HARMONIZE KUFUNGULIWA MASHTAKA KWA MADAI YA KUMTUMIA VIBAYA MTOTO WAKE

HARMONIZE KUFUNGULIWA MASHTAKA KWA MADAI YA KUMTUMIA VIBAYA MTOTO WAKE

Mwanamuziki na CEO wa Konde Gang Harmonize amejipta pabaya mara baada ya kukosolewa vikali na wadau mbalimbali wanaosimamia haki za watoto nchini Tanzania kufuatia kitendo chake cha kupanda stejini usiku na mtoto wake wa kike katika tamasha lake la Afro East Carnival lililofanyika wekeend hii iliyopita jijini Dar es salaam. Kituo kimoja cha redio nchini Tanzania kimethibitisha kuwa msanii huyo kwa sasa anasakwa na mamlaka za Ustawi wa Jamii, kufuatia kitendo chake hicho cha kuambatana na kumpandisha mtoto mdogo katika tamasha lililofanyika usiku.

Read More
 HARMONIZE KUACHIA WIMBO MPYA SIKU MOJA BAADA YA EP YA DIAMOND PLATINUMZ KUTOKA

HARMONIZE KUACHIA WIMBO MPYA SIKU MOJA BAADA YA EP YA DIAMOND PLATINUMZ KUTOKA

Baada ya Diamond Platnumz kusogeza mbele kuachia Extended Playlist yake ya FOA Machi 11 ,mwanamuziki wa Bongofleva Harmonize nae amesogeza mbele zoezi la kuachia wimbo wake mpya ambao utatoka machi 12. Awali Diamond alitaja kuachia EP yake machi siku moja kabla ya tamasha la Afro East Carnival ambapo Harmonize nae alijibu mapigo kwa kutangaza kuachia wimbo mpya siku hiyo. Hata hivyo ushindani huo haikuishia hapo kwani licha ya diamond platnumz kusogeza mbele tarehe ya kuachia EP yake mwanamuziki Harmonize pia amesogeza mbele tarehe ya kutoa wimbo wake mpya alioupa jina la ‘Bakhresa’ na sasa utatoka machi 12, siku moja baada ya kutoka kwa FOA The EP ya mtu mzima Diamond Platnumz .

Read More
 HARMONIZE ABADILI RATIBA YA TAMASHA LAKE LA AFRO EAST CARNIVAL

HARMONIZE ABADILI RATIBA YA TAMASHA LAKE LA AFRO EAST CARNIVAL

Staa wa Muziki Nchini Tanzania Harmonize ametangaza mabadiliko ya Ratiba ya Kufanyika kwa tamasha lake la Afro East Carnival kutoka siku tatu hadi siku mbili. Kupitia ukurasa wa Instagram harmonize_amesema kwa sababu ambazo zipo  nje ya uwezo wake sasa tamasha hilo litaanza Siku ya ijumaa na kumalizika Jumamosi wiki hii,nhaa sio Alhamisi kama ilivyotangazwa mwanzo. “Tulitamani Sana ….!!!! Kuimba Nanyi Siku (3) Ila Kutokana Na Sababu Zilizo Nje Ya Uwezo Wetu Tumeridhiaa Kuipisha Siku Ya Alhamisi..Kuacha Shughuli Zaki Elimu Ziendele…. SO YESS LETS GO FRIDAY & SARTUDAY afro east carnival TABATA SHULE”. Ukumbukwe tamasha la Afro East Carnival’ litafanyika Jijini Dar Es Salaam machi 4 mwaka huu. Kwa mujibu Harmonize, tamasha hilo litawakutanisha kwenye steji moja nyota wakubwa kwenye kiwanda cha muziki Afrika Mashariki.

Read More
 WIMBO WA HARMONIZE “MWAKA WANGU” WACHEZWA KANISANI KWENYE IBADA

WIMBO WA HARMONIZE “MWAKA WANGU” WACHEZWA KANISANI KWENYE IBADA

Mwanamuziki wa Bongofleva Harmonize anaendelea kuchukua headlines mbalimbali mara baada ya wimbo wake wa Mwaka Wangu kutajwa na kuchezwa katika ibada kwenye moja ya kanisa mkoani Arusha inayoongozwa na Mchungaji Geor Davie. Mtumishi huyo ambaye anajulikana kama Nabii Geor Davie , ameuelezea wimbo huo kama wimbo mzuri usio na maneno mabaya , na kumtamkia Harmonize maneno ya baraka na kumshahuri kuokoka kabla ya kurusu wimbo huo kupigwa na kuchezwa katikati ya ibada siku ya juma pili Februari 21. Hata hivyo Harmonize ameonekana kukoshwa na hatua ya wimbo wake wa mwaka wangu kuchezwa kanisani ambapo ameahidi kutembelea kanisa hilo hivi karibuni. Ikumbukwe kuwa Harmonize pia ametoa wimbo wa injili uitwao ‘Omoyo Remix’ alioimba na mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za injili Jane Misso ndani ya mwezi huu..

Read More
 HARMONIZE AWEKA WAZI KUHUSU MAPATO YA WIMBO WA “OMOYO REMIX” WA JANE MISSO

HARMONIZE AWEKA WAZI KUHUSU MAPATO YA WIMBO WA “OMOYO REMIX” WA JANE MISSO

Staa wa muziki wa Bongofleva Harmonize ameweka wazi masuala ya umiliki wa wimbo wa “Omoyo Remix”. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Harmonize ambapo amesema hana umiliki wowote kwenye wimbo huo na mapato yote yanakwenda kwa Mchungaji Jane Misso. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Outside” amesema licha ya kutumia gharama zake kwenye Audio na Video, hatachukua hata asilimia 1 kwenye wimbo huo. Hata hivyo amesema lengo ni kumuona Jane Misso akiwa amerejesha furaha yake na kung’aa kwa baraka za Mungu

Read More
 HARMONIZE AFUNGUKA SABABU ZA KUWAONDOA DARASSA NA JUMA JUX KWENYE TAMASHA LA AFRO EAST CARNIVAL

HARMONIZE AFUNGUKA SABABU ZA KUWAONDOA DARASSA NA JUMA JUX KWENYE TAMASHA LA AFRO EAST CARNIVAL

Staa wa muziki wa Bongo fleva Harmonize amefunguka sababu za kuwaondoa Juma jux na Darassa katika orodha ya wasanii watakao kuwepo kwenye Tamasha la AFRO EAST CARNIVAL ambalo litafanyika machi 5 mwaka huu. Kwenye mkao na Waandishi wa habari nchini Tanzania, Harmonize Anasema hayo yalitokea kutokana na Kutokuwa na mawasiliano mazuri baina ya Uongozi wake na uongozi wa Mastaa hao, huku akisema kuwa hakuna ugomvi wowote kati yake na Msanii juma jux pamoja Darassa, Hivyo watu wasikuze vitu. Sanjari na hilo Harmonize ametoa ofa ya watu 1000 wa kwanza kununua Tiketi za kuudhuria katika Tamasha la AFRO EAST CARNIVAL ambapo tiketi zitaanza kuuzwa rasmi siku ya tarehe 15, hivyo watapata tiketi kwa Shilingi elfu 5 za Kitanzania. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Outside” amesisitiza kuwa idadi ya wasanii watakao kuwepo kwenye Tamasha la AFRO EAST CARNIVAL bado itaendelea kutangazwa ikizingatiwa kuwa mpaka sasa ni wasanii 43 ambao wameshatangazwa kumsindikiza harmonize kwenye tamasha lake.

Read More
 H. BABA AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA KUMU-UNFOLLOW HARMONIZE NA KUMFUATA DIAMOND PLATINUMZ INSTAGRAM

H. BABA AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA KUMU-UNFOLLOW HARMONIZE NA KUMFUATA DIAMOND PLATINUMZ INSTAGRAM

Mwanamuziki wa Bongofleva, H. Baba kwa sasa anam-follow Diamond Platnumz pekee kwenye ukurasa wake wa Instagram ambao una followers zaidi ya laki 6. Juzi kati H. Baba alimpongeza Diamond kwa kutumbuiza kwenye show maalumu iliyoandaliwa na waandaaji wa tuzo za Grammy, Recording Academy iitawayo Global Spin ambayo ina lengo la kuuibua na kuutangaza zaidi muziki wa Afro Beat, Pop na Latin Music. Hatua hiyo iliwashangaza wengi kwani kwa miaka ya hivi karibuni H. Baba alikuwa karibu sana na Harmonize hadi kushirikiana kwenye wimbo, uitwao Attitude ambao Awilo Longomba kutoka DRC Congo naye alishirikishwa. Kwa inavyoonekana sasa uhusiano kati ya H. Baba na Harmonoze umeingia na ukungu baada ya kuamua kumu-unfollow Instagram na kum-follow Diamond pamoja na kuupigia debe muziki wake.

Read More
 HARMONIZE AONDOA MAJINA YA WASANII JUX NA DARASSA KWENYE BANGO LA TAMASHA LAKE  “AFRO EAST CARNIVAL”

HARMONIZE AONDOA MAJINA YA WASANII JUX NA DARASSA KWENYE BANGO LA TAMASHA LAKE “AFRO EAST CARNIVAL”

Staa wa muziki wa Bongofleva Harmonize ameyaondoa majina ya wasanii Jux na Darassa kwenye bango lenye orodha ya wasanii ambao wametajwa kutumbuiza kwenye tamasha la Afro East Carnival. Kwenye bango jipya ambalo Hitmaker huyo wa “Outside” ameliweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, majina ya wakali hao yameondolewa kufuatia malalamiko yao kwamba hawakuwa na taarifa yoyote au makubaliano na menejimenti ya Harmonize. Tamasha la Afro East Carnival’ litafanyika Jijini Dar Es Salaam Machi 5, mwaka wa 2022 na litawakutanisha kwenye steji moja nyota wakubwa kwenye kiwanda cha muziki Afrika Mashariki. Hii si mara ya kwanza kwa Harmonize kupanga kufanyika kwa tamasha kubwa la muziki nchini tanzania, August 4 mwaka wa 2020 aliitambulisha rasmi Harmo night Carnival ambayo ilipangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huo kwa siku tatu mfululizo. Hata hivyo tamasha hilo halikufanyika kwa sababu ambazo hadi leo hazijawekwa wazi.

Read More
 HARMONIZE ATANGAZA KUACHIA WA WIMBO WA GOSPEL LEO

HARMONIZE ATANGAZA KUACHIA WA WIMBO WA GOSPEL LEO

CEO wa record label ya KondeGang Harmonize ametangaza rasmi ujio wa remix ya wimbo wa dini  uitwao “Omoyo” kutoka kwa mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Tanzania Jane Misso Hitmaker huyo wa ngoma ya “Outside” amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kumchana mwimbaji wa nyimbo za injili Goodluck Gozbert kwa tafsiri ya kutomzungumzia vizuri juu ya matamanio yake ya kufanya muziki huo wa injili. Mbali na hayo Harmonize ambaye ni muumini wa dini ya kiislam ameeleza kuwa yeye ni bado ni muumini wa dini ya kiislamu na ataendelea kuwa na upendo kwa watu wa dini zote bila kujali utofauti wa imani zao.  

Read More
 MWANAMUZIKI WA BONGOFLEVA HARMONIZE AWEKA REKODI BOOMPLAY TANZANIA

MWANAMUZIKI WA BONGOFLEVA HARMONIZE AWEKA REKODI BOOMPLAY TANZANIA

Nyota wa muziki nchini Tanzania na mmiliki wa record label ya Konde Gang Harmonize amefanikiwa kufikisha jumla ya streams million 50+ katika mtandao wa boom play music Tanzania. Kwa streams hizo Konde Boy anaungana na wanamuziki wengine wenye zaidi ya streams 50+ katika mtandao huo kama Diamond Platnumz ,Mbosso na Rayvanny ambaye ndiye kinara wa streams Afrika Mashariki. Mpaka sasa mkali huyo wa ngoma ya “Teacher’ ametoa Album mbili ambazo ni Afro East ya mwaka 2020 yenye streams million 2.7 na Highschool ya 2021 yenye streams million 19, na EP moja ‘ inayokwenda kwa jina la Afro Bongo.

Read More
 HARMONIZE ATANGAZA UJIO WA TAMASHA LA “AFRO EAST CARNIVAL”

HARMONIZE ATANGAZA UJIO WA TAMASHA LA “AFRO EAST CARNIVAL”

Mwanamuziki wa bongofleva Harmonize ameitangaza rasmi Machi 5, mwaka wa 2022 kuwa tarehe rasmi ambayo tamasha lake ‘Afro East Carnival’ litafanyika Jijini Dar Es Salaam. Kwa mujibu wake, tamasha hilo litawakutanisha kwenye steji moja nyota wakubwa kwenye kiwanda cha muziki Afrika Mashariki. Hii si mara ya kwanza kwa Harmonize kupanga kufanyika kwa tamasha kubwa la muziki nchini tanzania, August 4 mwaka wa 2020 aliitambulisha rasmi Harmo night Carnival ambayo ilipangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huo kwa siku tatu mfululizo. Hata hivyo tamasha hilo halikufanyika kwa sababu ambazo hadi leo hazijawekwa wazi.

Read More
 HARMONIZE AMTAKA ALI KIBA KUTUMBUIZA KATIKA SIKU YAKE YA UCHUMBA

HARMONIZE AMTAKA ALI KIBA KUTUMBUIZA KATIKA SIKU YAKE YA UCHUMBA

Mwanamuziki Maarufu nchini Tanzania, Harmonize ameonesha heshima kwa mwanamuziki mwenzake Alikiba kwa kumpongeza kwa kazi nzuri anayofanya kwenye tasnia ya Muziki wa Bongofleva. Kupitia ukurasa wake wa instagram, Harmonize alichapisha video fupi iliyokuwa ikicheza wimbo mpya wa Alikiba unaoitwa ‘Utu’ huku akiambatinisha na ujumbe kwamba siku ya kuvisha pete mpenzi wake lazima King Kiba atumbuize mashabiki wake. “Mtu amwambie mkongwe, mfalme Ali Kiba lazima aimbe kwenye usiku wa kumvisha pete mchumba wangu, huu muziki mzuri sana,” Harmonize aliandika. Utakumbuka juzi kati wanamuziki hao walionekana wakisafiri kwenye ndege pamoja jambo ambalo liliteka mazungumzo mtandaoni kwa muda

Read More