Timu ya Kenya Police FC ilijipatia ushindi baada ya kuilaza Tusker FC kwa mabao 2-1 katika mchuano wa Ligi Kuu ya FKF uliochezwa katika uwanja wa Ruaraka. Police FC ilijipatia bao la kwanza kupitia mchezaji Erick Zakayo kwenye dakika ya 13.
Ubabe wao ulizaa matunda tena katika dakika 30 baada ya David Simiyu kufunga bao la pili. Tusker, mabingwa wa awali walifunga bao la kufutia machozi katika dakika za lala salama kupitia kwa Eric Kapaito, huku Polisi wakishikilia kidete na kujipatia alama zote tatu.
Ushindi huo umeipandisha Police FC hadi nafasi ya 10 kwa pointi 11, ilihali Tusker FC ikishuka hadi nafasi ya 7 ikiwa na pointi 12.
Kwingineko, AFC Leopards ilitoka sare tasa na Murang’a SEAL katika Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo. Gor Mahia inanongoza kwenye msimamo wa ligi kwa alama 16, alama moja pekee mbele ya Kakamega Homeboyz, nayo AFC Leopards inashikilia nafasi ya tatu kwa alama 13