WIMBO WA C-KAY LOVE  NWANTITI WAONGOZA KWA STREAMS SPOTIFY

WIMBO WA C-KAY LOVE NWANTITI WAONGOZA KWA STREAMS SPOTIFY

Hitmaker wa ngoma ya Love Nwantiti C-kay ameendelea kufanya poa haswa upande wa streams katika mtandao mbalimbali ya kuuza na kusikiliza muziki duniani. Hii ni baada ya kufikisha zaidi ya wasikilizaji Million 17 ndani ya mwezi yaani monthly listeners katika mtandao wa Spotify. C-Kay anakuwa msanii wa kwanza kutoka barani Africa kufikisha jumla ya wasikilizaji hao millioni 17.4 ndani ya mwezi mmoja ,akiivunja rekodi ya mtu mzima burna boy mwenye wasikilizaji millioni 10.2 wa mwezi katika mtandao wa spotify.

Read More
 BRUNO K AMCHANA CINDY SANYU KWA KUSHINDWA KUWATETEA WASANII

BRUNO K AMCHANA CINDY SANYU KWA KUSHINDWA KUWATETEA WASANII

Mwanamuziki kutoka nchini uganda Bruno K amemtolea uvivu msanii mwenzake Cindy Sanyu hii ni baada ya msanii huyo kudai kwamba Bruno K alisaini mkataba na lebo ya muziki ya Black markert Records bila kuelewa mkataba wenyewe.   Akiwa kwenye moja ya interview Bruno K amesema madai ya Cindy ambaye ni rais wa chama cha wanamuziki nchini Uganda hayana msingi wote wote kwani kauli yake hiyo inaonyesha ni jinsi gani ameshindwa kuwatetea wasanii wanaonyanyaswa na lebo za muziki.   Bruno K kwa sasa anaendelea kushinikiza lebo ya muziki ya Black Market records impe channel yake ya youtube baada ya lebo hiyo kuchukua akaunti yake hiyo alipoigura lebo ya muziki ya Black Market  records.   Ikumbukwe juzi kati Cindy Sanyu aliwataka wasanii nchini uganda kuwa makini wanapotia sahihi mikataba na lebo za muziki kwani wengi wao wamekuwa wakifanya hivyo bila kuwashirikisha mawakili.            

Read More
 RINGTONE APEWA NOTISI YA SIKU 10 KUONDOKA KWENYE NYUMBA YAKE YA RUNDA

RINGTONE APEWA NOTISI YA SIKU 10 KUONDOKA KWENYE NYUMBA YAKE YA RUNDA

Mwànamziki wa nyimbo za injili nchini Ringtone Apoko amepewa makataa ya siku kumi kuondoka kwenye nyumba anayoishi mitaa ya Runda jijini Nairobi.   Kulingana na barua ya kampuni ya mawakili ya AGN Kamau Advocates,  nyumba ambayo ringtone anaishi ni ya raia wa Sweden kwa jina Mona Ingegard aliyefariki mwaka wa 2007 na Ringtone alinunua nyumba hiyo bila kufuata njia sahihi.   Hata hivyo Ringtone ambaye amekuwa akijinadi kwamba ni mwanamuziki utajiri afrika mashariki hajatoa tamko lolote kuhusiana madai yaliyoibuliwa na kampuni ya wanasheria ya AGN Kamau Advocates.    

Read More
 MADINI CLASSIC ATANGAZA KUHAMIA KWENYE MAPENZI YA JINSIA MOJA

MADINI CLASSIC ATANGAZA KUHAMIA KWENYE MAPENZI YA JINSIA MOJA

Mkali wa muziki nchini Madini Classic amewashangaza wadau wa muziki nchini baada ya kutangaza kwamba amekukumbatia mapenzi ya jinsia moja kwani amechoshwa na mapenzi kabisa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram amepost picha akiwa amejipodoa wanja, na lipstick kama mwanamke na kusema kwamba ameamua kuhamia mapenzi ya jinsia moja kwani siyo dhambi. Hitmaker huyo wa Toto la Kanairo amewaomba mashabiki wake kutomchukulia vibaya kwani ameumizwa sana kwenye mahusiano yake ya zamani hadi amekata tamaa kuanza mahusiano na wanawake. Hata hivyo mashabiki zake wameonekana kukerwa na kauli ya Madini Classic huku wengi wakimtaka atoe muziki mzuri badala ya kujihusisha na kiki zisizokuwa na msingi aachane na masuala ya kiki nmuziki kama ameshindwa kuipambania kazi

Read More
 VIDEO ZA OTILE BROWN ZAONDOLEWA YOUTUBE

VIDEO ZA OTILE BROWN ZAONDOLEWA YOUTUBE

Music Video za Staa wa muziki nchini otile brown zimeondolewa kwenye akaunti ya mtandao wa YouTube ya msanii huyo   Ukitembelea kwenye akaunti ya YouTube ya Otile Brown hutafanikiwa kuziona video za nyimbo kama Dusuma, Such Kinda Love, Chaguo La Moyo Wangu na Aiyana kutokana na kuondolewa na aliyezi-upload   Mpaka sasa haijafahamika sababu za kushushwa kwa video hizo za Otile Brown.   Chaguo la Moyo wangu na Dusuma ni video za muziki zenye watazamaji wengi zaidi kwenye mtandao wa YouTube nchini Kenya            

Read More
 COUNTRY BOY ADAI LEBO YA KONDE GANG IMEIPA HADHI MUZIKI WAKE

COUNTRY BOY ADAI LEBO YA KONDE GANG IMEIPA HADHI MUZIKI WAKE

Rapper mkali kwa michano kutoka Tanzania country boy amefunguka namna lebo ya muziki ya Konde Gang ilivyobadilisha maisha yake na kuupa hadhi mziki wa Hip Hop nchini tanzania. Kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni, rapa huyo amesema kuwa chini ya lebo hiyo imemuongezea thamani kama msanii na hata imepelekea hadhi ya muziki wa hiphop tanzania kupanda kwani mara nyingi wasanii wa Hip-hop huwa wanakosa nafasi ya kujiunga na lebo kubwa. Kwenye lebo ya Konde Gang, Country boy ndiye msanii pekee anayefanya muziki wa Hip-hop na Kabla ya kuingia kwenye lebo hiyo, Rapa huyo alipita kwenye lebo kadhaa za muziki ikiwemo Rooftop Entertainment.

Read More
 KANYE WEST MBIONI KUZINDUA KAMPUNI INAYOJIHUSISHA NA VIFAA VYA KITEKNOLOJIA

KANYE WEST MBIONI KUZINDUA KAMPUNI INAYOJIHUSISHA NA VIFAA VYA KITEKNOLOJIA

Baada ya kukuvalisha viatu na mavazi ya aina yake kupitia chapa ya Yeezy, Kanye West yupo tayari kukuletea vifaa vya kiteknolojia. Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ, Kanye ameripotiwa kulisajili kibiashara jina la ‘DONDA’ mnano Septemba 21 mwaka huu ambapo dhumuni ni kutengeneza vifaa kama Simu, (laptop), Tablets, Headphones na Bluetooth speakers. Akiwa muumini mkubwa wa vifaa vya kampuni ya Apple, sasa Kanye West amedhamiria kuwa mshindani mkuu wa kampuni hiyo kubwa ya vifaa vya kiteknolojia duniani. Kwenye DONDA, Kanye West amepanga pia kutengeneza Saa za mkononi pamoja na miwani za kisasa, vifaa vingine kama earbuds na wireless headset ambavyo vitakuwa sehemu ya bidhaa za DONDA. DONDA ni jina la mama mzazi wa Kanye West ambaye alifariki dunia Novemba mwaka wa 2007 na amelitumia jina hilo kwenye album yake ya 10 ambayo ilitoka Agosti 29 mwaka huu

Read More
 ALI KIBA AWEKA HADHARANI TRACKLIST YA ALBUM YAKE MPYA “ONLY ONE KING”

ALI KIBA AWEKA HADHARANI TRACKLIST YA ALBUM YAKE MPYA “ONLY ONE KING”

Hatimaye orodha ya nyimbo ambazo zinaunda Album ya Mfalme wa muziki wa Bongo Fleva ali kiba iitwayo Only One King imeachiwa rasmi. Album hiyo ina jumla ya nyimbo kumi na sita na kwa sasa unaweza kui-pre order kupitia mtandao wa kusambaza muziki duniani wa Apple Music. Kwenye Album hiyo wasanii mbalimbali kama patoranking, black diamond, sauti sol, nyashinski, khaligraph jones, sarkodie, Mayorkun, tommy flavour, k2ga na abdu kiba ndio watasikika Nyimbo 12 kwenye album hiyo ndio geni haujawahi kuzisikia masikioni mwako na nyimbo 4 tu ndizo ambazo Ali kiba ameshaziachia tayari. Only one king Album kutoka kwa mtu mzima Ali kiba inatoka Oktoba 7, mwaka wa 2021 kwenye mitandao ya kusambaza muziki duniani.

Read More
 GOOGLE YAWEKA UWEZO WA SIMU KUREKODI VIDEO WAKATI WA DHARURA.

GOOGLE YAWEKA UWEZO WA SIMU KUREKODI VIDEO WAKATI WA DHARURA.

Google imeweka uwezo wa simu kurekodi video katika wakati wa dharura kwenye Android 12. Imeweka uwezo wa kurekodi video automatic endapo mtu akibonyeza power button zaidi ya mara 5 au unapokwepo katika hali ya hatari.   Katika sehemu ya Emergency SOS, mtumiaji anaweza kuwasha option ya “Record emergency Video” ambapo endapo ukibonyeza Power Button mara 5 na kuendelea, moja kwa moja simu itakuwa katika SOS Mode, itakuwa inarekodi video huku ikipiga simu ya Emergency Services.   Video za dharura inaweza kuwa na urefu wa dakika 45 na ikubwa wa 10MB kwa dakika moja ili kusaidia storage na kufanya backup. Hii itasaidia mtu akipata matatizo, anaweza kutumia simu yake kurekodi ushahidi kwa Video.   Google imesema ukirekodi video, kama upo unatumia huduma ya internet; video hiyo inakuwa inajisevu ili endapo simu yako ikifa au kuibiwa ile video itabaki katika Cloud Storage yako.    

Read More
 FACEBOOK YAANZA KUWEKA REELS KATIKA APP YAKE

FACEBOOK YAANZA KUWEKA REELS KATIKA APP YAKE

Facebook iliweka videos fupi katika mtandao wa Instagram zilizopewa jina la Reels, mbinu ambayo inasemekana ni kushindana na soko la TikTok na YouTube Shorts kwa sababu imeonekana kuna watu wengi wanapendelea short videos.   Sasa habari njema ni kwamba Facebook imeanza kuweka rasmi Reels katika app yake ya Facebook kwa watumiaji wa Marekani na imesema itaweka katika nchi zote zilizobaki. Watumiaji wa Facebook wataweza kuweka Reels na kushare katika mtandao wa Instagram na Facebook.   Reels za Instagram pia zitaweza kuonekana katika mtandao wa Facebook na mpangilio na muonekano unaonekana kama Instagram Reels na TikTok. Reels za Facebook zitakuwa na Audio, AR Effects, Timer/Countdown/Speeds na sehemu ya Multi Clips ambayo itawezesha watumiaji kumix videos.   Watumiaji wa Facebook wataona tab mpya ya “Reels” katika app ya Facebook na hivi karibuni itaanza kupatikana kwa watumiaji wa nchi zote duni kwani ni update ambayo imeanza rasmi leo.         Facebook iliweka videos fupi katika mtandao wa Instagram zilizopewa jina la Reels, mbinu ambayo inasemekana ni kushindana na soko la TikTok na YouTube Shorts kwa sababu imeonekana kuna watu wengi wanapendelea short videos.   Sasa habari njema ni kwamba Facebook imeanza kuweka rasmi Reels katika app yake ya Facebook kwa watumiaji wa Marekani na imesema itaweka katika nchi zote zilizobaki. Watumiaji wa Facebook wataweza kuweka Reels na kushare katika mtandao wa Instagram na Facebook.   Reels za Instagram pia zitaweza kuonekana katika mtandao wa Facebook na mpangilio na muonekano unaonekana kama Instagram Reels na TikTok. Reels za Facebook zitakuwa na Audio, AR Effects, Timer/Countdown/Speeds na sehemu ya Multi Clips ambayo itawezesha watumiaji kumix videos.   Watumiaji wa Facebook wataona tab mpya ya “Reels” katika app ya Facebook na hivi karibuni itaanza kupatikana kwa watumiaji wa nchi zote duni kwani ni update ambayo imeanza rasmi leo.        

Read More
 MEEK MILL AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA “EXPENSIVE PAIN”

MEEK MILL AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA “EXPENSIVE PAIN”

Hatimaye Rapa kutoka nchini marekani meek mill Ameikata Kiu Ya Mashabaki Zake Baada Ya Kuiachia Album Yake Mpya inayokwenda kwa jina la EXPENSIVE PAIN Meek Mill Amethibitisha Hilo Kupitia Ukurasa Wake Wa Instagram kwa kuandika ujumbe unaosomeka “My new album Expensive Pain out now ” akimaanisha kwamba album yake mpya sasa inapatikana kwenye digital platform zote. Expensive Pain inakuwa album ya 5 kwa mtu mzima Meek Mill, lakini pia inavunja ukimya wake wa miaka 3 tangu alipoachia yake ya Championships

Read More
 ZULITUMS ATOA CHANGAMOTO KWA WASANII WA UGANDA KUTUMIA KIINGEREZA KWENYE NYIMBO ZAO

ZULITUMS ATOA CHANGAMOTO KWA WASANII WA UGANDA KUTUMIA KIINGEREZA KWENYE NYIMBO ZAO

Mwanamuziki kutoka nchini uganda Zulitums ametoa changamoto kwa wasanii nchini humo kuanza kutumia lugha ya kiingereza kwenye nyimbo zao ili muziki wa uganda uweze kufika mbali zaidi. Zulitums amesema licha ya wasanii wa uganda kutoa muziki mzuri wengi wao wamekuwa wakitumia lugha ya luganda kwenye nyimbo zao jambo analosema limewafanya wasanii kushindwa kutanua wigo wa muziki wao kwenye nchini zingine. Zulitums ni mmoja wa wasanii nchini uganda walioshindwa kuupeleka muziki wao kimataifa hadi pale alipojiunga na lebo ya muziki ya Black Avie iliyoko nchini Nigeria ambayo imebadilisha aina ya muziki wake.

Read More