Gossip

Mulamwah Atambulisha Emillianah Mwikali Kama Mpenzi Wake Mpya

Mulamwah Atambulisha Emillianah Mwikali Kama Mpenzi Wake Mpya

Mchekeshaji na msanii wa Kenya, Mulamwah, ametambulisha rasmi Emillianah Mwikali, maarufu kama Instagram model, kama mpenzi wake mpya. Hii inajiri takribani miezi minne tu baada ya kutangaza kuachana na aliyekuwa mchumba wake, Ruth K.

Kupitia mitandao ya kijamii, Mulamwah alichapisha picha zikimuonesha akiwa na Mwikali ndani ya Mercedes Benz S-Class yake ya thamani ya takribani KSh milioni 8. Aidha, alionyesha picha ya karibu ya mkono wake uliochorwa tattoo yenye maandishi “Blessed,” ambayo mashabiki waliitambua mara moja kama alama ya Mwikali.

Hatua ya Mulamwah imeibua mjadala miongoni mwa mashabiki, wengine wakimpongeza kwa kurudi kwenye maisha ya mapenzi huku wengine wakionyesha mshangao kutokana na hatua yake ya haraka kuanza ukurasa mpya.

Hadi sasa, wawili hao hawajatoa maelezo zaidi kuhusu safari yao ya kimapenzi, lakini picha na ujumbe wa Mulamwah umeonekana kuthibitisha rasmi uhusiano wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *