PENZI LA HARMONIZE LAMPONZA KAJALA

PENZI LA HARMONIZE LAMPONZA KAJALA

Hakuna ubishi kuwa penzi la Staa wa Bongofleva toka Konde Music, Harmonize na Kajala linaendelea kutaradadi kila uchao baada ya wawili hao kurudiana wiki kadhaa zilizopita. Kwa sasa Harmonize yupo katika ziara ya kimuziki jijini Goma, DR Congo na kwa kweli Kajala ameshindwa kuvumilia upweke nyumbani. Muigizaji huyo ametumia ukurasa wake wa Instagram kuthibitisha mahaba yake kwa Harmonize na kumueleza jinsi anayompeza. “I miss you @harmonize_tz,” Kajala aliandika kwenye Insta story yake. Ujumbe huo ulijiri masaa machache tu baada ya Harmonize kutengeneza video kwa ajili ya mpenzi huyo wake. Katika video hiyo Harmonize alionyesha upendo mkubwa kwa Kajala wakati anapokelea Dt Congo na kusema kuwa yuko pale ili kumfanya Kajala ajivunie. “Nataka ujue kuwa niko hapa na nakupend sana. Najua uko mbali lakini sina la kufanya kwa sababu najua unajiandaa kwa siku yetu kubwa, najuvunia wewe na niko hapa kukufanya ujivunie,” alisema Harmonize. Mwanamuziki huyo pia alitumia video hiyo kumshukuru mpenzi wake huyo kwa kumpa motisha ya kuchapa kazi yake ya muziki

Read More
 HARMONIZE AWAPA SOMO WANAUME, TAFUTENI HELA

HARMONIZE AWAPA SOMO WANAUME, TAFUTENI HELA

Msanii mkubwa wa muziki nchini Tanzania na CEO wa Lebo ya Konde Music amewashauri wanaume kutafuta hela ili kuboresha uhusiano kati yao na wapenzi wao. Kwa mujibu wa Harmonize, hatua ya kuomba msamaha huwa rahisi zaidi wakati mwanaume anapomsapoti mpenzi wake kihela, Alishauri kwamba mwanaume anapaswa kutumia hela kumfanya mwanamke asahau makosa yake badala ya kumtumia jumbe nyingi za kuomba msamaha. “Tafuta hela ukishakuwa nazo ndiyo utajua msamaha unaombwaje. Hizo SMS zako unamjazia WhatsApp unazidi kumuumiza na kumkumbusha machungu. Mfanye asahau babuu. Mpeleke katika dunia nyingine,” anasema Konde Boy Mjeshi. Harmonize anasema hayo wiki chache tu baada ya kumwaga mamilioni ya pesa katika juhudi za kumuomba msamaha mpenzi wake, Kajala Masanja.

Read More
 FRIDAH KAJALA ATAMBULISHWA KAMA MENEJA WA HARMONIZE

FRIDAH KAJALA ATAMBULISHWA KAMA MENEJA WA HARMONIZE

Ni Rasmi sasa mwanadada Fridah Kajala ni meneja wa Lebo ya Konde Music Worldwide. Kajala ameongezeka kwenye uongozi wa Konde music ikiwa ni tamanio la Harmonize ambaye ndiye CEO wa lebo hiyo, kumtaka asimamie biashara yake ya Muziki. Kajala ametangazwa rasmi na Choppa_ambaye ni mmoja wa mameneja wa Harmonize, kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika; “Allow Me To Welcome In Management Team New C.E.O And Manager Kajala Frida I’m Excited To Work With You Shem #kondegang4you“. Naye Harmonize alishusha comment kwenye posti hiyo yenye maneno yanayosomeka; “Big Team, Big Dream” huku Kajala akiachia emoji za moto na kuonyoosha mikono juu. Utakumbuka, Harmonize kabla hajarudiana na mpenzi wake Kajala, aliwahi kusema kwamba anatamani siku moja akirudiana na mrembo huyo, awe meneja wake.

