RINGTONE APOTEZA MILLIONI 3 ZA KENYA BAADA YA WIMBO WA YESU ANG’ARE KUFUTWA YOUTUBE

RINGTONE APOTEZA MILLIONI 3 ZA KENYA BAADA YA WIMBO WA YESU ANG’ARE KUFUTWA YOUTUBE

Msanii wa nyimbo za injili nchini Ringtone ameumizwa na kitendo cha wimbo wake uitwao Yesu Ang’are aliyomshirikisha Rose Muhando kufutwa kwenye mtandao wa youtube kwa madai ya haki miliki.   Kupitia ukurasa wake wa instagram Ringtone amesema  anakadiria hasara ya shillingi millioni tatu alizotumia kutayarisha audio na video ya wimbo huo jambo ambalo amesema limempelekea kupata na msongo wa mawazo.   Ikumbukwe wimbo wa yesu Ang’are kutoka kwa mtu mzima Ringtone ulifutwa kwenye mtandao wa youtube baada ya ringtone kushindwa kumaliza tofauti zake na lucy ndanu aliyewasilisha lalama kwenye mtandao wa youtube kuwa rose muhando alitumia mashairi ya wimbo wake kwenye wimbo wa ringtone.          

Read More
 “BLACK CHILD ALBUM” YA MR. SEED YAFIKISHA STREAMS 500,000 BOOMPLAY

“BLACK CHILD ALBUM” YA MR. SEED YAFIKISHA STREAMS 500,000 BOOMPLAY

Nyota wa muziki nchini Mr. Seed anazidi kufanya vizuri kupitia mauzo ya mtandaoni na Albamu yake “Black Child” ambayo tayari ina takriban wiki tatu tangu itoke rasmi.   Album ya “Black Child” ambayo ndio albamu ya kwanza ya  Mr. Seed tangu aanze muziki imefanikiwa kufikisha  zaidi ya Streams laki tano kwenye mtandao wa kusikiliza na kupakua muziki wa Boomplay.   Ikumbukwe album ya Black Child kutoka kwa mtu mzima iliachiwa rasmi Septemba 13 mwaka huu wa 2021 ikiwa na jumla ya mikwaju 10 ya moto huku  ikiwa na kolabo 9 pekee.    

Read More