Gossip

Msanii Mkongwe Bebe Cool Aingia Kwenye Bifu na Msanii Mtukutu Alien Skin

Msanii Mkongwe Bebe Cool Aingia Kwenye Bifu na Msanii Mtukutu Alien Skin

Msanii mkongwe wa muziki nchini Uganda, Bebe Cool, anaripotiwa kuingia kwenye bifu kali na msanii mtukutu Alien Skin, hatua inayotamatisha urafiki wao wa karibu uliodumu kwa zaidi ya miaka miwili.

Duru za kuaminika zinasema kuwa uhusiano kati ya wawili hao umedorora, huku wakidaiwa kutokuelewana kabisa. Chanzo cha ugomvi huo bado hakijathibitishwa rasmi, ingawa mwanamama Full Figure amedai kuwa tamaa ya Alien Skin ndiyo iliyosababisha mgogoro huo.

Kwa mujibu wa madai hayo, Alien Skin alidai alipwe mamilioni ya pesa ili kutumbuiza katika mikutano ya kampeni ya Rais Museveni (Sevo) huko mashariki mwa Uganda. Inadaiwa kwamba baada ya Bebe Cool kushindwa kukidhi matakwa hayo, Alien Skin alijiondoa kwenye ziara hiyo na kurejea Kampala.

Ripoti zaidi zinaeleza kuwa Bebe Cool amefanya juhudi kadhaa kujaribu kumrejesha msanii huyo wa Fangone Forest katika urafiki wao wa awali, lakini Alien Skin amekataa maridhiano, jambo lililozidisha mvutano kati yao.

Kwa muda mrefu, Bebe Cool amekuwa mmoja wa watu waliomsaidia sana Alien Skin katika safari yake ya muziki, akimtoa polisi mara kadhaa, kusuluhisha migogoro yake na wasanii wenzake, pamoja na kumsifia hadharani kupitia mahojiano mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *