LifeStyle

Bahati Ashindwa Kujizuia Baada ya Kukutana na Mwanamke Aliyedai kuwa Mama yake Mzazi

Bahati Ashindwa Kujizuia Baada ya Kukutana na Mwanamke Aliyedai kuwa Mama yake Mzazi

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Bahati, ameshindwa kujizuia baada ya kukutana ana kwa ana na mwanamke aliyedai kuwa ndiye mama yake mzazi mwishoni mwaka 2025.

Katika video inayoenea mtandaoni, Bahati ameonekana kuguswa sana na tukio la mwanamke huyo kumkumbatia kwa muda mrefu huku akilia kwa uchungu. Kwenye video hiyo, Mama huyo ameoneka akiomba Mungu msamaha kwa kile alichodai kuwa ni kumpoteza mwanawe kwa miaka mingi, akieleza maumivu aliyoyabeba moyoni kwa kipindi chote hicho.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Bahati amesema amechanganyikiwa na hajui aanzie wapi. Amekiri kuwa na maswali mengi kichwani mwake kuhusu maisha yake ya awali na ukweli wa madai ya mama huyo. Amesema hali hiyo si rahisi kuikubali mara moja, hasa ikizingatiwa historia yake ya kukulia katika mazingira ya changamoto tangu utotoni.

Ikumbukwe mwanamke huyo alijitokeza mwishoni mwa mwaka jana akidai kuwa yeye ndiye mama halisi wa Bahati, akieleza kuwa amekuwa akimtafuta kwa muda mrefu bila mafanikio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *