Entertainment

Kauli ya Omondi Kwa Vijana Yazua Mjadala Kuhusu Siasa za Lang’ata

Kauli ya Omondi Kwa Vijana Yazua Mjadala Kuhusu Siasa za Lang’ata

Ziara ya mwanaharakati na mchekeshaji Eric Omondi katika eneo la Lang’ata imezidi kuibua gumzo kubwa kuhusu mustakabali wa kisiasa wa mbunge wa sasa Felix Oduor (Jalang’o) kuelekea uchaguzi wa 2027 baada ya umati mkubwa wa vijana kumkaribisha kwa shangwe na nderemo katika mtaa wa Mugumoini.

Katika ziara hiyo iliyovutia mamia ya vijana, Omondi alitembea mitaani akiandamana na umati uliokuwa ukimuimbia na kumpa mapokezi ya kishujaa. Mapokezi hayo yamechochea uvumi kuwa huenda anajiandaa kuwania kiti cha ubunge wa Lang’ata, jambo ambalo limeanza kuongeza shinikizo kwa mbunge wa sasa.

Hata hivyo, kauli yake kwa vijana imezua mjadala mpya baada ya Omondi kuwataka vijana kujisali kama wapiga kura, akiwahimiza kuonyesha msimamo wao dhidi ya kile alichokitaja kama mfumo unaowatelekeza vijana. Wadadisi wa siasa za Nairobi wanasema kuwa Omondi ana ushawishi mkubwa miongoni mwa vijana, na kauli zake zinaweza kuwa na athari katika mienendo ya kisiasa ya eneo hilo.

Hadi kufikia sasa, Eric Omondi hajatangaza rasmi iwapo atawania kiti cha ubunge cha Lang’ata mwaka 2027. Hata hivyo, ziara yake na mapokezi aliyopata yanaendelea kuongeza tashwishi kuhusu ramani ya kisiasa ya Lang’ata katika miaka ijayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *