Entertainment

Eric Omondi Awahimiza Wasanii Kuhudhuria Ibada ya Wafu ya Marehemu Shalkido

Eric Omondi Awahimiza Wasanii Kuhudhuria Ibada ya Wafu ya Marehemu Shalkido

Mchekeshaji na mwanaharakati Eric Omondi ametoa wito kwa wasanii nchini Kenya kuhudhuria ibada ya wafu ya marehemu msanii wa Gengetone Shalkido, itakayofanyika Jumatano tarehe 15, katika kanisa la All Saints Cathedral, Nairobi, kuanzia saa 11:30 asubuhi.

Kupitia ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Eric amewahimiza wasanii wa Kenya kuonyesha umoja na upendo kwa kuhudhuria ibada hiyo, akisema kuwa ni muhimu kwa wasanii kusimama pamoja hasa nyakati za huzuni.

Eric ameongeza kuwa ibada hiyo si tu ya kumuaga Shalkido, bali pia ni ishara ya mshikamano katika tasnia ya muziki wa Kenya. amesema wasanii wanapaswa kuacha tofauti zao pembeni na kuungana katika maombi na heshima za mwisho kwa marehemu.

Ibada hiyo inatarajiwa kuwaleta pamoja wasanii, wadau wa muziki, na mashabiki wengi watakaoungana kumuaga Shalkido kwa heshima na upendo kabla ya mazishi yake baadaye wiki hii.

Ikumbukwe Shalkido, aliyepata umaarufu kupitia kundi la Sailors Gang, alifariki dunia hivi karibuni kufuatia ajali mbaya ya barabarani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *