SAVARA ADAI HAAMINI KWENYE SUALA LA WANANDOA KUVISHANA PETE

SAVARA ADAI HAAMINI KWENYE SUALA LA WANANDOA KUVISHANA PETE

Msanii Savara ametoa ya moyoni kwa kusema kwamba haamini kwenye suala la wapenzi kuvishana pete wanapofunga ndoa. Msanii huyo wa Sauti Sol amehoji kuwa pete haina umuhimu wowote kwa wanandoa, hivyo haoni kama inaashiria uaminifu kwa kuwa ni pambo kama mapambo mengine. Kwenye mahojiano na podcast ya SPM Buzz Savara amesema kuna watu wamevishwa pete na wapenzi wao lakini mwisho wa siku wanafanya udanganyifu kwenye mahusiano yao. Hata hivyo amesisitiza kuwa penzi la kweli linatoka moyoni na wala sio kupitia pete, hivyo hatokuja kumvisha pete mchumba wake Yvonne Endo.

Read More
 BIEN WA SAUTI SOL ATAKA SERIKALI KUPUNGUZA BEI YA UNGA

BIEN WA SAUTI SOL ATAKA SERIKALI KUPUNGUZA BEI YA UNGA

Msanii anayeunda kundi la Sauti Sol, Bien Baraza amezua gumzo mtandaoni mara baada ya kusema kwamba hatawahi kuwa na amani hadi pale bei ya unga itakaposhuka. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram Bien amedai kwamba moja kati ya bidhaa ambayo anatamani ishuke bei ni unga wa sima huku akipendekeza iuzwe shillingi 99 za Kenya “You won’t see me smiling till the price of unga goes down to Ksh. 99 #Inauma”, Aliandika Hata hivyo wafuasi wake wameonekana kumfanyia mzaha kwenye uwanja wa comment ya posti yake kwa kusema kwamba itabidi azoee huku wengine wakihoji kuwa anashinikiza bei ya unga wa sima ishuke kwa kuwa anatokea katika jamii ya Waluhya ambayo imekuwa ikihusishwa sana na uraibu wa ugali.

Read More
 SAVARA AMCHANA ERIC OMONDI, AMTAKA AACHE KUINGILIA WANAMUZIKI

SAVARA AMCHANA ERIC OMONDI, AMTAKA AACHE KUINGILIA WANAMUZIKI

Msaniii wa Sauti Sol, Savara Mudigi amepinga kauli ya mchekeshaji Eric Omondi kuwa wasanii wakenya hawana ubunifu wa kutengeneza matukio yatakayowafanya wazungumziwe kwenye tasnia ya muziki nchini. Katika mahijiano yake hivi karibuni Savara amemtaka awache kujihusisha na masuala ya wanamuziki na badala yake awekeze muda wake kuboresha kazi yake ya ucheshi. Sanjari na hilo Savara ameweka wazi matamanio yake ya kuingia kwenye siasa kwa kusema kuwa amekuwa akishinikizwa na watu wake wa karibu awanie wadhfa wa kisiasa lakini muda sahihi wa kufanya hivyo haujafika. Utakumbuka Savara anafanya vizuri na album yake iitwayo Savage Level ambayo ina jumla ya nyimbo 14 ya moto

Read More
 BIEN WA SAUTI SOL AFUNGUKA KUHUSU UCHAGUZI MKUU NCHINI KENYA

BIEN WA SAUTI SOL AFUNGUKA KUHUSU UCHAGUZI MKUU NCHINI KENYA

Mwana kikundi wa Sauti Sol, Bien amefunguka namna uchaguzi nchini Kenya ulivyoendeshwa. Katika mahojiano na Mungai Eve, Bien amesema mchakato mzima wa uchaguzi mkuu nchini ulikuwa wa haki na huru ambapo amewapongeza wakenya kwa kudumisha Amani kabla na hata baada ya uchaguzi. Hitmaker huyo “Inauma” amewataka wakenya kurejea kazini baada ya Rais mteule William Ruto kutangazwa na Tume huru ya uchaguzi IEBC hata kama kuna wale ambao hawakuridhishwa na matokeoa ya urais. Bien ametoa wito kwa serikali mpya itakayoingia mamlakani kuboresha sanaa nchini Kenya ili vijana waweze kupata ajira. Kuhusu mgogoro wao na muungano wa kisiasa wa Azimio la Umoja kutumia wimbo wao wa “Extravangaza bila ridhaa ya Sauti Sol, Bien amesema mawakili wao wanashughulikia suala hilo kuhakikisha wanapata haki.

Read More
 BIEN AFUNGUKA KUHUSU SAUTI SOL KUTOTUMBUIZA KWENYE MAJUKWAA YA KISIASA.

BIEN AFUNGUKA KUHUSU SAUTI SOL KUTOTUMBUIZA KWENYE MAJUKWAA YA KISIASA.

