BAHATI AIDHINISHWA NA TUME YA UCHAGUZI NCHINI KENYA KUWANIA UBUNGE MATHARE

BAHATI AIDHINISHWA NA TUME YA UCHAGUZI NCHINI KENYA KUWANIA UBUNGE MATHARE

Mwanamuziki aliyegeukia siasa Bahati ameshindwa kuficha furaha yake baada ya tume ya IEBC kumuidhinisha kuwa atawania ubunge wa Mathare kwenye uchaguzi mkuu ujao kupitia Tiketi ya chama cha Jubilee. Kupitia ukurasa wake wa instagram bahati ameandika waraka mrefu wa kuwashukuru kumshukuru mungu, chama cha jubilee na watu wa mathare kwa kumpa nafasi ya kuwawakilisha kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti huku akitoa wito kwa wafuasi wake wampe kura ili aweze kuleta mabadiliko. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Adhiambo” amesema ndoto yake na watu wa mathare imetimia kwa kuwa wamekuwa wakiomba kwa muda kumpata mbunge ambaye ni mzaliwa wa eneo hilo. Wasanii wengine walioidhinishwa na IEBC ni mchekeshaji Jalang’o ambaye ni mgombea wa ubunge Lang’at kupitia cha cha ODM, na Mc Jessy ambaye ni mgombea wa ubunge Imenti Kusini.

Read More
 BAHATI AFIKISHA SUBSCRIBERS MILLIONI MOJA YOUTUBE

BAHATI AFIKISHA SUBSCRIBERS MILLIONI MOJA YOUTUBE

Nyota wa muziki nchini Bahati amefikisha idadi ya subscribers Milioni 1 kwenye mtandao wa Youtube. Bahati ambaye alijiunga na mtandao wa youtube Agosti 7, mwaka 2012  amepata subscribers wengi kutokana na kazi zake mbalimbali anazoziweka katika mtandao huo. Baadhi ya matukio anayoyaweka  katika channel yake ni shoo anazozifanya, video zake za muziki pamoja na utayarishaji wa video za nyimbo zake. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Adhiambo” hadi sasa Kupitia channel yake ya YouTube kazi zake zimetazamwa zaidi ya mara milioni  172 tangu ilipofunguliwa rasmi  channel yake ya youtube miaka 10 iliyopita. Bahati anakuwa msanii wa pili nchini mwenye wafuasi wengi katika mtandao wa youtube baada ya Oitle Brown ambaye ndiye alikuwa msanii wa kwanza nchini kufikisha subscribers milllioni moja youtube.

Read More
 BAHATI AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA RAILA ODINGA KUSHINDWA KUMTAMBUA JUKWAANI

BAHATI AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA RAILA ODINGA KUSHINDWA KUMTAMBUA JUKWAANI

Staa wa muziki nchini Bahati amezua gumzo mtandaoni mara baada ya mgombea wa urais kupitia Muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga kushindwa kumtambua akiwa jukwaani. Raila ambaye alikuwa anawatambulisha wagombea wa viti mbali mbali vya kisiasa kupitia Azimio la Umoja huko Kamkunji, jijini Nairobi alijipata amemuita Bahati jina la Mathew baada ya wandani wake kujaribu kumtambulisha msanii huyo kwake. Sasa jambo hilo limezuia mjadala mzito miongoni mwa wakenya kwenye mitandao ya kijamii ambapo baadhi wameonekana kumkejeli Bahati wakihoji ni kwa nini Raila alishindwa kumtambua msanii huyo mbele ya umma ikizingatiwa Bahti mwenyewe amekuwa akijinadi kwamba ana ukaribu na mgombea huyo wa urais kupitia muungano wa Azimio laUmoja. Hata hivyo wafuasi wa Raila Odinga wameonekana kumkingia kifua mwanasiasa huyo kwa kusema kwamba ana mambo mengi ya kuwaza kutokana na shinikizo za uchaguzi mkuu wa Agosti 9. Utakumbuka miezi kadhaa iliyopita Bahati aliachia wimbo wa uitwao “Fire” aliyomshirikisha Raila Odinga ambapo alimwagia sifa kinara huyo wa chama cha ODM kwenye azma yake ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu.

Read More
 BAHATI AKABIDHIWA CHETI CHA KUWANIA UBUNGE MATHARE KUPITIA CHAMA CHA JUBILEE

BAHATI AKABIDHIWA CHETI CHA KUWANIA UBUNGE MATHARE KUPITIA CHAMA CHA JUBILEE

Staa wa muziki nchini Bahati ameshindwa kuficha furaha yake baada ya kukabidhiwa tena cheti chake cha kuwania ubunge mathare kupitia  chama cha Jubilee Katika mkao na wanahabari bahati amemshukuru Rais Uhuru Kenyatta kwa kumpa nafasi tena kuwania ubunge kwa tiketi ya chama cha Jubilee na kinara wa ODM Raila Odinga kwa kumuamini kugombea ubunge wa mathare kupitia mwavuli wa Azimio la Umoja. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Adhiambo” amesema ndoto yake na watu wa Mathare imetimia kwa kuwa wamekuwa wakiomba kwa muda kumpata mbunge ambaye ni mzaliwa wa eneo hilo. Hata hivyo amewashukuru wajumbe wa Jubilee na wakaazi wa Mathare kwa ujumla kwa kumkingia kifua alipony’ang’anywa cheti cha jubilee wiki kadhaa zilizopita huku akitoa rai waendelee kumuunga mkono kwenye azma yake ya kuwa mbunge wa Mathare. Kwa sasa Bahati anatarajiwa kumenyana  na wapinzani wake kutoka vyama mbali mbali kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022.

Read More

BAHATI AFUNGUKA SABABU ZA KUTOWANIA BUNGE MATHARE KAMA MGOMBEA HURU

Staa wa muziki nchini Bahati ameweka wazi kuwa hatagombea kama mgombea binafsi kwenye kinyanganyiro cha ubunge wa mathare, siku chache baada ya kuangua kilio aliposhurutishwa na chama cha jubilee kujiuzulu wadhfa wa ubunge kwa ajili ya kumpa nafasi mbunge wa sasa tom olouch. Bahati amesema atakuwa amekisaliti chama chake cha Jubilee akiwania kiti ubunge mathare kama mgombea huru, jambo ambalo amedai hayuko tayari kukifanya. Katika mahojiano na Radio Maisha, Bahati hata hivyo ameshikilia kuwa bado ana Cheti chake cha Uteuzi na ana matumaini kuwa jina lake litawasilishwa kwa tume ya uchaguzi  IEBC leo. ‘Naweza kukuambia kitu? Unajua kwangu, sina haja na kuwa mgombea huru, kwa sababu nahisi hiyo ni kama kukisaliti chama changu na ninaamini pia chama hakitasaliti watu wao… kwa sababu … kina nafasi kwa vijana …’’ Bahati alisema. Msanii huyo aliyelelewa Mathare hata hivyo amesema kuwa amefanya mazungumzo na chama hicho baada ya kutakiwa kurejesha Cheti chake na hivyo amewatolea hofu wafuasi wake kuwa mambo yatakuwa mazuri hivi karibuni. “Mgombea wangu…waliitisha mkutano … nilifikiri chama kilitaka kunifadhili, lakini waliniomba nijiuzulu kama mgombea wa ubunge mathare kwa ajili ya mbunge wa sasa… Wanajua mashinani mambo yamebadilika… nimefanya mazungumzo upya na chama …” alifichua.

Read More
 BAHATI ANYANG’ANYWA CHETI CHA KUWANIA UBUNGE MATHARE

BAHATI ANYANG’ANYWA CHETI CHA KUWANIA UBUNGE MATHARE

Mwanamuziki aliyegeukia siasa Bahati amenyang’anywa tiketi ya kuwania ubunge wa Mathare kupitia chama cha Jubilee ikiwa ni siku chache zimepita tangu ashinde kwenye uchaguzi wa mchujo wa chama hicho. Katika mkao na wanahabari Bahati amesema alishurutishwa kujiuzulu kama mgombea wa kiti cha ubunge wa Mathare katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9 mwaka huu baada ya muungano wa Azimio la Umoja kuamua kumuunga mkono mgombea wa ODM ambaye ni mbunge wa sasa Tom Oluoch. Hata hivyo, amemtaka Kiongozi wa Chama cha Jubilee Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga kuwapa wakazi wa Mathare nafasi ya kumchagua mbunge wao wanayempenda kwa kuwa alijiunga na siasa baada ya kupewa shinikizo na wapiga kura wa eneo hilo. Utakumbukwa Mnamo Machi 18, Bahati alitangaza kuwa amejiunga na chama tawala cha jubilee na alikabidhiwa tikiti ya moja kwa moja na chama hicho kuwania kiti cha ubunge wa Mathare

Read More
 BAHATI NA DIANA MARUA WATANGAZWA MABALOZI WA OPPO KENYA

BAHATI NA DIANA MARUA WATANGAZWA MABALOZI WA OPPO KENYA

Kampuni ya OPPO inayojishughulisha na  uzalishaji na usambazaji wa simu na vifaa vingine vya kielectroniki imemtangaza rasmi  Bahati na mke wake Diana Marua kuwa mabalozi wake. Katika taarifa rasmi iliyochapishwa kwenye mtandao wa instagram katika page ya Oppo Kenya imeeleza kuwa wamefurahi kumkaribisha Bahati pamoja na Diana Marua kuwa balozi wa Oppo. “We partnered with @wabosha_maxine @bahatikenya @diana_marua to officially introduce you all to our newest model, the OPPO Reno 7!”,  Imesema sehemu ya chapicho hilo. Kwa upande mwingine Bahati amethibitisha pia katika chapisho lake kwenye mtandao wa Instagram kwa kusema kwamba amejisikia faraja kuwa balozi  wa OPPO na kuahidi kuitendea kazi katika kutangaza kampuni hiyo kupitia bidhaa zao za simu. “ANNOUNCEMENT‼️ JUST SIGNED AS THE NEW OPPO Reno 7 BRAND AMBASSADORS 🔥 So excited to partner with @oppo_kenya @wabosha.maxine and Wifey @Diana_Marua as we officially introduce to you the new OPPO Reno 7!”,  imesema taarifa hiyo. Wakati huo huo Oppo imeitambulisha simu yake mpya ya Oppo Reno ambayo imeingia hivi karibuni sokoni, simu hiyo yenye 8GB RAM + 250 GB ROM inatarajiwa kuuzwa kwa bei nafuu zaidi ili kumsaidia kila Mkenya kumiliki smartphone.

Read More
 BAHATI AFUNGULIWA MASHTAKA KWA KUSHINDWA KULIPA DENI LA SHILLINGI 150,000 ZA KENYA

BAHATI AFUNGULIWA MASHTAKA KWA KUSHINDWA KULIPA DENI LA SHILLINGI 150,000 ZA KENYA

Mwanamuziki aliyegeukia siasa nchini Kenya Bahati amefunguliwa mashtaka na kampuni ya ya mawakili ya Katunga Mbuvi & Co Advocates kwa madai ya kushindwa kumlipa mpiga picha mmoja shillingi 150000 baada ya kumfanyia kazi. Kupitia barua rasmi waliyomuandikia Bahati tarehe 30 mwezi machi mwaka huu,  kampuni hiyo imemtaka msanii huyo kumlipa mteja wao aitwaye Jeremiah Mathambu Thomas JT Shillingi 150,000 katika kipindi cha siku saba zijazo la sivyo watamfungulia kesi katika mahakama kuu ya nairobi. Barua hiyo imeibua hisia mseto miongoni mwa wakenya kwenye mitandao ya kijamii ambao wameonekana kupuzilia mbali tuhuma hizo wakisema kuwa ni njema ya kumchafulia jina Bahati ikizingatiwa kuwa Bahati ni msanii mkubwa ambaye tayari ana timu yake ya kupiga picha na kuchukua video hivyo hawezi mkodisha mtu wa nje. Hata hivyo mpaka sasa Bahati hajatoa tamko lolote kuhusu kashfa zilizoibuliwa na kampuni ya ya mawakili ya Katunga Mbuvi & Co Advocates dhidi yake ila ni jambo la kusubiriwa.

Read More
 MR. SEED AFUNGUKA MAZITO KUHUSU UKARIBU WAKE NA BAHATI

MR. SEED AFUNGUKA MAZITO KUHUSU UKARIBU WAKE NA BAHATI

Msanii nyota nchini Mr Seed amemuandika waraka mrefu msanii mwenzake Bahati baada ya hitmaker huyo wa ngoma ya Adhiambo kuweka wazi azma yake ya kuwania ubunge wa Mathare kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Kupitia waraka huo ambao aliuandika kupitia ukurasa wake wa Instagram Mr. Seed ameeleza namna alivyokula maisha ya taabu na bahati wakiwa wanaishi mathare, kipindi ambacho walikuwa wanajaribu kupenya kwenye kiwanda cha muziki nchini. Kulingana na Hitmaker huyo wa ngoma ya “Around”, umaskini ulikuwa sehemu ya maisha yao na haikuwazuia kuwaza mambo makubwa ambayo walikuwa wanatamani kufanikisha katika maisha yao. Mr. Seed ambaye ni bosi wa lebo y muziki ya Starbon ametangza kumuunga mkono bahati kwenye azma yake ya kuwa mbunge wa mathare kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka wa 2022 ambapo amemtaja msanii huyo kama kiongozi ambaye anawafaa wakaazi wa eneo hilo. Itakumbukwa mapema mwaka wa 2019 mr seed waliingia kwenye bifu na bahati baada msanii huyo kuigura lebo ya muziki ya EMB ambako alikuwa amesainiwa kwa kipindi cha miaka miwili. Lakini ilikuja ikabainika baadae kuwa bifu ya wawili hao ilisababishwa na ugomvi ulioibuka kati ya wake zao.

Read More
 BAHATI ATANGAZA KUFANYA HOME COMING YAKE WIKIENDI HII HUKO MATHARE, NAIROBI

BAHATI ATANGAZA KUFANYA HOME COMING YAKE WIKIENDI HII HUKO MATHARE, NAIROBI

Nyota wa muziki nchini Bahati ametangaza kufanya ziara yake iitwayo ‘Bahati Mtoto wa Mama Home Coming’ Machi 27 mwaka huu katika uwanja wa Huruma grounds, Kaunti ya Nairobi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram hitmaker huyo wa ngoma ya “Adhiambo” amesema amehamua kuja na ziara hiyo kwa ajili ya kunadi sera zake kwa wakaazi wa Mathare kama mbunge wao mtarajiwa kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu. Mbali na hayo, amesema kutakuwepo na fainali za soka katika uwanja wa Mathare Grounds ambapo timu ya Asec Huruma FC itachuana na Oostrom FC kwenye fainali huku Lucio FC ikicheza na True Colours FC kwenye mchezo wa kutafuta timu itakayochukua nafasi ya tatu. Hata hivyo Bahati amesema timu ambayo itaibuka kidedea kwenye fainali hizo itatunukiwa shillingi elfu 150 huku nafasi ya pili na tatu ikizawadiwa shillingi elfu 100 na 50 mtawalia. Utakumbuka Bahati anawania kiti cha ubunge eneo la Mathare kupitia tiketi ya chama cha Jubilee.

Read More
 MWANAMUZIKI BAHATI KUWANIA URAIS NCHINI KENYA MWAKA 2037

MWANAMUZIKI BAHATI KUWANIA URAIS NCHINI KENYA MWAKA 2037

Staa wa muziki nchini Bahati ametangaza nia ya kugombea kiti cha Urais nchini Kenya kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2037. Bahati ameyaweka wazi hayo mbele ya waandishi wa habari alipokuwa akizindua azma yake ya kuwania ubunge wa mathare kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu kwa kusema kuwa ana nia njema kwa wananchi wa Kenya kwani ana vigezo vya kutosha ya kuwa kiongozi atakayeleta mabadiliko nchini. Hitmaker huyo wa ngoma “Adhiambo” amedai kwamba hana mpango wa kuacha muziki licha ya kwamba ametia nia ya kuomba ridhaa ya ubunge wa eneo la Mathare. Lakini pia Bahati ameweka wazi mpango wa kuachia EP yake mpya mwezi Mei mwaka huu wakati atakapokuwa anaendeleza kampeini yake ya kujipigia debe kwenye azma ya kuwania ubunge wa Mathare.

Read More
 BAHATI ATANGAZA MSIMAMO WAKE KISIASA, AACHIA WIMBO UNAOMPIGIA DEBE RAILA ODINGA KWENYE AZMA YAKE YA URAIS.

BAHATI ATANGAZA MSIMAMO WAKE KISIASA, AACHIA WIMBO UNAOMPIGIA DEBE RAILA ODINGA KWENYE AZMA YAKE YA URAIS.

Staa wa muziki nchini Bahati amehamua kutangaza msimamo wake wa kisiasa ikiwa ni siku chache imepita tangu msanii mwenzake Willy Paul atangaze kumuunga mkono kinara wa ODM Raila Odinga. Kupitia wimbo wake mpya uitwao Fire ambao amemshirika Raila Odinga bahati ameonekana kumwagia sifa kinara huyo wa chama odm jambo ambalo limetafsiriwa moja kwa moja kuwa amehamua kumuunga mkono odinga kwenye azma yake ya kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu kupitia muungano wa Azimio la umoja. Hata hivyo wimbo huo wa Bahati umeibua hisia mseto miongoni mwa mashabiki zake ambapo wengi wameonekana kumpongeza kwa hatua ya kuweka msimamo wake kisiasa huku wengine wakimkosoa kwa hatua ya kuukimbia mrengo wa kenya kwanza ambao unaongozwa na naibu wa raias dakta William Ruto kupitia chama chake cha UDA. Utakumbuka mwaka wa 2021 Bahati pia alitangaza kumuunga mkono naibu rais dakta William Ruto kwenye azma yake ya kuliongoza taifa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Read More