Harmonize akanusha kumdai Anjella shillingi millioni 52

Harmonize akanusha kumdai Anjella shillingi millioni 52

Bosi wa lebo ya Konde Music Worldwide, Msanii Harmonize ameamua kuvunja kimya chake juu ya stori zinazotembea mtandaoni kuhusu kumkimbia msanii wake Anjella. Kupitia instastoy yake Harmonize ameweka wazi kuwa ni kweli amefika mwisho wa kumsapoti Anjella, hivyo kwa yeyote mwenye uwezo anaruhusiwa kumshika mkono msanii huyo bila pingamizi. Hitmaker huyo wa “Leave Me Alone amesema kuwa hamdai pesa yoyote Anjella kama malipo ya kuachana na lebo ya Konde Gang huku akiwataka watu kupuuza mambo ya uongo yanayoendelea mtandaoni. “Nilikutana na Anjella akiwa amejikatia tamaa akiwa na ndoto kichwani, sikujiangalia nina kiasi gani niliamini kuwa wapo wanaonisapoti bila kuwalipa senti 5 basi watasapoti kipaji cha sister Anjella”. “Nilichoangalia ni ndoto hasa za mtoto wa kike nimejitahidi kadri ya uwezo wangu najua kuna wenye uwezo mkubwa kunizidi ukizingangatia nimeanza juzi” “Kama kuna anayeweza kumuendeleza kipaji chake ni faraja kwangu asisite kujitokeza. Puuzia siasa za kusema sijui namdai mahela sikumuuliza kuhusu pesa hata senti 1”

Read More
 Harmonize atangaza utaratibu mpya wa Promotion ya Album yake mpya.

Harmonize atangaza utaratibu mpya wa Promotion ya Album yake mpya.

Staa wa muziki nchini Harmonize ametangaza rasmi hatoifanyia promotion album mpya kama ilivyoozeka kwa wasanii wengine kufanya mkutano na waandishi wa habari, Ziara kwenye vyombo vya habari, kuweka bango lolote barabarani au kufanya listening party. Harmonize amebainisha hayo kupitia insta story yake kwa kueleza kwamba ameshafanya kila kitu (studio), hivyo anataka mashabiki wasikilize muziki mzuri aliouandaa. Na pia ameongeza, ikiwezekana ataishare mara moja tu kwenye platform zake. Kauli ya Harmonize imekuja mara baada ya kutangaza kuachia Album yake ya tatu itwayo Made For Us Oktoba 28 mwaka huu na tayari ametuonesha Tracklist yenye Jumla ya nyimbo 14.

Read More
 Harmonize adai kusepa na hela ya promota wa Nigeria

Harmonize adai kusepa na hela ya promota wa Nigeria

Promota wa show kutoka Nchini Nigeria Deejay Chii analalamika kuwa msanii wa Bongofleva Harmonize ameshindwa kufanya show nchini Canada baada ya kulipwa kiasi cha Kshs. millioni 1.2. Kupitia video inayosambaa mtandaoni Deejay Chii anasema licha ya kuwa walishafanya makubaliano na Harmonize kiasi cha kumlipa pesa zote alizokuwa anahitaji, Hitmaker huyo wa “Leave Me Alone” ameingiwa na jeuri ya kutopokea simu zake mpaka muda huu. Kwa mujibu wa promota huyo anasema kwamba tayari jambo hilo amelifikisha mikononi mwa polisi nchini Tanzania na linafanyiwa kazi. Harmonize alitakiwa kutumbuiza kwenye miji mitatu nchini Canada kuanzia Oktoba 7 hadi Oktoba 10 , 2022. Hata hivyo mpaka sasa Harmonize hajajibu chochote kuhusiana na tuhuma hizo ila ni jambo la kusubiriwa.

Read More
 Cheed na Killy wafuta urafiki na Harmonize Instagram

Cheed na Killy wafuta urafiki na Harmonize Instagram

Wasanii Cheed na Killy huenda kwa sasa wakawa hawataki kuona chochote kuhusu Harmonize. Wawili hao wameamua kumu-unfollow bosi wao huyo wa zamani katika kurasa zao za Instagram baada ya lebo ya Konde Music Worldwide kusitisha mkataba wao kwa sababu ambazo hawakuziweka wazi. Utakumbuka mwisho mwa wiki iliyopita, Cheed na Killy waliwasilisha lalama zao kwa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kupata mwanga kuhusu sakata la kutimuliwa kwao. Lakini kikao cha kutatua mgogoro wao na lebo hiyo hakikuweza kufanyika baada ya uongozi wa Konde Music Worldwide kushindwa kufika Basata.

Read More
 Harmonize ajiweka namba mbili kwa ukubwa duniani.

Harmonize ajiweka namba mbili kwa ukubwa duniani.

Staa wa muziki wa Bongofleva Harmonize ameendelea kushusha sifa kwa mwanamuziki wa Nigeria Burna Boy kwa hatua kubwa anazopiga katika muziki wake kimataifa na kusema kuwa wapambanaji pekee ndio wanaweza kumuelewa. Kupitia instastory yake ameshare ujumbe akisisitiza kuwa Burna Boy ndiye msanii namba moja kwa sasa Afrika huku akitaja baadhi ya matukio aliyojifunza kutoka kwa Staa huyo kipindi yupo Lagos, Nigeria na kusema kuwa hakuwahi kumsikia Burna Boy akimzungumzia mtu vibaya lakini pia akijisifia juu ya mafanikio yake na tuzo alizonazo . Mbali na hayo, Harmonize amesema kila mtu ana uhuru wa kumtaja Staa anayehisi ni namba moja kwa sasa barani Afrika lakini wasisahau kuwa yeye ndio anayefuata baada ya Burna Boy. Harmonize na Burna Boy tayari wameshafanya nyimbo mbili za pamoja ambazo ni Kainama inayopatikana kwenye Afro Bongo EP ya mwaka wa 2018 pamoja na Shake your body inayopatikana kwenye album ya Afro East ya mwaka wa 2018.

Read More
 Harmonize azima tetesi za lebo ya Konde Gang kufilisika

Harmonize azima tetesi za lebo ya Konde Gang kufilisika

Mwanamuziki kutoka nchini Tanzania Harmonize amewafunga mdomo wale wote waliodhani kuwa ameshindwa kuendesha lebo ya Konde Gang. Kupitia insta stori yake kwenye mtandao wa Instagram amefichua mpango wa kutambulisha makao mapya ya lebo hiyo sambamba na kuwasajili wasanii wapya Oktoba 10 mwaka huu wakati Konde Gang itaandhimisha miaka mitatu tangu kuzinduliwa kwake. Hitmaker huyo wa “Leave Me Alone” amewashukuru mashabiki kwa kusimama na lebo ya Konde Gang huku akisisitiza kuwa lebo hiyo itaendelea kukuza vipaji vya vijana wasiojiweza kwenye jamii. Kauli ya Harmonize imekuja mara baada ya picha kusambaa kuwa Makao Makuu ya lebo ya Konde Gang yanapigwa mnada na pia kuna wasanii wanaondoka kwenye lebo hiyo.

Read More
 HARMONIZE AFUNGUKA CHANZO CHA SARAH KUKIMBIA MAHAKAMANI

HARMONIZE AFUNGUKA CHANZO CHA SARAH KUKIMBIA MAHAKAMANI

Bosi wa Konde Music Worldwide, Msanii Harmonize ameendelea kutoa ya moyoni baada ya aliyekuwa mke wake, Sarah kwenda Mahakamani. Katika mazungumzo na mchumba wake wa sasa Kajala Masanja, amesema sababu ya Sarah kudai talaka ni kuwa anataka wagawane mali. Msanii huyo amedai kuwa hakuna mali yoyote ambayo anapaswa kugawana na mwanamitindo huyo kutoka Italia huku akibainisha kuwa aliondoka bila chochote wakati walipoachana mwishoni mwa mwaka 2020. Hata hivyo Harmonize anapanga kuandika talaka tatu baada ya ex-wake huyo kuwasilisha kesi mahakamani kudai talaka yake. Utakumbuka Harmonize na Sarah walifunga ndoa Septemba mwaka 2019 na waliachana Desemba mwaka 2020 ukiwa ni mwaka mmoja tu wa ndoa yao.

Read More
 HARMONIZE AMWAGIA SIFA KAJALA, ADAI HAKUNA MWANAMKE MZURI ZAIDI YAKE

HARMONIZE AMWAGIA SIFA KAJALA, ADAI HAKUNA MWANAMKE MZURI ZAIDI YAKE

Penzi la Harmonize na mchumba wake Kajala Masanja linazidi kushamiri kila kukicha na kuwafanya wenye makasiriko kusubiriwa wajinyonge. Kupitia mfululizo wa Instastory zake, Harmonize amemwagia sifa kajala kwa kusema kuwa hakuna mwanamke mzuri kwa sasa anayemzidi mwanamama huyo. Harmonize ambaye anafanya vizuri na ngoma zake mbili, “Nitaubeba” pamoja na “Amelowa” anasema kwamba penzi lao linazidi kuwa la moto kila siku na kama kuna mtu anatarajia litabuma basi avute kiti akae kwa sababu atasubiri sana. Kauli ya Harmonize inakuja mara baada ya Kajala kuchora tattoo yake kwenye kidole cha pete; tattoo yenye herufi ya ‘R’ ikiwa ni herufi ya kwanza ya jina la Rajabu ambalo ndilo jina halisi la Harmonize.

Read More
 HARMONIZE AFICHUA KUWEKEZA KWENYE KILIMO CHA MIWA

HARMONIZE AFICHUA KUWEKEZA KWENYE KILIMO CHA MIWA

Huenda msanii wa Bongofleva Harmonize ameamua kuwekeza katika kilimo cha miwa. Hii ni baada ya kushare video clip akiwa katika shamba la miwa na kudai ni mara ya kwanza kufika kwenye shamba hilo. Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Harmonize ametoa changamoto kwa vijana kuwekeza katika aina hiyo ya kilimo kama njia ya kujikwamua kiuchumi. “Kuna Maisha Baada Akicheza Pesa Zako Zote Club” Huku Akiwa Katika Shamba La Miwa”. Ameandika kwenye caption ya video clip yake. Hata hivyo inatajwa kuwepo na uwezekano wa msanii huyo kutoka Konde Gang kuwa amelamba dili lingine la ubalozi katika kampuni moja ya Sukari nchini Tanzania.

Read More
 PAULA KAJALA AMUITA HARMONIZE BABA KWA MARA YA KWANZA

PAULA KAJALA AMUITA HARMONIZE BABA KWA MARA YA KWANZA

Hatimaye mtoto wa mpenzi wa mwanamuziki Harmonize, Kajala Masanja, aitwaye Paula kwa mara ya kwanza amemtambua Harmonize kama baba yake hadharani kupitia ukurasa wake wa instagram (insta story yake). Paula amemtaja Harmonize kama baba yake akishare kionjo cha wimbo mpya wa Harmonize uitwao Amelowa. Kupitia Instastory yake Paula amepost video hiyo na kisha kuandika “Baba unajua mpaka unajua tena”. Paula hakuishia hapo ameenda mbali zaidi na kuandika, “Utaweza kukomoana na Jeshi wewe?”. Utakumbuka wawili hao wamewahi kuwa katika tofauti kubwa kiasi cha Paula kutomtambua Harmonize kama baba yake alipomvisha mama yake Kajala Masanja pete ya uchumba, kitendo kilichopelekea walimwengu kuhisi kuwa bado ana kinyongo na baba yake Harmonize.

Read More
 HARMONIZE KUISHTAKI KAMPUNI YA UCHINA KWA TUHUMA ZA WIZI

HARMONIZE KUISHTAKI KAMPUNI YA UCHINA KWA TUHUMA ZA WIZI

Staa wa muziki wa Bongofleva Harmonize amemtaka meneja wake Kajala Frida kuichukulia hatua za kisheria kampuni moja kutoka China ambayo inatengeneza cheni zenye chapa yake ya Konde Boy. Kupitia Insta story yake kwenye mtandao wa Instagram, Harmonize ameeleza kwamba bila makubaliano yoyote, kampuni hiyo inatengeneza pesa kupitia chapa (brand) yake na inaziuza cheni hizo katika tovuti mtandaoni. “Big brand in China. Am not getting any money out of it. Manager do something please @kajalafrida ” – ameandika Harmonize. Aidha, madai ya namna hii yamekuwa yakitokea sana kwa mastaa kuhusiana na chapa zao kuigwa na kutengenezewa bidhaa na watu wengine bila makubaliano yoyote. Sanjari na hilo amewapa utaratibu mpya mapromota wanapompatia show huku akiwataka wahakikishe kuna tiketi mbili za ndege daraja la juu (Business) ambapo moja yake na nyingine ya meneja wake Kajala. Pia ziwepo nyingine nane za kawaida (Economy) kwa timu yake na watu wa bendi.

Read More
 HARMONIZE AMVISHA PETE YA UCHUMBA KAJALA MASANJA

HARMONIZE AMVISHA PETE YA UCHUMBA KAJALA MASANJA

Msanii wa Bongofleva Harmonize amemvisha pete ya uchumba Mwigizaji Kajala Masanja ikiwa ni siku chache toka wawili hao warudiane baada ya penzi lao kuvunjika kipindi cha nyuma. Tukio hilo limefanyika Jumamosi Juni 25,mwaka 2022  katika hoteli ya Serena huku likihudhuriwa na watu wa karibu wa wasanii hao ukiwemo uongozi wa lebo ya Konde Gang. Wakati wa tukio hili Harmonize amekiri kwamba Kajala ni Mwanamke bora kwake na kuna wakati Kajala alimpa hifadhi kwenye nyumba yake wakati Harmonize akiwa hana nyumba. Harmonize na Kajala wamechumbiana ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu walipotengana baada ya mwanamuziki huyo kumfungulia mashtaka Kajala na binti yake Paula akiwatuhumu kuvujisha picha zake za utupu

Read More