Msanii wa muziki, KRG The Don, ameonekana kupanua wigo wake wa kibiashara baada ya kuashiria kuingia katika biashara ya kuzalisha tissue paper.
Kupitia Instagram Story, KRG amechapisha picha za vifurushi vya tissue paper, akizisindikiza na neno “mboka” linalomaanisha kazi. Hatua hiyo imekitafsiri kuwa msanii huyo huenda tayari ameanza rasmi shughuli za uzalishaji wa bidhaa hiyo.
Ingawa KRG The Don bado hajatangaza rasmi uzinduzi wa kampuni yake, dalili zinaonyesha kuwa anaweza kuwa katika hatua za mwisho za kuanzisha biashara hiyo, huku uzinduzi rasmi ukitarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Hatua yake ya kuingia kwenye sekta ya uzalishaji wa bidhaa za matumizi ya kila siku inaonekana kama mkakati mwingine wa kuongeza vyanzo vya mapato, huku mashabiki wakingoja kwa hamu taarifa rasmi kuhusu jina la kampuni, bei na upatikanaji wa bidhaa hiyo sokoni.