Mr. Seed afunguka chanzo cha kumaliza ugomvi wake na Bahati

Mr. Seed afunguka chanzo cha kumaliza ugomvi wake na Bahati

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Seed amefichua kuwa waliamua kumaliza ugomvi wao na Bahati kwa manufaa ya watoto wao. Kwenye mahojiano na World IS, Mr. Seed amesema watoto wao walikuwa wakishambuliwa kila mara kwenye mitandao ya kijamii kutokana na utofauti wao kimuziki, kitendo kilichowalazimu kukutana na kuweka kando uhasama wao ambao ungeathiri ukuaji wa watoto wao katika siku za mbeleni. “Nilikuwa nikiposti picha za mtoto wangu Gold na mashabiki wenye roho chafu walikuwa na mazoea ya kumlinganisha na mtoto wa Bahati Majesty. Hilo pia lilitokea kwa upande wa Bahati na watoto wetu wangeishia kutusiwa,” Alisema. Mr. Seed na Bahati ambao walikuwa marafiki wa karibu, walitofautiana mwaka 2018 baada ya wake zao Diana Marua na Nimo Gachuiri kukosa maelewano katika hafla ya mkesha wa mwaka mpya. Kwa mujibu wa mashuhuda, Diana alipinga wazo la Nimo la kuuza kahawa na vitafunio kwenye sherehe hiyo na aliishia kuwapigia simu polisi kumuondoa Nimo ambaye kwa wakati huo alikuwa mjamzito mzito.

Read More
 Bahati akerwa na kitendo cha mashabiki kumuita mheshimiwa

Bahati akerwa na kitendo cha mashabiki kumuita mheshimiwa

Msanii nyota nchini Bahati amewaonya mashabiki dhidi ya kumuita Mheshimiwa ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu ashindwe kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti mwaka huu. Kupitia mitandao yake ya kijamii hitmaker huyo wa Adhiambo ameshangazwa na kitendo cha watu kumhusisha na jina hilo kila mara huku akiwataka kutumia jina la Bahati ambalo amekuwa akilitumia kwenye muziki “Sielewi Mbona Bado Watu Wananiita MHESH… Niiteni tuu Bahati Please.” Ameandika Instagram. Lakini pia Bahati amewataka mashabiki kuacha kumhusisha na siasa kwa sababu amerudi kwenye shughuli ya muziki ambayo amekuwa akifanya kwa muda mrefu. “Hii Mambo Ya Mhesh Wekeni Kando…. THE KING IS BACK!!! Tell Me. What Happened While I Was Away???”, Ameongeza. Bahati ambaye alikuwa kimya kwa miezi miwili baada ya kushindwa kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu, anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao “Mambo ya Mhesh” Utakumbuka Bahati alikuwa anawania kiti cha ubunge Mathare kupitia tiketi ya chama cha jubilee lakini alishindwa na mpenzani wake Anthony Oluoch wa chama cha ODM.

Read More
 Diana B na Bahati watangaza jinsia ya mtoto wao

Diana B na Bahati watangaza jinsia ya mtoto wao

Couple pendwa nchini inayoundwa na wasanii Diana B pamoja na Bahati imetangaza jinsia ya mtoto wao wa tatu ambaye atazaliwa hivi karibuni. Katika hafla ya kutambulisha jinsia ya mtoto huyo wawili hao wameweka wazi kuwa wanatarajia kupata mtoto wa kiumemuda wowote kuanzia sasa Hata hivyo mashabiki na mastaa mbali mbali wamewapongeza wawili hao kwa hatua hiyo wakati huu wapo mbioni mkaribisha mtoto wao wa watatu. Utakumbuka juzi kati taarifa zilisambaa mtandaoni kwamba huenda Diana B amejifungua kwa siri kutokana na jumbe zenye ukakasi alizokuwa anachapisha kwenye mtandao wake wa Instagram.

Read More
 Ringtone afunguka sababu za kuwaponda Willy Paul na Bahati

Ringtone afunguka sababu za kuwaponda Willy Paul na Bahati

Hitmaker wa Ombi Langu, Ringtone Apoko amefunguka sababu ya kuwakosoa wasanii Willy Paul na Bahati kila mara kwenye majukwaa mbali mbali. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema wawili hao walimvunjia heshima mwenyezi Mungu kwa kutumia vibaya kiwanda cha muziki wa injili kwa ajili ya kujilimbikizia mali na kisha wakageukia muziki wa kidunia. Msanii huyo ameenda mbali zaidi na kusema kuwa kitendo cha Willy Paul na Bahati kutumia njia haramu kuchuma mali wanayomiliki kwa sasa imewaponza kisanaa kiasi cha kutopata mafanikio kwenye muziki wao. Katika hatua nyingine Ringtone ametetea utajiri wake kwa kusema kuwa ana vyanzo vingi halali vinavyomuinguzia kipato huku akikanusha tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya ulanguzi wa pesa kwani inakwenda kinyume na maandiko matakatifu.

Read More
 Bahati amkataa Raila Odinga, akiri uchaguzi mkuu nchini Kenya ulikumbwa na dosari

Bahati amkataa Raila Odinga, akiri uchaguzi mkuu nchini Kenya ulikumbwa na dosari

Staa wa muziki nchini Bahati amefunguka sababu za kudinda kuchukua kazi ambayo kinara wa Azimio Raila Odinga aliahidi kumpa pindi atakapotua uongozi wa nchi kwenye uchaguzi uliokamilika. Bahati amesema alijua kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu ungekumbwa na dosari na ndio maana akaendelea na azma yake ya kuwania ubunge Mathare licha ya kushurutishwa kujiondoa kwenye kinyanganyiro hicho. Katika hatua nyingine Hitmaker huyo wa “”Adhiambo anaamini kuna siku jamii ya Kamba itamtoa rais ambaye ataongoza taifa la Kenya licha ya Odinga kumtumia vibaya Kalonzo Musyoka ambaye alikuwa na nyota ya kuiongoza jamii hiyo. Hata hivyo Bahati ambaye amesisitiza kuwa atakuwa kwenye kinyanganyiro cha urais mwaka 2037 amejinasibu kuwa hajutii kitendo cha kukosa ubunge Mathare kwa kuwa yeye ni moja kati ya watu ambao wapo ndani ya serikali.

Read More
 Ringtone aanika siri za Bahati, Adai yupo mbioni kuja na EP mpya

Ringtone aanika siri za Bahati, Adai yupo mbioni kuja na EP mpya

Mwanamuziki asiyeishiwa na matukio kila leo Ringtone Apoko amefunguka tusiyoyajua kuhusu ukimya wa Bahati kwa kusema kwamba amekuwa chimbo akiandaa EP yake mpya. Kulingana na Ringtone hatua ya Bahati kufuta kila kitu kwenye ukurasa wake wa Instagram ilikuwa ni njia ya kutengeneza mazingira ya ujio wa EP hiyo ambayo ina jumla ya nyimbo 6. Katika hatua nyingine Ringtone amewataka mashabiki kumweka Bahati kwa maombi kwa sababu mkali huyo wa ngoma ya “Adhiambo” amekuwa na msongo wa mawazo tangu ashindwe kwenye kinyanganyiro cha ubunge Mathare. Bahati amekuwa kimya baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9 kukamilika nchini Kenya, jambo ambalo liliwaacha mashabiki zake na maswali mengi kiasi cha kutaka kufahamu ni nini hasa kimemsibu msanii huyo.

Read More
 BAHATI AZUA GUMZO MTANDAONI KWA KUFUTA KILA KITU INSTAGRAM

BAHATI AZUA GUMZO MTANDAONI KWA KUFUTA KILA KITU INSTAGRAM

Staa wa muziki nchini Bahati amefuta picha na video zake kwenye mtandao wa Instagram, hatua iliyohisiwa ni ujio wake mpya. Hatua hii ya Bahati imevuta hisia za baadhi ya mashabiki ikihisiwa kuwa huenda akaachia kazi mpya hivi karibuni baada ya kukaa kimya tangu apoteze kiti cha ubunge mathare kwenye uchaguzi mkuu uliokamilika nchini kenya. Uamuzi wa Bahati hakujali hata picha alizopiga na mke wake, Diana B huku upande mwingine ikihisiwa kuwa pengine kuna kingine kisichohusiana na ujio wa kazi kutoka kwake. Utakumbuka juzi kati Bahati alifunguka kuwa familia yake ipo njia panda ambapo aliwataka mashabiki kumweka kwenye maombi pamoja na mke wake Diana ambaye alikuwa mbioni kujifungua.

Read More
 BAHATI AFUNGUKA CHANZO CHA UKIMYA WAKE

BAHATI AFUNGUKA CHANZO CHA UKIMYA WAKE

Hatimaye staa wa muziki nchini Bahati ameamua kuvunja kimya chake kwa mara ya kwanza baada ya kupoteza ubunge wa Mathare kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu. Kwenye mahojiano na Nairobi News mkali huyo wa ngoma ya “Adhiambo” amefichua kuwa hali sio shwari katika familia yake hasa upande mke wake Diana. Bahati hata hivyo amepata kigugumzi kueleza kwa kina kinachoendelea ndani ya familia yake licha mtandao huo kumsisitizia kuweka wazi kinachomsibu. Siku chache zilizopita Diana aliposti picha ya njiwa mweupe kwenye background nyeusi na kusindikiza na ujumbe unaosomeka ” Only in the Darkness, Can you see the Stars .” Ujumbe huo uliowaacha mashabiki njia panda ikizingatiwa kuwa alikuwa amezima uwanja wa kutoa maoni kwenye posti yake instagram. Mashabiki hata hivyo walienda mbali na kuhoji kuwa huenda kuna habari mbaya imemtokea mwanamama huyo ambaye alikuwa na ujauzito wa miezi nane. Mara ya mwisho Diana kuonekana hadharini ilikuwa kwenye hafla ya baby shower yake ambapo alifunguka kupitia changamoto nyingi kwenye safari yake ya uja uzito.

Read More
 MASAUTI AKIRI KUPATA UGUMU KUFIKIA BAHATI

MASAUTI AKIRI KUPATA UGUMU KUFIKIA BAHATI

Hitmaker wa “Sing’oki”, msanii Masauti amekiri kupata ugumu kumfikia msanii mwenzake Bahati tangu kukamilika kwa uchaguzi mkuu Agosti 9 mwaka huu nchini Kenya. Masauti amedai Bahati hapokei simu wala hajibu jumbe zake kwenye mtandao wa Instagram, kitendo ambacho kinampa wasi wasi kuhusu hali ya mkali huyo wa ngoma ya “Adhiambo.” Kauli ya Masauti imekuja mara baada ya moja ya shabiki yake kwenye mtandao wa Instagram kumuuliza kama ana mpango wa kufanya kazi ya pamoja na Bahati. Utakumbuka Bahati amekuwa kimya tangu apoteze kiti cha ubunge eneo la Mathare kwenye uchaguzi ambao alidai kwamba ulikumbwa na udanganyifu mwingi.

Read More
 BAHATI AKIRI BADO NI MWANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI

BAHATI AKIRI BADO NI MWANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI

Hitmaker wa ngoma ya “Adhiambo”, Msanii Bahati amedai kwamba bado yeye ni msanii wa injili kwani alimuahidi Mungu kwamba hatawahi kumuacha. Akizungumza kwenye mahojiano na Mzazi Willy M. Tuva, msanii huyo amesema kwamba mafanikio yake katika maisha yameletwa na neema ya Mungu, hivyo basi hawezi kuziacha njia zake. Katika hatua nyingine Bahati ametusanua kuhusu ndoto yake ya kuwa rais wa Kenya mwaka wa 2037 kwa kusema kwamba amekuwa akiota ndoto hiyo kwa kipindi kirefu tangu alipokalia kiti cha rais kwenye mkutano wa kisiasa huko Kasarani. Utakumbuka Bahati alikuwa mgombea wa kiti cha ubunge eneo la Mathare kwenye uchaguzi mkuu uliokamilika juzi kati lakini kwa bahati mbaya alishindwa baada ya mpinzani wake Anthony Oluoch kuibuka kidedea kwenye kinyang’anyiro cha ubunge eneo hilo.

Read More
 BAHATI AWAJIBU WANAOMKOSOA MTANDAONI KWA KUSHINDWA UBUNGE MATHARE

BAHATI AWAJIBU WANAOMKOSOA MTANDAONI KWA KUSHINDWA UBUNGE MATHARE

Mwanamuziki aliyegeukia siasa, Bahati amewajibu kitaalamu wanaomubeza kwenye mitandao ya kijamii baada ya kupoteza kiti cha ubunge Mathare kwenye uchaguzi mkuu uliokamilika majuzi nchini Kenya. Katika mahojiano yake hivi karibuni Bahati amesema hatojutia maamuzi yake ya kuwania ubunge Mathare kwa kuwa amejifunza mambo mengi kwenye ulingo wa siasa licha ya kwamba zoezi zima la kuhesabu kura lilikumbwa na dosari. Hitmaker huyo wa “Adhiambo” amesema wanaomkosoa kwenye mitandao ya kijamii wanamuonea kijicho kutokana na hatua kubwa aliyopiga maishani. Utakumbuka baadhi ya mastaa akiwemo Willy Paul walimkejeli Bahati kwa kumpongeza mpinzani wake Anthony Oluoch ambaye ndiye mbunge mteule wa Mathare, kaunti ya Nairobi.

Read More
 BAHATI AWEKA WAZI GHARAMA YA KAMPEINI YAKE YA KISIASA

BAHATI AWEKA WAZI GHARAMA YA KAMPEINI YAKE YA KISIASA

Mwanamuziki Kevin Bahati Kioko maarufu kama Bahati ambaye pia ni mgombea Ubunge katika Jimbo la Mathare kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu nchini, amefunguka kiasi cha pesa ambacho ametumia hadi sasa kwenye kampeni zake. Kwenye mahojiano yake na Millard Ayo, Bahati ambaye anagombea nafasi hiyo kwa tiketi ya chama cha Jubilee amesema ametumia kiasi cha shillingi millioni 33 za Kenya kuendesha kampeni zake. Mbali na hilo Hitmaker huyo wa Adhiambo amesema ametenga zaidi ya KSh. 10 millioni kwa ajili ya siku ya Uchaguzi tu ambao utafanyika Kesho Jumanne huku akisisitiza kuwa pesa za kampeini zake za kisiasa zilitoka kwa wasamaria wema  wakiwemo marafiki pamoja na chama chake cha Jubilee. Hata hivyo Bahati ambaye anawania kiti cha ubunge eneo la Mathare kwenye uchaguzi wa Agosti 9 mwaka huu amedokeza kwamba ana mpango wa kuwania wadhfa wa juu kwenye uchaguzi wa mwaka wa 2037, akisema ni ndoto yake kuwa rais wa taifa la Kenya.

Read More