Tech news

Meta Yatangaza Kuondoa Huduma za AI Kwenye WhatsApp Kuanzia 2026

Meta Yatangaza Kuondoa Huduma za AI Kwenye WhatsApp Kuanzia 2026

Kampuni ya Meta imetangaza kuwa kuanzia mwaka 2026, haitaruhusu tena kampuni za teknolojia ya akili bandia (AI) kama OpenAI (ChatGPT) na Perplexity kutumia jukwaa la WhatsApp kutoa huduma zao. Uamuzi huu unalenga kuimarisha matumizi ya Meta AI pekee ndani ya app hiyo maarufu ya kutuma ujumbe.

Kwa sasa, huduma kama ChatGPT na Perplexity zimekuwa zikipatikana moja kwa moja ndani ya WhatsApp, ambapo watumiaji wamekuwa wakichat na mifumo ya AI bila kulazimika kutumia app ya nje. Hata hivyo, kwa mujibu wa sheria mpya za Meta, fursa hiyo itaondolewa rasmi.

Tayari OpenAI imethibitisha kuwa itasitisha huduma ya ChatGPT ndani ya WhatsApp ifikapo Januari 15, 2026. Kampuni ya Perplexity pia imetangaza kuwa itafuta akaunti yake ya WhatsApp katika kipindi hicho.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa teknolojia, hatua ya Meta inaweza kuelekezwa katika kuimarisha ushawishi wa Meta AI na kupunguza ushindani wa moja kwa moja kutoka kwa huduma za AI huru ndani ya majukwaa yake.

Wakati huo huo, kampuni hizo za AI zimeanza kuhamia kwenye Telegram, jukwaa ambalo halijaweka vikwazo kwa huduma za AI, na linatoa uhuru zaidi kwa watumiaji kuchagua mfumo wa AI wanaotaka kutumia.

Hatua hii inaibua maswali kuhusu mustakabali wa huduma huria za AI ndani ya majukwaa binafsi na huenda ikawa mwanzo wa mapambano mapya ya udhibiti wa huduma za akili bandia kwenye majukwaa ya kidijitali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *