LifeStyle

Moji Shortbaba na Mkewe Nyawira Watangaza Kupata Mtoto wa Kwanza

Moji Shortbaba na Mkewe Nyawira Watangaza Kupata Mtoto wa Kwanza

Msanii wa muziki wa injili, Moji Shortbaba, pamoja na mkewe Nyawira Gachugi, wamekaribisha mtoto wao wa kwanza, tukio lililojaa furaha na shukrani kubwa kwa familia hiyo changa.

Kupitia ujumbe wenye hisia waliomchapisha mtandaoni, wanandoa hao wametangaza kwa furaha kuwa mtoto wao mchanga amewasili salama, wakieleza kuwa ni baraka waliyoingojea kwa hamu kubwa.

Moji Shortbaba na Nyawira pia wametoa shukrani za dhati kwa familia, marafiki na jamii yao ya karibu kwa upendo mkubwa waliowaonyesha katika safari yao ya ujauzito. Wameeleza kuwa wameguswa sana na simu nyingi za pongezi, kuangaliwa hali mara kwa mara na msaada wa vitendo walioupata.

Katika ujumbe wao, Nyawira amebainisha kuwa sasa yeye na Moji Shortbaba wanaanza safari mpya ya kulea na kutunza mtoto wao ambaye Mungu amewabarik nayo, akisema mikono na mioyo yao imejaa shukrani na unyenyekevu mkubwa.

Habari za ujio wa mtoto wao zimepokelewa kwa furaha na mashabiki, marafiki na wadau wa muziki wa injili, wengi wakimpongeza wanandoa hao na kuwatakia baraka tele katika ukurasa mpya wa maisha yao ya kifamilia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *