Others

Kendrick Lamar ashinda Tuzo ya Msanii Bora wa Hiphop kwenye BET Hip-Hop Awards 2022

Kendrick Lamar ashinda Tuzo ya Msanii Bora wa  Hiphop kwenye BET Hip-Hop Awards 2022

Rapa Kendrick Lamar ameibuka mshindi wa kipengele cha Hip-Hop Artist Of The Year kwenye Tuzo za BET Hip-Hop 2022 ambazo zinatolewa usiku wa kuamki leo nchini Marekani. Kendrick Lamar pia ameondoka na ushindi kwenye vipengele vya Lyricist Of The Year, Best Hip Hop Video “Family Ties”, Best Live Performer na Hip Hop Album Of The Year (Mr. Morale & The Big Steppers)

Kwa upande mwingine Rapa 50 Cent ameibuka mshindi wa Tuzo ya ‘Hustler Of The Year’ akiwaangusha DJ Khaled, Drake, Cardi B, Jay-Z, Kanye West na Megan Thee Stallion.

Kolabo ya Future, Tems na Drake “Wait For You” imeshinda Tuzo ya Best Collaboration kwenye Tuzo za BET Hip Hop 2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *