DIANA B AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU TETESI ZA UJA UZITO

DIANA B AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU TETESI ZA UJA UZITO

Youtuber kutoka nchini Kenya ambaye pia ni rapa Diana B, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu ishu ya kupata mtoto wa tatu na mume wake Kevin Bahati. Katika mahojiano yake hivi karibuni Diana B amesema sio mbaya akimpata mtoto mwingine huku akisisitiza kwamba watoto ni baraka kutoka kwa Mungu. Bi Marua pia ameweka wazi kuwa kupata mtoto mwingine itakuwa zawadi bora zaidi kwa mumewe Bahati ambaye pia ni mwanamuziki. “Ikiwa kuna mtoto mwingine anakuja, ni sawa. Watoto ni baraka na nikiongeza kifungu kingine katika familia yangu, na nadhani hiyo ndiyo baraka bora zaidi ninayoweza kumpa mume wangu Bahati,” alisema Diana. Kauli ya Diana B imekuja mara baada ya walimwengu kwenye mitandao ya kijamii kuhoji kuwa huenda rapa huyo ana uja uzito na anatarajia kupata mtoto katika siku za hivi karibuni.

Read More
 DIANA B AKUTANA NA ALIYECHORA TATTOO YAKE

DIANA B AKUTANA NA ALIYECHORA TATTOO YAKE

Mke wa msanii Bahati na YouTuber maarufu nchini Kenya, Diana Marua amekutana na Rose Waithera ambaye alivuma mtandaoni baada ya kuchora tattoo ya Diana kwenye mgongo wake. Baada ya wiki kadhaa hatimaye Diana alimtembelea mwanafunzi huyo wa chuo cha urembo katika mtaa wa Githurai na kufanya naye mazungumzo. Waithera amesema aliamua kuchora tattoo ya mama huyo wa watoto wawili kwa kuwa anamshabikia sana na huwa anatamani kuwa kama yeye. “Huwa napenda haiba yako, napenda sifa zako, huwa natamani kuwa kama wewe, uko na nyumba ya kifahari, uko na mume mzuri mwenye anakupamba kila wakati, uko na watoto wazuri. Sijawahi kupata mtu yupo na roho kama yako, ningependa kuwa kama wewe, nakupenda,” Waithera alimwambia Diana. Mwanadada huyo amesema alianza mipango ya kuchorwa tattoo hiyo Desemba mwaka jana, huku akiri kwamba alikosolewa sana baada ya kuchorwa tattoo hiyo ila hana majuto yoyote kwa kile alichofanya.

Read More
 DIANA B AKOSHWA NA SHABIKI ALIYECHORA TATTOO YENYE USO WAKE MGONGONI

DIANA B AKOSHWA NA SHABIKI ALIYECHORA TATTOO YENYE USO WAKE MGONGONI

Mwanamitandao aliyegeukia muziki nchini Diana B amefurahishwa sana na kitendo alichofanyiwa na shabiki yake ya kujichora Tatoo yenye uso wake mgongoni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diana B ameshindwa kuficha furaha yake kwa shabiki huyo ambapo amewataka watumiaji wa  mitandao ya kijamii wamsaidie kumtafuta mrembo huyo ili aweze kukutana nae kwani amekoshwa na upendo ambao amemuonyesha kwa kuchora tattoo ya uso wake. Kauli ya Diana B imekuja mara baada ya binti mmoja ambaye ni shabiki yake kuchora tattoo ya uso wa msanii huyo kama njia ya kumuonyesha upendo kwani anazikubali nyimbo zake. Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wametilia shaka tattoo ya mrembo huyo wakihoji kuwa heunda Diana B amemlipa mrembo achore tattoo yenye uso wake mgongoni kama njia ya kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa kwenye vyombo vya habari.

