HARMONIZE NA ERIC OMONDI WAMALIZA TOFAUTI ZAO

HARMONIZE NA ERIC OMONDI WAMALIZA TOFAUTI ZAO

Wasanii Harmonize  na Eric Omondi hatimaye wamemaliza tofauti zao kwa kusameheana kufuatia matukio yaliyojiri Jumapili Mei mosi, 2022. Baada ya uvumi wa ugomvi wake na Harmonize, Eric Omondi ameomba radhi kutokana na kisa hicho ambacho kinadaiwa kuwafanya yeye na nyota huyo kutoka Tanzania kukaa karibu siku nzima katika kituo cha polisi cha Kileleshwa jijini nairobi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Eric Omondi ameweka wazi kuwa walisuluhisha changamoto iliyopelekea kukosekana kwa maelewano kati yao. “Kama kaka mkubwa, kama mshereheshaji na kama msanii mwenzangu wa Afrika Mashariki nataka kuomba radhi kwa yote yaliyotokea,” Eric alisema. Kwa upande wa Harmonize alisema hakuna aliyekamilika na kuongeza kuwa anachukulia kilichotokea kama sehemu ya changamoto za kazi na si vinginevyo huku akikanusha kumshambulia Eric Omondi kwa ngumi. “Bado mimi na kaka yangu tunampenda na kumheshimu hakuna mtu mkamilifu katika dunia hii, mimi niko poa kutoka moyoni mwangu. Kilichotokea ni changamoto za kazi tu na katika ulimwengu huu huwezi kuwa na furaha siku zote sisi ni ndugu,” Harmonize amesema katika instastory yake Instagram. Ikumbukwe Harmonize alikamatwa wikiendi hii iliyopita na kushikiliwa katika kituo cha Polisi cha Kileleshwa kwa madai ya kukiuka makubaliano ya kutokea kwenye club kadhaa za jijini Nairobi baada ya malipo kutolewa. Inasemekana Eric Omondi ndiye alipokea malipo hayo kwa niaba ya Harmonize.

Read More
 HARMONIZE AZIDI KULILIA PENZI LA KAJALA, AMNUNULIA GARI AINA RANGE ROVER EVOQUE

HARMONIZE AZIDI KULILIA PENZI LA KAJALA, AMNUNULIA GARI AINA RANGE ROVER EVOQUE

Staa wa muziki wa Bongofleva Harmonize bado anaendelea kulilia penzi la mpenzi wake wa zamani Fridah Kajala mtandaoni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ametangaza kumnunulia gari aina ya Range Rover Evoque yenye jina lake “Kajala 1” kwenye Number Plate. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mdomo” amechapisha sehemu ya video ikionesha gari hilo na kuandika maneno ya kuomba msamaha. Konde ameitumia njia hiyo katika mchakato wake wa kuendelea kuomba msamaha kwa mrembo huyo huku akisema gari hiyo ni ya ndoto yake. “Hatakama Zingekuwa KAJALA 1. mpaka 10. Haziwezi Kufuta Maumivu Niliyo Kusababishia wewe Pamoja Na Familia Haziwezi Badili Chochote Tulichopitia Nawala Haiwezi Kuwa Sababu Ya Kunirudia ila Hiii (1) Inaeleza Majuto Ya Yote Niliyo Kufanyia ..!!!! Ninacho omba Kwako ni Msamaha wa thati Ya Moyo Wako ..!!!! FRIDA wewe ni Mtu Wa Mungu Sanaa…!!!” Ameandika Harmonize. Ameendelea kwa kusema “Unasali Pia Bila shaka Unatambua Hakuna Mkamilifu Hutokuja Kuanza Upya Mama You Know me Better COME BACK Usisahau Mimi ni Mtoto wa Masikini Mwenzio Tuu Nina Familia Wajomba Shangazi Wadogo Na Ndugu Kibao Masikini Ambao Nikifa Leo Ndio Watakao Nizika Ila Nimeona Wewe Ndo Unastahili HICHI Kidogo Changu 🙏” “Natamani Ujue Kwamba Nakupenda Sana Narudia Tena Nisamehe Na Unipatie Nafasi Ya Mwisho I LOVE YOU TAKE ME BACK Nakumbuka Kuna Siku Ulisha Wahi Niambia Hii Ni MOJA YA GARI YA NDOTO YAKO PLEASE TAKE IT FROM ME I LOVE YOU ❤❤🌹🌹🥲🥲 THANKS MY BROTHER @royazdad Samahani Kwa Usumbufu 🙏🙏🙏 @ceekvr”

Read More
 HARMONIZE APATA VIEWS MILLIONI 1.3 NDANI YA SEKUNDE 21 YOUTUBE

HARMONIZE APATA VIEWS MILLIONI 1.3 NDANI YA SEKUNDE 21 YOUTUBE

Staa wa muziki wa Bongo Fleva Harmonize amevunja rekodi ya Video iliyotazamwa zaidi ndani ya muda mfupi iliyowekwa na kundi la wasanii kutoka South Korean ‘BTS’. Hii ni baada ya Video ya wimbo mpya wa Harmonize na Ibraah, Mdomo imeipata views milioni 1 YouTube ndani ya sekude 21 tu!. Hivi karibuni video ya Ibraah, Rara iliweza kupata views zaidi laki 6 ndani ya dakika tatu lakini ikachukua siku nne kufikisha views milioni 1 YouTube. Ikumbukwe Mei mwaka 2021, bendi kutoka Korea Kusini, BTS ilivunja rekodi mara baada ya video ya wimbo wao, Butter kufikisha views milioni 108.2 ndani ya saa 24 na kuivunjilia mbali rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Black Pink toka Korea ambao video yao, How You Like That’ M/V ya mwaka 2020 ilipata views milioni 86.3 ndani ya saa 24.

Read More
 HARMONIZE ATANGAZA ZIARA YA “HIGH SCHOOL” BARANI ULAYA

HARMONIZE ATANGAZA ZIARA YA “HIGH SCHOOL” BARANI ULAYA

Msanii wa Bongofleva, Harmonize ametangaza tour barani Ulaya kwa ajili ya albamu yake ya pili, High School. Bosi huyo wa lebo ya muziki ya Konde Music Worldwide amethibitisha ujio wa ziara hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amesema itaanza Julai 2 hadi Agosti 6 mwaka huu. Harmonize ambaye anafanya vizuri na ngoma yake “Bakhresa” atapita kwenye mataifa kama Ufaransa, Ujerumani, Hungary, Denmark, Sweden na Finland. Ujio wa tour hiyo yenye show tisa inakuja wiki chache tangu Harmonize aitangaze ziara yake ya Afrika Mashariki ya “Afro East Carnival” ambayo itaanza baada ya kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa waumini wa dini ya Kiislamu.

Read More
 HARMONIZE AWATOLEA UVIVU WAANDAAJI WA TAMASHA LA AFRIKA MOJA KISA PICHA YA ERIC OMONDI

HARMONIZE AWATOLEA UVIVU WAANDAAJI WA TAMASHA LA AFRIKA MOJA KISA PICHA YA ERIC OMONDI

Mkali wa muziki wa Bongofleva Harmonize ameonesha wazi kutofurahishwa na poster ya tamasha la Afrika Moja linalotarajiwa kufanyika nchini, Aprili 30 mwaka huu. Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Boss huyo wa Konde Gang ameeleza kwamba kitendo walichokifanya waandaaji wa tamasha hilo sio cha kiungwana kufuatia picha yake kuonekana kubwa huku picha ya mchekeshaji nyota nchini Eric Omondi ikiwa ndogo. Harmonize ameeleza kuwa Omondi ni mkubwa kwake kiumri na kisanaa pia, huku akidai kuwa picha hiyo imewekwa kama Omondi anakuja kufanya usafi tu katika uwanja wa KICC ambapo tamasha hilo litafanyika. Hata hivyo amewataka waandaaji wa tamasha hilo watengeneze poster nyingine ili aweze kupost kwenye uso wa ukurasa wake wa Instagram.

Read More
 HARMONIZE ATAMBA NA TUZO ZA TANZANIA MUSIC AWARDS, ADAI HATAKI TUZO ZA KIMATAIFA

HARMONIZE ATAMBA NA TUZO ZA TANZANIA MUSIC AWARDS, ADAI HATAKI TUZO ZA KIMATAIFA

Mwanamuziki wa Bongofleva Harmonize bado anaendelea kuzitukuza Tuzo zake Tatu ambazo alishinda kwenye tuzo za Tanzania Music Awards mwaka huu. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Harmonize amesema haitaji Tuzo za nje kama Grammy, BET na zote za Kimataifa kama hatofanikiwa kushinda za Tanzania kwani kizuri huanzia nyumbani. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Outside” anaonekana ana mipango mikubwa na Tuzo za Tanzania kwani amewasisitizia mashabiki zake kumuombea kichwa chake kikae sawa hadi mwakani utakapofanyika msimu mwingine. “It was a Dream..!!! Happy to See Tanzania Music Awards Back ..!!! 🙌 I don’t Need Grammy & BET & And All International Awards if I Don’t Wen This ..!!! START FROM HOME #TMA2021 TRIPPLE BEST 🏆🏆🏆 Niombeeni Tuu Kichwa Kikae Sawa Then Tukutane #TMA2022 🤞@amherman_ 🎬 PLEASE…!!!! PLEASE …!!!! PLEASE …!!! DO NOT SLIDE 🔞,” Ameandika Instagram.

Read More
 ALI KIBA NA HARMONIZE WANG’ARA KWENYE TUZO ZA TANZANIA MUSIC AWARDS 2021

ALI KIBA NA HARMONIZE WANG’ARA KWENYE TUZO ZA TANZANIA MUSIC AWARDS 2021

Tuzo za Tanzania Music Awards 2021 zimetolewa usiku wa kuamkia Aprili 3 huko Jijini Dares-Salaam, nchini Tanzania ambapo nyota wawili wa muziki wa BongoFleva, Ali Kiba na Harmonize wameibuka na ushindi kwenye vipengele vingi zaidi. C.E.O wa Kings Music, Ali kiba ameibuka mshindi na tuzo 5 za Tanzania Music Awards (TMA) kwenye vipengele vya Album bora (One Only King), video bora ya mwaka (Salute FT RudeBoy), mtunzi bora wa mwaka, Mwanamuziki bora wa Afrika Mashariki na Mwanamuziki Bora wa Kiume Chaguo la Watu mwaka 2021. Kwa upande wa Harmonize, yeye ameshinda tuzo 3 za Tanzania Music Awards kwenye vipengele vya Mtumbuizaji bora wa kiume, Msanii bora wa mwaka na Kolabo bora Afrika (Attitude ya Harmonize FT Awilo Longomba). Wasanii wengine walioshinda tuzo hizo ni pamoja na Nandy, Professa Jay, Darassa, Marioo, Diamond Platnumz, Young Lunya, Chemical, Saraphina, Baddest 47, Snura, Sholo Mwamba, Khadja Yusuph, Mzee Yusuph na wengine wengi.

Read More
 HARMONIZE AKANUSHA VIKALI KUTUMIA BANGO AKIWA EX WAKE FRIDA KAJALA KUTANGAZA VIDEO YA WIMBO

HARMONIZE AKANUSHA VIKALI KUTUMIA BANGO AKIWA EX WAKE FRIDA KAJALA KUTANGAZA VIDEO YA WIMBO

Mwanamuziki wa Bongofleva Harmonize  amekana na kukataa madai ya uwepo wa video ya wimbo wake uitwao Mtaje” ambao aliuimba mahususi kwa ajili ya aliyekuwa mpenzi wake Frida Kajala, kufuatia kusambaa kwa bango linalo onesha picha yake na mrembo huyo. Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa instagram Harmonize ameendelea kushare mfululizo wa post zinazo eleza kumkumbuka mpenzi wake huyo wa zamani huku akisisitiza kwamba hafanyi hivyo kwa ajili ya promotion ya wimbo wake wa Mtaje’. Mbali na hayo hitmaker huyo wa ngoma ya “Outside” amejitapa kuwa mwanamuziki alie sikilizwa zaidi Afrika Mashariki katika mtandao wa Spotify baada ya kufikisha jumla ya streams laki 8 katika mtandao huo huku akidai kwa sasa anaweza tabasamu kufuatia hilo.

Read More
 HARMONIZE KUACHIA DELUXE VERSION YA ALBUM YAKE YA HIGH SCHOOL

HARMONIZE KUACHIA DELUXE VERSION YA ALBUM YAKE YA HIGH SCHOOL

Mwanamuziki wa bongofleva Harmonize ametusanua huenda akaja na High school Deluxe Album version, mara baada ya album hiyo kufanya vizuri mtandaoni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Harmonize ametangaza rasmi kuachia ‘Deluxe edition’ ya album hiyo iliyotoka Novemba 5 mwaka Jana ikiwa na nyimbo 20. Aidha amesema mzigo huo utatoka baada ya video ya wimbo wa Bakhresa kufikisha VIEWS million 5 kwenye mtandao wa youtube. Mfumo huo wa deluxe version’ hufanywa na msanii katika album husika kwa kuongeza baadhi ya remix, au nyimbo mpya ambapo harmonize ametaja kuiongeza ngoma ya Bakhresa ambayo kwa sasa inafanya vizuri.

Read More
 HARMONIZE AWATOLEA UVIVU WANAOPINGA TUZO ZA MUZIKI TANZANIA

HARMONIZE AWATOLEA UVIVU WANAOPINGA TUZO ZA MUZIKI TANZANIA

Bosi wa lebo ya Konde Music Worldwide, Harmonize amesema atashiriki kwenye Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) licha ya kuwepo malalamiko kutoka kwa baadhi ya watu. Akizungumza kwenye One Love Concert Harmonize ameitaka serikali kutokatishwa tamaa na maneno ya watu kwani hata tuzo kubwa za nje zimekuwa zikilalamikiwa kwa sana. “Kama umeliona jina langu basi ujue nitashiriki kwa asilimia 100, kila mtu ana haki ya kusema kile anachojisikia kwa sababu hata tuzo nyingine ambazo tunaweza kusema ni bora kuliko tuzo za nyumbani zinalalamikiwa siku zote” amesema Harmonize. Utakumbuka tuzo za muziki nchini Tanzania zinarejea baada ya miaka saba tangu kusitishwa kwa Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) mwaka 2015.

Read More
 HARMONIZE ADAI MASHINDANO YA  BONGO STAR SEARCH YALIMSHAWISHI KUFANYA MUZIKI

HARMONIZE ADAI MASHINDANO YA BONGO STAR SEARCH YALIMSHAWISHI KUFANYA MUZIKI

Staa wa Muziki wa Bongofleva Harmonize Anasema kwamba Mashindano ya Bongo Star Search ndio yalimshawishi kuingia katika uimbaji. Kupitia Instagram yake Harmonize ameandika mengi huku akimpa sifa Nyingi muanzilishi wa Mashindano hayo ya BSS madam rita na kusema kuwa amekuwa ni chanzo cha vijana wengi kuzifikia ndoto zao. Kauli ya Harmonize imekuja baada ya kumpa heshima ‘Madam Rita’ mbele ya mashabiki kwenye tamasha la burudani la Serengeti Music Festival Februari 13 kwa kumpigia magoti kama njia moja wapo ya kutoa shukran zake kwa kumsaidia kujenga kipaji chake. Ikumbukwe kuwa boss huyo wa Konde Gang ni miongoni mwa wanamuziki waliowahi kushiriki Bongo Star Search (BSS) miaka mingi nyuma na kukosolewa vikali kwa uimbaji wake kwa kuambiwa hajui kuimba.

Read More
 HARMONIZE AFUNGUKA SABABU KUBWA YA KUMUIMBIA BAKHRESA

HARMONIZE AFUNGUKA SABABU KUBWA YA KUMUIMBIA BAKHRESA

Staa wa muziki wa Bongofleva Harmonize kwa mara ya kwanza ametoa ufafanuzi juu wa wimbo wake mpya wa Bakhresa’ ambao umezua gumzo mtandaoni. Kupitia ujumbe mrefu aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram Harmonize amesema sababu kubwa iliyompelekea kuimba wimbo huo ni kutoa hamasa kwa watu wasio na kipato kizuri katika jamii kupata nguvu ya kutafuta zaidi kwenye shughuli zao. “MY MUSIC 🎶 IS MORE ABOUT LIFE & PEOPLE Binafsi Nitafarijika Zaidi Kuona Watu Wakibadirisha Mwenendo Wa Maisha Kupitia Wimbo Huu ..!!!! Nitafarijika Sana Kumuona Kijana Mwenzangu Yeyote Mtaani Mwenye Kipato Kidogo Akiutumia Huu Wimbo Kama WEK UP CALL Na Kumtazama BAKHRESA Kama Mfano Wa Wazi …!!! Na Kuanza Zikimbilia Ndoto Kubwa Zaidi Nitafarijika Kuona Hakuna Kudharauliana Tunaishi Kwa Heshima Na Usawa Bila Kujali Hapa INTAGRAM Una Followers Wangapi ..!!! Maisha Ya BAKHRESA Ni Mfano Bora Wakuigwa Ingawa Sio Lazima Kila Tajiri Aishi Kama Anavyoishi BAKHRESA ..!!!” ameandika Harmonize kupitia ukurasa wake wa Instagram Hitmaker huyo wa ngoma ya “Outside” ameendelea kwa kusema “Nimalize Kwakusema MZEE BAKHRESA KUSIKIA WIMBO HUU Haitokuwa Ni Jambo La Ajabu Kwake Kwasababu Niliyo Ya Sema Yote ANAYAFANYA mafanikio Niliyo Yataja Yote Anayo Na Bila Shaka Haya Ni Machache tuu …!!! Kama Angetaka Kuimbwa Basi Angemlipa Hata (DRAKE) Maaana Uwezo Huwo Bila Shaka Anao Binafsi Sina Haja Kabisa Ya Mzee BAKHRESA kuusikia Wimbo Huu Maaana Ningetaka Hivyo Basi Ningefanya Utaratibu Wa Kuitafuta Familia Yake Ndugu Jamaa Na Marafiki ILI WIMBO UMFIKIE ASIKILIZE KAMA LENGO LILIKUWA NI KUMSIFIA ..!!!” Harmonize amemalizia kwa kusema “KIFUPI SINA URAFIKI AU UKARIBU WOWOTE NA NDUGU WA MZEE (BAKHRESA) LENGO LANGU KUBWA …!!! HUU WIMBO UKUFIKIE WEWE MASKINI MWENZANGU ULIENYANYASIKA NA MASKINI WENZAKO AMBAO WANAKUZIDI KIPATO KIDOGO TUUU UPATE NGUVU 💪🏼 NA UAMKE TENA ..!!! 💪🏼💪🏼 WIMBO HUU UKUFIKIE WEWE MWENYE NDOTO NDOGO UACHANE NAYO UTAFUTE KUBWA ZAIDII ….!!!! MWISHO WE THANK GOD FOR THE LIFE OF BIG BOSS (BAKHRESA ) PIA WALE MNAOSEMA NIMEFANYA TANGAZO LA BURE …!!! NI WAKATI WAKUWAKUMBUSHA MATAJIRI WENGINE WAYAFANYE MEMA YA KUMPENDEZA MUNGU & BINADAMU ILI WAPATE MATANGAZO YA BURE KAMA HAYA …..!!!! PERIOD NO ONE LIKE BAKHRESA Link in bio” Kauli ya mtu mzima Harmonize imekuja mara baada ya walimwengu kwwnye mitandao ya kijamii kumbeza kuwa ameishusha Brand au chapa yake ya muziki kwa kuachia wimbo wa bure kutangaza biashara na kampuni zinazomilikiwa na tajiri huyo ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Azam ya nchini Tanzania.

Read More