Mwanakikundi wa Sauti Sol Bien amefunguka mara baada ya Diamond Platnumz kupewa nafasi ya kutumbuiza kwenye mkutano wa kisiasa wa mrengo wa Azimio la Umoja juzi kati. Kulingana na Hitmaker huyo “Inauma”,  sio wasanii wote wana haja ya kutumbuiza kwenye majukwaa ya kisiasa. “We don’t want to be in political forums” Amesema Bien. Bien ametoa kauli hiyo kufuatia hatua ya mchekeshaji Eric Omondi kuwatolea uvivu wasanii wa Kenya kwa kutotumbuiza kwenye hafla ya kisiasa ya Azimio la Umoja huko Kasarani.

Read More
 BIEN: SILALI CHUMBA KIMOJA NA MKE WANGU

BIEN: SILALI CHUMBA KIMOJA NA MKE WANGU

Msanii wa kundi la Sauti Sol Bien kwa mara nyingine tena ameibuka na kauli yenye utata kuhusu maisha yake na mkewe Mtangazaji Chikki. Akipiga stori na Mambo Mseto ya Radio Citizen Bien amesema licha ya mkewe kuwa Meneja wake, wanaposafiri kwa ajili ya show kila mmoja hulala chumba chake. “Katika ndoa yetu kuna mipaka pia, kwa mfano kama nimeitwa mahali niko na shoo, nakaa kwa chumba cha hoteli mimi peke yangu. Huwa sitaki hata muziki hapo ndani. Nataka tu kukaa peke yangu nijisikilize na kujitathmini kuhusu jinsi nitakavyoifanya hiyo shoo” alisema. “Kwa hiyo kama unaniita kama ajenti ama promota, huwezi nitengea chumba kimoja mimi na mke wangu, sitaki kulala na yeye kitanda kimoja hiyo siku, nataka kuenda kujisikilizia,” alisema Bien. Hittmaker huyo wa ngoma ya “Inauma” amefafanua kwamba wakienda kwa shoo na mke wake mambo ya uchumba yanabaki nyumbani na kule wanaenda kama msanii na Meneja wake na kwa hiyo kuna umuhimu wa kila mmoja kutengewa chumba chake binafsi mbali na mwingine.

Read More
 BIEN AWAPA SOMO VIJANA WALIO CHINI YA UMRI WA MIAKA 30

BIEN AWAPA SOMO VIJANA WALIO CHINI YA UMRI WA MIAKA 30

Mwimbaji mkuu wa Kundi la Sauti Sol nchini Kenya Bien amesema hashauri watu waliopo katika umri wa miaka ya ishirini kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwani ni kupotezeana muda. Bien amesema watu walio katika umri huo wanapaswa kujijali wenyewe na kusafiri kwa kuwa mtu aliyeko katika umri huo bado anajitafuta ajue kitu gani hasa anakihitaji. “Siwezi kumpa ushauri mtu mwenye umri wa miaka ishirini awe kwenye mahusiano, ni kupoteza muda, angalau fanya kazi, usafiri pia uwe na watu wengine huku na huko.” alisema Bien. Aidha aliongeza kwamba mtu akiwa katika umri huo hajitambui na mtu aliye naye pia hajitambui “Unadhani unafanya nini? Mnajaribu kusuluhisha mambo pamoja lakini mwisho wa siku yaani nadhani ni bora kuwa peke yako ikiwa uko katika miaka ya 20” alimaliza Mwanamuziki huyo.

Read More
 SAUTI SOL WASITISHA MKATABA NA UNIVERSAL MUSIC GROUP

SAUTI SOL WASITISHA MKATABA NA UNIVERSAL MUSIC GROUP

Kundi la Sauti Sol limeweka wazi kuwa limesitisha mkataba wao na kampuni ya Universal Music Group. Kwenye mahaojiano aliofanya mjini Nairobi Msanii wakundi hilo Bein amesema kuwa waliamua kutosaini mkataba mwingine na kampuni hiyo. Bein amesema kuwa lengo la msanii kujulikana zaidi na kufika kimataifa ni swala ambalo haliko kwa mtu anayesamabaza mziki wake bali ni kwa msanii mwenye . Aidha amefichua kwa sasa wametayarisha Album mpya ambayo itasambazwa na kampuni tofauti. Utakumbuka Sauti Sol na Universal Music Group walisaini mkataba mwaka wa 2020.

Read More
 BIEN WA SAUTI SOL AFUNGUKA KUHUSU KUPANGA UZAZI

BIEN WA SAUTI SOL AFUNGUKA KUHUSU KUPANGA UZAZI

Msanii kutoka kundi la Sauti Sol Bein Aim Baraza amesema kuwa yupo tayari kukata mshipa wa uzazi maarufu vascectomy punde atakapo pata watoto na mke wake Chiki Kuruka. Akizungumza kwenye kipindi cha Baldmen Session kwenye mtandao wa youtube Bein amesema kuwa kupanga uzazi barani Afrika ni swala ambalo limewachiwa wanawake. Bien amesema kuwa hawezi kumwachia mke wake mzigo huo pekee licha ya kuwa wanaume wengi wanaogopa kufanyiwa vasectomy. “Wanaume wengi hawako tayari kufanyiwa vasektomi lakini mimi niko tayari kuangalia vasektomi, nimechoka kuweka mzigo huu kwa vifaranga wetu, kwanza najua dawa mbalimbali za uzazi wa mpango zina madhara tofauti. “Amesema Bien kwenye kipindi anachoandaa. Lakini pia amefunguka kuwa mashabiki wamekuwa wakimshinikiza kupata mtoto na mke wake Chiki Kuruka licha ya kuwa kwenye ndoa kwa miezi 18 pekee. “Hata mimi Wakenya wameniangalia weird, I’ve stayed karibu for 18 months na sijafanya kitu lakini kila kitu na time yake,” alisema. “Sijawahi kuwa na hamu ya kuzaliana! Kwa hiyo haijawahi kunisumbua sana.” amesema

Read More
 SAUTI SOL WAAHIRISHA ZIARA YAO YA MUZIKI BARANI ULAYA

SAUTI SOL WAAHIRISHA ZIARA YAO YA MUZIKI BARANI ULAYA

Wasanii wa Kundi la Sauti Sol wametangaza kusitisha ziara yao ya muziki iliyopaswa kuanza rasmi mwezi huu wa Juni huko barani Ulaya. Kupitia taarifa waliyochapisha kwenye mitandao ya kijamii wasanii wa kundi hilo kwa masikitiko makubwa wamesema wamelazimika kupiga chini show hiyo kwa sababu ya changamoto ya kupata visa. Sauti Sol Wamesema licha ya kutuma maombi ya kupata visa kwa ubalozi wa uingereza umewaambia wameshindwa kuwapatia visa kwa wakati kutokana mzozo unaoshuhudiwa kati ukraine na urusi. Hata hivyo wamewaomba radhi  mashabiki wao wote ambao kwa njia moja au nyingine wameathirika na uamuzi wao huo huku wakiahidi kufanya mazungumzo na mapromota wa muziki nchini uingereza kutoa tarehe nyingine ya kufanyika kwa ziara yao ya muziki.

Read More
 SAUTI SOL WALAMBA SHAVU LA KUFANYA KAZI NA NDOVU TECH

SAUTI SOL WALAMBA SHAVU LA KUFANYA KAZI NA NDOVU TECH

Kundi la muziki nchini Sauti Sol wameingia ubia wa kufanya kazi na jukwaa la uwekezaji linakuja kwa kasi barani kwa jina la Ndovu tech. Sauti sol wamethibitisha taarifa hiyo njema kwa mashabiki kupitia ukurasa wao wa Instagram kwa kusema kwamba ushirikiano wao na jukwaa hilo litawapa fursa ya kuhamasisha watu kuhusu umihimu wa kuzingatia matumizi sahihi ya fedha kwenye masuala ya uwekezaji. Hitmaker hao wa ngoma ya “Suzzana” wamesema dili hilo itatoa nafasi pia  kwa mashabiki zao kufikia uhuru wao wa kifedha kwa kuwekeza kwa vitu vitakavyowaingizia kipato. Hata hivyo Ndovu Tech ambayo ni jukwaa la uwekezaji   linalotoa nafasi kwa watu kupata huduma za kifedha sokoni imewakaribisha sauti sol katika familia yao.

Read More
 MAWAKILI WA RAILA ODINGA NA SAUTI SOL WAKUTANA.

MAWAKILI WA RAILA ODINGA NA SAUTI SOL WAKUTANA.

Mawakili wa Kinara wa ODM Raila Odinga na wale wa kundi la muziki la Sauti Sol wamekutana kwa ajili ya mazungumzo ili kutatua mgogoro wa hakimiliki ulioibuka mapema wiki hii baada ya wimbo wa Sauti Sol “Extravaganza” kupigwa kwenye mkutano wa Azimio. Wakili wa kundi la Sauti Sol, Moriasi Omambia ndiye amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter. “Ningependa kuthibitisha kwamba kundi linaloongoza kampeni za Raila Odinga na mawakili wao wanashirikiana nasi katika juhudi za kutatua mzozo uliopo kuhusu hakimiliki. Tunatambua kujitolea kwao katika kutafuta kusuluhisha jambo hili haraka iwezekanavyo.”  imesomeka tweet hiyo ya Omambia. Utakumbuka Chama cha ODM cha Raila Odinga kilitoa taarifa hapo awali kikisema kwamba walitumia muziki wa Sauti Sol kwa sababu wanapenda kazi za kundi hilo.

Read More