Read More
 DIANA B ALAMBA DILI NONO LA UBALOZI PHOINA BEAUTY COSMETICS

DIANA B ALAMBA DILI NONO LA UBALOZI PHOINA BEAUTY COSMETICS

Mwanamitandao aliyegeukia Muziki nchini Diana B amelamba dili la nono la kuwa balozi mpya wa kampuni ya bidhaa za urembo iitwayo Phoina Beauty Cosmetics. Diana B ameshare habari hiyo njema kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Instagram akieleza kwamba ana furaha kujiunga na familia ya Phoina Beauty Cosmetics. Kwa mafanikio hayo Diana B atatakiwa kutangaza na kuwashawishi wafuasi wake wazinunue bidhaa hizo za urembo wa ngozi za Phoina Beauty Cosmetics kupitia mitandao yake ya kijamii. Bado haijajulikana amelipwa kiasi gani kwa kuitangaza bidhaa hiyo lakini Diana B sio mgeni katika uteuzi wa kuwa balozi wa bidhaa za makampuni kwani mwaka wa 2021 alilamba shavu ya kuwa balozi wa kampuni ya Unga wa ugali wa Raha Premium. Hata hivyo mashabiki zake wameonekana kumpongeza kwa mafanikio hayo huku wengine wakitilia shaka ubalozi wake huo na kampuni ya Phoina Beauty Cosmetics ikizingatiwa kuwa balozi wa kwanza wa kampuni hiyo Amber Ray aliingia kwenye ugomvi mzito na mmiliki wa  Phoina Beauty Cosmetics kutokana na ishu ya malipo.

Read More
 BAHATI AWAJIBU WALIMWENGU BAADA YA KUTILIA SHAKA ZAWADI ANAZOMPA MKE WAKE DIANA MARUA

BAHATI AWAJIBU WALIMWENGU BAADA YA KUTILIA SHAKA ZAWADI ANAZOMPA MKE WAKE DIANA MARUA

Staa wa muziki nchini Bahati amewajibu watu wanaotilia shaka vitu vya thamani ambavyo amekuwa akimzawadi mke wake Diana B katika miaka ya hivi karibuni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram bahati amesema kuwa vitu vyote ambavyo amekuwa akimpa mke wake vinatoka kwa mungu ambaye alimtoa kwenye lindi la umaskani katika mitaa ya mabanda ya mathare. Hitmaker huyo wa ngoma “Adhiambo” ameenda mbali na kuwapa changamoto watu wanaombeza mitandao wawe na imani pamoja na subira katika maisha kwani mungu pekee ndiye ana uwezo wa kubadilisha maisha ya mtu. Kauli ya Bahati inakuja mara baada ya shabiki mmoja mapema wiki hii kuhoji kuwa wawili hao ni jirani zake lakini hajawahi mwona diana akiendasha magari mawali aina Mercedez ambazo alipatiwa awali ila amekuwa akimwona akiendesha gari aina na vitz. Siku ya valentines Bahati alimzawadi Diana Marua gari la shillingi million 10 aina ya Land Cruiser TX pamoja na jumba la kifahari lilogharimu shillingi million 27. Tukio hili lilipelekea mashabiki kwenye mitandao kuhoji kuwa huenda ni kiki wawili hao wanafanya

Read More
 STAA WA MUZIKI NCHINI KENYA BAHATI AMZAWADI MKE WAKE DIANA B MJENGO WA KIFAHARI

STAA WA MUZIKI NCHINI KENYA BAHATI AMZAWADI MKE WAKE DIANA B MJENGO WA KIFAHARI

Upendo wa Staa wa muziki nchini Bahati kwa baby mama wake Diana B unazidi kuongezeka kila uchao. Baada ya kumnunulia gari aina Prado TX kama zawadi ya siku ya wapendanao duniani amekuja na suprise nyingine kwa mke wake huyo. Kupitia ukurasa wake wa instagram hitmaker huyo wa ngoma ya “Adhiambo” amepost mjengo wa kifahari ambao amezawadi mke wake Diana B  na kusema kwamba ameahamua kumpa zawadi hiyo kama njia ya kumuonyesha upendo kwa kusimama nae kwenye shida na raha. Hata hivyo mashabiki na mastaa mbali mbali wameonekana kufurahishwa na hatua ya Bahati kumuonyesha upendo baby mama wake huku wakimpongeza kwa mafanikio makubwa maishani.  

Read More
 BAHATI AMZAWADI MKE WAKE DIANA MARUA GARI AINA YA LAND CRUISER PRADO TX

BAHATI AMZAWADI MKE WAKE DIANA MARUA GARI AINA YA LAND CRUISER PRADO TX

Wakati ukichukulia poa siku ya Valentines, Staa wa muziki nchini Kenya Bahati  hakuwa na jambo dogo kwa Baby Mama wake Diana B , kwani amempatia zawadi ya gari aina ya Land Cruiser Prado TX yenye thamani ya shillingi millioni 6.9. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diana B ametoa shukrani za dhati kwa mumewe Bahati kwa zawadi hiyo ya kitofauti ambayo hakuitegemea,ikizingatiwa kuwa Land Cruiser Prado TX ni gari ya ndoto yake. “Sina neno, sina la kusema, Sipumui. Asante mpenzi Bahati. Tumetoka mbali na tunaweza kufika mbali zaidi kutoka hapa. Umetimiza ndoto zangu zote”. “Gari hili ni zawadi yangu kwa bidii yangu katika kutengeneza content, bado nimeshtuka. Shukran. Sijui nilifanya nini ili nistahili wewe. Kila siku, namshukuru Mungu kwa ajili yako. Daima akupe neema kati ya wanaume wengine. Nakupenda Bahati” amesema. Hii sio mara ya kwanza kwa Bahati kumnunulia mkewe wake Diana B zawadi za mkwanja mrefu kwani kipindi cha nyuma alimzawadi gari aina ya Mercedes Benz wakisherekea mitano ya ndoa lakini pia aliwahi kumnunulia shamba ya hekari mbili kama zawadi ya kumbukizi yake ya kuzaliwa

Read More
 DIANA B AIREJESHA CHANELI YAKE YA YOUTUBE BAADA YA KUFUTWA NA WADUKUZI

DIANA B AIREJESHA CHANELI YAKE YA YOUTUBE BAADA YA KUFUTWA NA WADUKUZI

Mwana mitandao aliyegeukia muziki Diana Marua amefanikiwa kurejesha akaunti ya Youtube ambayo ilikuwa imedukuliwa mapema wiki hii. Kupitia ukurasa wa instagram Diana Marua ameshindwa kuficha furaha yake kwa kuipongeza kampuni ya ngoma na uongozi wa Youtube kwa kumsaidia kuirejesha chaneli yake ya youtube yenye subscribers laki 5. Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kutofautiana kimawazo na Diana Marua ambapo wameenda na kumshambulia hitmaker huyo wa “One Day” aache suala la kutengeneza kiki mwenyewe kwani aliifuta akaunti yake ya youtube kwa ajili ya kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa nchini kabla ya ujio wa wimbo wake mpya. Utakumbuka juzi kati mumewe Bahati alitangaza kuwa Diana B ataachia wimbo wake mpya januari 25 mwaka huu lakini baada ya wadukuzi kuifuta chaneli ya youtube ya mrembo huyo ilibidi mchakato wa kuachia ngoma hiyo iahirishwe.

Read More
 DIANA MARUA APOTEZA AKAUNTI YA YOUTUBE KWA WADUKUZI

DIANA MARUA APOTEZA AKAUNTI YA YOUTUBE KWA WADUKUZI

Mwanamitandao aliyegeukia muziki  Diana Marua amepata pigo kubwa baada ya kupoteza chaneli yake  ya YouTube kwa wadukuzi. Diana Marua ametumia ukurasa wake wa Instagram, kutangaza taarifa  hiyo mbaya kwa mashabiki zake ambayo imemuacha akikadiria hasara. Akaunti hiyo yya youtube ambayo ilidukuliwa ilikuwa na zaidi ya subscribers laki 6 tangu ajiunge na mtandao huo Agosti 19 mwaka wa 2019. Marua mwenye uhuzuni amesema kwamba wadukuzi walianza kwa kubadilisha jina lake la Yoiutube kabla ya kuifuta akaunti yake hiyo. “😭😭😭😭😭😭😭😭 Nimeishi kwa amani na kila mtu na siku zote nimekaa kwenye njia yangu; Sijui kwanini mtu yeyote angenifanyia hivi! Unadukua akaunti yangu ya YouTube; badilisha jina na mbaya zaidi unaifuta 😭😭😭😭😭😭😭😭,” alisema. Hata hivyo, mwimbaji huyo wa One Day amewahakikishia mashabiki wake kwamba suala hilo linashughulikiwa na usimamizi wake na ana matumaini kwamba mambo yatarejea kama kawaida. Katika ukaguzi uliofanywa na mwandishi huyu hukupa ujumbe unaosomeka: “Video haipatikani. Video hii haipatikani tena kwa sababu akaunti ya YouTube inayohusishwa na video hii imesimamishwa. Chaneli ya Marua ilidukuliwa wakati alikuwa miongoni mwa WanaYouTube mashuhuri nchini Kenya ikizingatiwa kuwa  amekuwaa akipata idadi kubwa ya watazamaji  kila wakati anapopakia maudhui kwenye akaunti yake ya youtube..

Read More