Shalkido Apata Msaada Kutoka kwa Eric Omondi

Shalkido Apata Msaada Kutoka kwa Eric Omondi

Mchekeshaji maarufu Eric Omondi ameonyesha moyo wa kusaidia baada ya kujitokeza kumsaidia msanii wa Gengetone, Shalkido, ambaye hivi karibuni alifichua kuwa maisha yamekuwa magumu kiasi cha kushindwa kumudu mahitaji ya familia yake. Mchekeshaji huyo amemkabidhi Shalkido pikipiki mpya pamoja na mahitaji ya nyumbani ikiwemo unga, sukari na mafuta ya kupikia. Kupitia msaada huo, Eric amesema lengo lake ni kuhakikisha msanii huyo anapata fursa ya kujiinua na kujitegemea tena. Shalkido, anayejulikana zaidi kupitia kundi la Sailors, amepokea msaada huo kwa furaha na shukrani, akisema utampa nafasi ya kurudia katika mstari sahihi wa kujikimu kimaisha. Kitendo cha Eric kimepongezwa na mashabiki wengi mitandaoni wakimtaja kuwa mfano wa kuigwa kwa wasanii wengine na jamii kwa ujumla.

Read More
 S2kizzy Amporomoshea Matusi Hussen Machozi

S2kizzy Amporomoshea Matusi Hussen Machozi

Mtayarishaji wa muziki wa Bongo Fleva, S2kizzy, ameimtolea maneno makali mwanamuziki Hussen Machozi, akimuita mpumbavu. Akipiga stori na East Africa Radio, mtayarishaji huyo amesema hana sababu ya kushirikiana naye kimuziki ikizingatiwa kuwa nyimbo zake zimepitwa na wakati. S2kizzy anayejulikana kwa jina la utani Zombie amemchana vikali Machozi na kutamka wazi kuwa hamheshimu huku akimshauri msanii huyo kutafuta njia nyingine za kuendeleza muziki wake. Kauli ya S2kizzy imeibuka kufuatia madai ya Hussen Machozi, aliyelalamika kuwa mtayarishaji huyo hajawahi pokea simu zake licha ya kujitambulisha kwake mapema. Hussen alienda mbali zaidi na kuhoji kuwa juhudi zake za kuwasiliana na S2kizzy zimekuwa zikigonga mwamba, jambo lililomfanya kulalamikia kutothaminiwa.

Read More
 Willy Paul Akataa Pambano la Ndondi na Shakib, Amwaga Hasira Kwa Diamond

Willy Paul Akataa Pambano la Ndondi na Shakib, Amwaga Hasira Kwa Diamond

Msanii wa Kenya, Willy Paul, amekataa ombi la kushiriki pambano la ndondi na Shakib Khan, mume wa mfanyibiashara na socialite maarufu wa Uganda, Zari Hassan. Kwa mujibu wa Willy Paul, hana sababu ya kupigana na Shakib kwani ugomvi wake halisi upo na Diamond Platnumz, aliyewahi kuwa mpenzi wa Zari na baba wa watoto wake. Mkali huyo wa ngoma ya Ahere, ameeleza kwamba hana mpango wa kugeuza masuala ya kifamilia kuwa kiki za ndondi, bali anaona changamoto hiyo haina msingi kwake. Kauli ya msanii huyo inakuja mara baaada ya Shakib kuwapa wasanii wa Kenya changamoto ya kuingia naye ulingoni kama njia ya kuonesha kuwa bado ana nguvu licha ya kichapo alichopokea Uganda hadi akapoteza fahamu.

Read More
 Zuchu: Ashurey Ndiye Dansa Namba Moja Afrika Mashariki

Zuchu: Ashurey Ndiye Dansa Namba Moja Afrika Mashariki

Staa wa Bongo Fleva, Zuchu, amempa nyota tano dansa wake maarufu Ashurey akimtaja kuwa ndiye Dansa bora namba moja Afrika Mashariki kwa sasa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zuchu alipakia video ya Ashurey akifanya challenge ya wimbo wake mpya “Inama”, kisha akaandika ujumbe wa kumpa heshima kubwa kwa umahiri wake wa kucheza. Wakati mashabiki wake wakiendelea kufurahia wimbo wake maarufu “Amanda”, Zuchu ametangaza kuwa yupo mbioni kuachia rasmi wimbo mpya uitwao “Inama”, akidai kuwa utafunika hata mafanikio ya hitsong yake, “Sukari”, ambayo imepata streams na views nyingi kwenye majukwaa ya kidigitali. Tangazo hili limeongeza hamasa kwa mashabiki wake kote Afrika Mashariki, ambao sasa wanasubiri kwa shauku kuona iwapo “Inama” itavunja rekodi na kufikia viwango vikubwa zaidi ya nyimbo zake zilizopita.

Read More
 Arrow Bwoy Akubali Changamoto ya Ndondi kutoka kwa Shakib Khan

Arrow Bwoy Akubali Changamoto ya Ndondi kutoka kwa Shakib Khan

Msanii wa Kenya, Arrow Bwoy, amekubali changamoto ya pambano la ngumi kutoka kwa Shakib Cham, mume wa sosholaiti Zari Hassan. Hii inajiri siku moja tu baada ya Shakib kupokea kichapo cha mbwa kwa knockout na msanii wa Uganda, Rickman Manrick. Kupitia ujumbe wake, Arrow Bwoy amemjibu Shakib kwa kejeli, akimtaka ajitayarishe ipasavyo endapo pambano hilo litatimia. Hata hivyo, amemtahadharisha Shakib asije akamleta mkewe Zari kwenye ukumbi wa pambano, akisema huenda akazimia kwa aibu baada ya mume wake kushindwa. Kauli ya msanii huyo inakuja mara baaada ya Shakib kuwapa wasanii wa Kenya changamoto ya kuingia naye ulingoni kama njia ya kuonesha kuwa bado ana nguvu licha ya kichapo alichopokea Uganda hadi akapoteza fahamu.

Read More
 Diamond Awataka Watanzania Waache Lawama kwa Serikali

Diamond Awataka Watanzania Waache Lawama kwa Serikali

Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ameibua gumzo baada ya kuwatolea uvivu watu wanaoendelea kulalamikia serikali kuhusu hali ya maisha. Kupitia ujumbe wake, Diamond amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuongeza bidii kwenye kazi zao badala ya kuishia kuilaumu serikali kila mara. Hitmaker huyo wa Mtasubiri ameongeza kuwa changamoto za maisha ni za kawaida, na anayejituma hupata matunda yake bila kujali nani yupo madarakani. Diamond, ambaye mara nyingi hujitokeza kuzungumzia masuala ya kijamii, amesema ataendelea kuwatia moyo vijana kufanya kazi kwa bidii na kutumia vipaji vyao ipasavyo ili kuondokana na utegemezi. Kauli hiyo imezua mjadala mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakimuunga mkono kwa kusema ujumbe huo ni wa kuhamasisha, huku wengine wakihisi amewabeza wananchi wanaopitia ugumu wa maisha.

Read More
 Zari Hassan Aangua Kilio Baada ya Shakib Kupigwa Knockout na Rickman

Zari Hassan Aangua Kilio Baada ya Shakib Kupigwa Knockout na Rickman

Mfanyibiashara na sosholaiti maarufu, Zari Hassan, alijikuta akibubujikwa na machozi baada ya mumewe, Shakib Cham, kupigwa knockout vibaya na msanii Rickman Manrick katika pambano la masupastaa lililoshuhudiwa usiku wa Jumamosi, 30 Agosti 2025, ndani ya MTN Arena, Lugogo. Pambano hilo lililokuwa limevuta maelfu ya mashabiki lilimalizika mapema katika raundi ya pili, baada ya Rickman kumshushia Shakib ngumi nzito pande zote za kichwa na kumwangusha chini akipoteza fahamu. Umati ulilipuka kwa shangwe, lakini macho yote yalihamia moja kwa moja kwa Zari, aliyekuwa safu ya mbele, akishuhudia mume wake akizimwa ringini. Awali, Zari alionekana akishangilia kwa nguvu akimhimizia mumewe kupambana, lakini alibadilika ghafla na kuangua kilio mara tu Shakib alipoanguka chini bila msaada. Alimkimbilia ulingoni, akimshika na kumfariji huku akibubujikwa na machozi, jambo lililoacha taswira ya aibu mbele ya umati na kamera zilizokuwa zikirekodi kila tukio. Mitandaoni, mashabiki hawakuchelewa kumrushia vijembe, wakimuita “First Lady wa Knockout”, huku wengine wakisema “hata machozi ya Zari hayawezi kufuta aibu ya kipigo cha Shakib.” Wengine walimkejeli kuwa safari hii si biashara zake wala mitindo yake ya kifahari iliyokuwa gumzo, bali machozi yake ringini. Rickman kwa upande wake aliendeleza rekodi yake ya ushindi, akipata ushindi wa pili katika michezo ya masupastaa baada ya kumbwaga pia msanii Grenade Official mnamo Desemba 2024. Kwa Shakib na Zari, pambano hili limeacha kumbukumbu chungu, knockout kwa ulingo, na machozi kwa jukwaa la mbele.

Read More
 Azziad Amchana Madollar Mapesa Kuhusu Deni la Milioni 3

Azziad Amchana Madollar Mapesa Kuhusu Deni la Milioni 3

Mrembo wa mitandao na mtangazaji maarufu, Azziad Nasenya, ameibua mjadala baada ya amemuanika hadharani kijana anayejulikana kama Madollar Mapesa, kufuatia madai kwamba anamdai shilingi milioni 3. Katika sauti ya simu iliyovuja mtandaoni, Azziad alisikika akimuuliza Madollar sababu za kusambaza taarifa za uongo, akisisitiza kuwa tayari alimlipa fedha zote alizokuwa akimdai, ambazo ni jumla ya milioni 2.5. Katika mazungumzo hayo, Madollar alisikika akipatwa na kigugumizi kabla ya kuongeza madai ya shilingi laki tano akizotaja kama interest au riba ya deni lake. Kauli hiyo ilimkasirisha Azziad ambaye alimwonya vikali akome kutumia jina lake vibaya na kueneza madai yasiyo na msingi. Tukio hili limezua gumzo mitandaoni, huku mashabiki wengi wakimtetea Azziad na kumtaka Madollar kuthibitisha madai yake au kuomba radhi hadharani.

Read More
 Amber Ray na Rapudo Waonekana Pamoja Tena, Video Yazua Gumzo

Amber Ray na Rapudo Waonekana Pamoja Tena, Video Yazua Gumzo

Mastaa wa mitandaoni, Amber Ray na Kennedy Rapudo, wameendelea kuvutia macho ya mashabiki baada ya kuonekana pamoja tena wikiendi hii, licha ya uvumi uliokuwa umesambaa kwamba wameachana. Kupitia video inayosambaa mitandaoni, Rapudo anaonekana akiogelea na binti yake kwenye bwawa la kuogelea huku Amber Ray akionekana kando akifurahia tukio hilo kwa bashasha. Tukio hilo limewafanya mashabiki wengi kuhoji kama kweli wawili hao walikuwa wameachana au tetesi hizo zilikuwa ni uvumi tu. Hapo awali, taarifa zilienea kwamba kila mmoja tayari alikuwa ameingia kwenye mahusiano mapya na hata kudaiwa kuwa Amber Ray aliuza baadhi ya vifaa vya nyumba walivyokuwa wamenunua wakiwa pamoja na Rapudo. Lakini picha hii mpya ya pamoja imeonekana kupinga madai hayo, au angalau kuonesha kuwa wawili hao bado wana ukaribu wa kifamilia. Mashabiki mitandaoni wameendelea kutoa maoni mseto; wengine wakifurahishwa na kuona familia hiyo ikijumuika tena, huku wengine wakisisitiza kuwa huenda wawili hao wanadumisha urafiki kwa ajili ya binti yao. Hadi sasa, hakuna yeyote kati yao aliyetoa kauli rasmi kuthibitisha hali halisi ya mahusiano yao.

Read More
 Sosuun Atoa Somo kwa Mabinti Kuhusu Maisha Bila Watoto

Sosuun Atoa Somo kwa Mabinti Kuhusu Maisha Bila Watoto

Msanii maarufu wa Kenya, Sosuun, ameibua mjadala mkubwa baada ya kutoa ujumbe mzito unaolenga mabinti nchini kuhusu uamuzi wa kutokuwa na watoto. Kupitia video yake Instagram, Sosuun alisema kuwa kutokuwa na watoto kunaweza kuonekana kama uamuzi sahihi katika kizazi cha sasa, hasa kwa kuzingatia changamoto za mahusiano yasiyodumu na watoto kukosa malezi ya wazazi wote wawili. Hata hivyo, aliwaonya mabinti kutofanya maamuzi hayo kwa misingi ya mitindo inayotrend mitandaoni bila kujitafakari kwa undani. Sosuun alisisitiza kuwa maisha ya uzee huja na changamoto zake, ikiwemo kupoteza nguvu, maradhi, na kuhitaji msaada wa kihisia na kimwili. Katika wakati kama huo, familia na watoto mara nyingi huwa nguzo muhimu ya msaada. “Fikiria kwa kina kabla ya kuamua, usifanye kwa sababu kila mtu anafanya,” alisema Sosuun. Ujumbe huo umetajwa kama somo kwa mabinti nchini Kenya, wengi wakimpongeza msanii huyo kwa kuzungumza ukweli unaoangazia thamani ya familia na malezi, huku mjadala ukiendelea mitandaoni kuhusu uhuru wa maamuzi ya kibinafsi.

Read More
 Ogier Aandika Historia Ueno Rally del Paraguay

Ogier Aandika Historia Ueno Rally del Paraguay

Bingwa mara nane wa dunia katika mbio za magari za WRC, Sebastien Ogier, aliibuka mshindi wa mkondo wa Ueno Rally del Paraguay uliomalizika Jumapili usiku, na kuiweka kampuni ya Toyota kwenye ramani kwa mara nyingine tena. Ushindi huo ulimfanya Ogier kuifikisha Toyota jumla ya ushindi 102 kwenye historia ya mashindano ya WRC rekodi inayolingana na ile ya kampuni ya Citroen. Licha ya kukumbwa na changamoto kadhaa, hasa Ijumaa alipoteza takribani sekunde 40 baada ya gari lake kukosa pumzi kwenye gurudumu, Ogier aliweza kurejea kwa kishindo na kumaliza mbio akiwa kileleni. Huu ni ushindi wake wa 18 akiwa na Toyota, na kwa mafanikio haya, anakuwa dereva aliyeiletea kampuni hiyo ushindi mwingi zaidi akivunja rekodi aliyokuwa akiishikilia kwa pamoja na Kalle Rovanperä. Katika ushindani mkali wa mkondo huo, tatizo la gari kwenye awamu ya mwisho ya Wolf Power lilimwangusha Adrien Fourmaux, ambaye alishuka hadi nafasi ya nne. Nafasi ya pili ilichukuliwa na Elfyn Evans huku Thierry Neuville akifunga tatu bora kwa kumaliza katika nafasi ya tatu.

Read More
 Zuchu Akutana na Dada Anayemwigiza Kenya

Zuchu Akutana na Dada Anayemwigiza Kenya

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuchu, ameonyesha furaha na upendo wake baada ya kukutana ana kwa ana na pacha wake kutoka Kenya anayemwigiza. Binti huyo, ambaye mashabiki wanamuita “Zuchu wa Mchongo”, amejizolea umaarufu mitandaoni kutokana na kumwigiza Zuchu katika mitindo ya uchezaji na mavazi, sambamba na kufanya challenges za nyimbo zake. Kutokana na kufanana kwao kimuonekano, mara nyingi mashabiki huchanganyikiwa kumtambua nani ni nani. Katika video iliyosambaa, Zuchu alionekana akimkumbatia dada huyo kwa upendo na kumshukuru kwa namna anavyounga mkono kazi zake za muziki. Msanii huyo wa WCB alikiri wazi kwamba anamthamini na anafarijika kuona kazi zake zikileta nafasi ya kuibua vipaji vipya hata nje ya Tanzania. Mashabiki mitandaoni wamefurahishwa na ukaribu huo, wakibainisha kuwa ni jambo la kipekee kwa Zuchu kumtambua na kumpongeza mtu anayemwigiza badala ya kuona kama ni ushindani.

Read More