Entertainment

Msanii Mad Ice Aahirisha Ziara Yake ya Muziki Nchini Tanzania Kufuatia Machafuko

Msanii Mad Ice Aahirisha Ziara Yake ya Muziki Nchini Tanzania Kufuatia Machafuko

Msanii mkongwe wa muziki kutoka Uganda, Mad Ice, ametangaza kuahirisha rasmi ziara yake ya muziki iliyokuwa imepangwa kufanyika nchini humo, akitaja hali ya machafuko iliyoshuhudiwa hivi karibuni kama sababu kuu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo amesema ameona ni vyema kusitisha matamasha hayo hadi hali itakapotulia, akisisitiza kuwa usalama wa mashabiki na timu yake ni jambo la kipaumbele.

Mad Ice, anayefahamika kwa vibao kama Baby Gal na Wote Wapo, alikuwa ameandaa mfululizo wa media tour katika miji mikubwa kama Dar es Salaam, Arusha na Mwanza, kabla ya kufanya uamuzi wa kuahirisha ziara hiyo.

Mad Ice alipata mkubwa miaka yah apo nyuma kupitia Albamu yake iitwayo “Baby Gal”, yenye nyimbo zilizotikisa miaka ya 2004 – 2005, ikiwemo wimbo wa “Baby Gal” uliompa umaarufu mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *