Entertainment

Mejja aachia albamu yake ya kwanza – Mtoto wa Khadija

Mejja aachia albamu yake ya kwanza – Mtoto wa Khadija

Msanii wa muziki wa Genge kutoka Kenya, Mejja, ameachia rasmi albamu yake mpya na ya kwanza katika maisha yake ya muziki inayokwenda kwa jina la Mtoto wa Khadija.

Albamu hiyo ina jumla ya nyimbo 13, ambapo kati ya hizo, 10 ni kolabo na wasanii mbalimbali huku nyimbo tatu zikiwa zimeimbwa na Mejja peke yake bila kumshirikisha msanii mwingine.

Kupitia mradi huo, Mejja amewakutanisha wasanii kadhaa kutoka Afrika Mashariki, akiwemo Jay Melody wa Tanzania, Fik Fameica wa Uganda, pamoja na Nadia Mukami na Toxic Lyrikali kutoka Kenya, miongoni mwa wengine wengi.

Albamu ya Mtoto wa Khadija ambayo imebeba uzito mkubwa katika safari ya muziki ya Mejja inatapatikana kwenye majukwaa yote ya kupakua na kusikiliza muziki mtandaoni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *