nchini Kenya, Toxic Lyrikali, ameandika historia baada ya wimbo wake “Chinje” kufikisha views milioni 10 kwenye mtandao wa YouTube ndani ya kipindi cha miezi tisa tangu uachiwe rasmi. Takwimu hizi zimempa nafasi kubwa katika muziki wa Afrika Mashariki, zikimuweka kwenye ramani kama moja ya vipaji vipya vinavyoibuka kwa nguvu. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Toxic Lyrikali ametoa shukrani kwa mashabiki wake wote waliomuunga mkono, akisisitiza kuwa mafanikio hayo yasingewezekana bila upendo na uaminifu wao. Aidha, ameahidi kuendelea kuwapa mashabiki wake ngoma kali zaidi katika siku zijazo. Wimbo “Chinje” umekuwa gumzo kwa mashabiki kutokana na midundo yake ya kipekee na ujumbe unaoendana na ladha ya muziki wa kizazi kipya. Wachambuzi wa muziki wanaona mafanikio haya kama kielelezo cha jinsi wasanii wapya wanavyoweza kufika mbali kwa kutumia mitandao ya kijamii na majukwaa ya kidijitali.

Read More
 Zari Amshauri Mumewe Shakib Aachane na Masumbwi Baada ya Kipigo

Zari Amshauri Mumewe Shakib Aachane na Masumbwi Baada ya Kipigo

Socialite maarufu wa Uganda, Zari Hassan, ameripotiwa kumshauri mumewe Shakib Cham kuachana na mchezo wa masumbwi na kuelekeza nguvu zake katika shughuli nyingine za kibinafsi zinazoweza kumuingizia kipato. Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na wawili hao, Zari amekuwa mstari wa mbele kushauri mumewe kutokana na hali iliyoonekana baada ya pambano la hivi karibuni lililomshirikisha Shakib na msanii Rickman Manrick. Katika pambano hilo, Shakib alipokea makonde mazito ya kichwa yaliyopelekea kuanguka chini na kupoteza fahamu, hali iliyomlazimu muamuzi kusitisha pambano hilo mara moja. Tukio hilo lilimuumiza mno Zari ambaye alishuhudia mumewe akizirai ulingoni na kulia machozi ya uchungu. Chanzo hicho kimeeleza kuwa, licha ya juhudi za Shakib kujaribu kujiweka kwenye tasnia ya masumbwi ya burudani, mchezo huo haujaweza kuleta mapato yaliyotarajiwa na badala yake umekuwa chanzo cha hofu na maumivu kwa familia.

Read More
 Keranta Awatolea Uvivu Wakosoaji Wake Kuhusu Video ya Jaba

Keranta Awatolea Uvivu Wakosoaji Wake Kuhusu Video ya Jaba

Content creator kutoka Kenya, Keranta, ameibuka na kuwatolea uvivu wakosoaji wake baada ya video yake ikimuonesha akitafuna jaba kusambaa mitandaoni. Video hiyo ilisababisha gumzo kubwa, ambapo baadhi ya watu walimkosoa wakidai haifai kwa mwanamke kujihusisha na jaba ikizingatiwa kuwa asilimia kubwa ya watu wanaotumia ni wanaume. Kupitia instastory, mrembo huyo amepuuza ukosoaji huo na kueleza kuwa kila mtu ana uhuru wa kujiburudisha anavyotaka. Lakini pia amekanusha dhana kwamba matajiri hawatumii jaba, akibainisha kuwa hata watu wenye uwezo kifedha katika maeneo ya Pwani wanajihusisha nalo. Jaba, ni majani ya mmea Catha edulis yanayotafunwa kwa burudani. Yana kemikali ya cathinone inayomfanya mtumiaji kuwa macho na mchangamfu, ingawa matumizi yake ya muda mrefu yanaweza kusababisha madhara kiafya na utegemezi.

Read More