Read More
 HARMONIZE AWAJIBU WANAOMU-DISS KWA KUTOBOA PUA

HARMONIZE AWAJIBU WANAOMU-DISS KWA KUTOBOA PUA

Staa wa Muziki wa Bongofleva Harmonize ameamua kuwajibu wanaomkosoa baada ya Kuonekana akiwa ametoboa pua na kuweka kipini puani. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Harmonize amesema hafanyi hivyo kwa ajili ya kufanana na Wamarekani Weusi , Bali kuwakilisha Tamaduni za Kabila lake la Makonde. Hatua ya Harmonize kutoboa pua’ yake inakuja siku chache baada ya kuonekana akiwa amevalia sketi jambo liloteka mazungumzo mtandaoni. Wanamuziki wengine waliowahi kutoboa pua na kuvaa kipini nchini Tanzania ni pamoja na Diamond, Damian Sol na Chidi Beenz.

Read More
 HARMONIZE KUMUACHIA KAJALA MAJUKUMU YOTE YA KIBIASHARA KWENYE MUZIKI WAKE

HARMONIZE KUMUACHIA KAJALA MAJUKUMU YOTE YA KIBIASHARA KWENYE MUZIKI WAKE

Staa wa muziki wa Bongofleva, Harmonize anaendelea kuweka wazi matamanio yake ya kumfanya aliyekuwa mpenzi wake Kajala Frida kuwa Meneja wake akiamini kuwa kufanya hivyo kutaongeza kitu kwenye uongozi wake kutokana na akili yake. Kupitia ukurasa wake wa Instagram harmonize amesema kwamba ifikapo mwezi Juni mwaka huu ataacha kujihusisha na majukumu ya biashara ya muziki na kumwachia mpenzi wake, Kajala. Lakini pia Kajala atashirikiana na mameneja wengine waliopo nyuma yake. Harmonize amekazia kurekodi muziki na kutumbuiza Jukwaani ndio majukumu yake kwa sasa, kisha mpenzi wake Kajala Frida atadondoa wino kwenye dili za Kibiashara.

Read More
 ALBUM YA HARMONIZE “AFRO EAST” YAFIKISHA STREAMS MILLIONI 15 AUDIOMACK

ALBUM YA HARMONIZE “AFRO EAST” YAFIKISHA STREAMS MILLIONI 15 AUDIOMACK

Album ya msanii Harmonize,  “Afro East” imefikisha jumla ya Streams millioni 15 kwenye mtandao wa Audiomack. Album hiyo ya kwanza kwa mtu mzima Harmonize iliachiwa rasmi Machi 14, mwaka 2020 ikiwa na jumla ya ngoma 17 za moto. Aidha, Boss huyo wa Konde Gang mapema mwezi huu alitangaza kuachia album yake mpya na ya tatu mwezi Juni. Ikumbukwe album yake ya pili ambayo ni “High School” ilitoka Novemba 5, mwaka 2021. Huu unakuwa ni muendelezo wa Harmonize  kuachia ngoma mfululizo bila kupoa huku namba zikiendelea kuwa nzuri pia kupitia akaunti zake za digital platforms.

Read More
 HARMONIZE ATANGAZA JINA LA BRAND YAKE YA SIGARA

HARMONIZE ATANGAZA JINA LA BRAND YAKE YA SIGARA

Msanii nyota wa Bongofleva Harmonize ametangaza rasmi bidhaa yake ya Sigara iitwayo “Tembo Cigarette”. Kupitia Instagram yake Harmonize ameomba wadau kuwekeza pesa lakini pia washirika wa Kibiashara wajitokeze kwa ajili ya kuisukuma biashara hiyo. Ikumbukwe boss huyo wa Konde Gang tarehe 5 mwezi huu kupitia insta story yake aliweka wazi kwa mara ya kwanza kuwa amepata wazo la kuanzisha chapa (brand) yake mwenyewe ya Sigara na yuko tayari kuwekeza katika biashara hiyo.

Read More
 HARMONIZE ATOA UFAFANUZI KUHUSU TAMASHA LA AFRO EAST CARNIVAL

HARMONIZE ATOA UFAFANUZI KUHUSU TAMASHA LA AFRO EAST CARNIVAL

Staa wa Muziki nchini Tanzania Harmonize ametoa ufafanuzi kuhusu Tamasha la Afro East Carnival msimu wa pili. Kupitia Ukurasa wake wa Instagram harmonize amesema Tamasha hilo linalotarajiwa Kufanyika Mei 29,mwaka 2022 katika Uwanja wa Uhuru,jijini Dar es salaam hakutokuwa na Wasanii waalikwa kama ilivyokuwa kwenye Tamasha la kwanza alilotangaza List ya Wasanii waliomsindikiza. Harmonize amebainisha kuwa hii ni show yake na wanaopaswa kuhudhuria ni mashabiki wake tu. “Hii ni show ya Konde Boy wanaopaswa kuhudhuria ni Kondegang F.C tu.”  ameandika Harmonize kupitia Instagram. Lakini pia staa huyo Amesema katika Tamasha hilo atatumia Masaa 4 jukwaani na atatumbuiza nyimbo 60 huku akisema kutakuwa na Suprise nyingi ambazo hazitotangazwa

Read More
 HARMONIZE AANIKA RASMI JINA LA ALBUM YAKE MPYA

HARMONIZE AANIKA RASMI JINA LA ALBUM YAKE MPYA

Staa wa Muziki wa Bongofleva Harmonize Ametangaza jina Rasmi la Album yake ambayo itaingia sokoni mwezi ujao. Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Harmonize ameipa album hiyo jina la “Smoker Vision na ameweka wazi album hiyo itatoka mwezi Juni mwaka huu wa 2022 Boss huyo wa Konde Gang ambaye jana aliweka wazi kuja na brand yake ya Sigara, hii inaenda kuwa album yake ya tatu baada ya “Afro East iliyotoka mwaka 2020 na “High School” iliyotoka mwaka 2021.

Read More
 HARMONIZE MBIONI KUJA NA BRAND YAKE YA SIGARA

HARMONIZE MBIONI KUJA NA BRAND YAKE YA SIGARA

Staa wa muziki kutoka nchini Tanzania Harmonize anataka kukibadilisha Kikohozi chake kuwa biashara. Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Harmonize ametangaza kuja na bidhaa yake ya Sigara ambapo amewaomba mashabiki zake kumpa Jina zuri na kumsaidia kubuni muundo wa Sigara hizo. Boi huyo wa Konde Gang Worldwide ametambua kuwa kwa hatua aliyofikia, si muziki wake pekee unaouza, bali ni jina lake ndilo lenye thamani zaidi ya kitu chochote kwa sasa. Kwa mtaji wa jina lake na wafuasi wake, anaweza kutengeneza fedha kubwa zaidi.

Read More
 HARMONIZE KUPOKEA GARI ALILOMNUNULIA EX WAKE IJUMAA HII

HARMONIZE KUPOKEA GARI ALILOMNUNULIA EX WAKE IJUMAA HII

Staa wa muziki kutoka nchini Tanzania Harmonize ameweka wazi kuwa siku ya Ijumaa atapokea gari jipya kutoka nchini Afrika Kusini aina ya Range Rover yenye rangi nyeusi kwa ajili ya aliyekuwa mpenzi wake Kajala Frida Staa huyo amelithibitisha hilo kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram  kwa kuweka video ikionesha gari la kwanza aina (Range Rover) nyeupe alilotuonesha siku za nyuma na kusema amemnunulia mrembo huyo kama njia moja wapo ya kuendelea kumuomba msamaha. Aidha amewatupia vijembe wakosoaji wake ambao wamekuwa wakimshutumu kwamba hana fedha za kutosha kununua magari ya kifahari kwa kusema kwamba anatumia suala hilo kutafuta kiki ili aendelee kuzungumzwa kwenye tasnia ya muziki Afrika Mashariki. Hata hivyo Harmonize ameahidi kuleta gari lingine lenye rangi nyeusi na atafanya ex-wake Frida Kajala kuwa na gari aina ya Range Rover mbili.

Read More
 HARMONIZE AWEKA WAZI TAREHE YA KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

HARMONIZE AWEKA WAZI TAREHE YA KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

Staa wa Muziki wa Bongofleva Harmonize Hataki kupoa kwenye harakati za kuupeleka muziki wake kimataifa hii ni baada ya kumetangaza Tarehe atakayoachia Album yake Mpya. Kupitia InstaStory yake kwenye mtandao wa Instagram Harmonize Ametangaza kuwa Ataachia Album yake Mpya Mei 20 Mwaka huu. Mapema mwezi Februari mwaka huu harmonize  alitangaza ujio wa High school Deluxe Album version, mara baada ya album yake ya high school  kufanya vizuri mtandaoni. Mfumo huo wa deluxe version’ hufanywa na msanii katika album husika kwa kuongeza baadhi ya remix, au nyimbo mpya.

Read More