Entertainment

Rais William Ruto Aomboleza Kifo cha Msanii wa Injili Betty Bayo

Rais William Ruto Aomboleza Kifo cha Msanii wa Injili Betty Bayo

Rais William Ruto ameongoza taifa la Kenya kuomboleza kifo cha mwimbaji wa nyimbo za injili Betty Bayo, aliyefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Kenyatta.

Kupitia mtandao wa X, Rais Ruto ameelezea huzuni yake, akimtaja marehemu kama msanii mwenye sauti ya kipekee aliyekuwa na ujumbe wa matumaini uliogusa maisha ya maelfu ya Wakenya.

Rais amesema kuwa kwa zaidi ya miaka 15, Betty Bayo alitumia kipaji chake kuinua roho za watu na kueneza ujumbe wa kutokata tamaa, bila kujali saa wala dhoruba inayowakabili.

Kiongozi wa taifa, ameutaja wimbo wake maarufu “11th Hour” kama wimbo unaoakisi imani thabiti na uwezo wa Mungu katika kuleta mabadiliko hata kwenye nyakati ngumu.

Hata hivyo rais ameumalizia ujumbe wake kwa kusema mchango wa Betty Bayo katika muziki wa injili utaendelea kukumbukwa kwa vizazi vijavyo, akisisitiza kuwa marehemu alikuwa mfano wa imani, uvumilivu na matumaini yasiyotetereka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *