Ringtone afunguka sababu za kuwaponda Willy Paul na Bahati

Ringtone afunguka sababu za kuwaponda Willy Paul na Bahati

Hitmaker wa Ombi Langu, Ringtone Apoko amefunguka sababu ya kuwakosoa wasanii Willy Paul na Bahati kila mara kwenye majukwaa mbali mbali. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema wawili hao walimvunjia heshima mwenyezi Mungu kwa kutumia vibaya kiwanda cha muziki wa injili kwa ajili ya kujilimbikizia mali na kisha wakageukia muziki wa kidunia. Msanii huyo ameenda mbali zaidi na kusema kuwa kitendo cha Willy Paul na Bahati kutumia njia haramu kuchuma mali wanayomiliki kwa sasa imewaponza kisanaa kiasi cha kutopata mafanikio kwenye muziki wao. Katika hatua nyingine Ringtone ametetea utajiri wake kwa kusema kuwa ana vyanzo vingi halali vinavyomuinguzia kipato huku akikanusha tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya ulanguzi wa pesa kwani inakwenda kinyume na maandiko matakatifu.

Read More
 Willy Paul alamba dili nono ya kufanya kazi na Kampuni ya Oppo

Willy Paul alamba dili nono ya kufanya kazi na Kampuni ya Oppo

Staa wa muziki nchini Willy Paul ametangaza kuingia ubia wa kufanya kazi na kampuni ya simu za mkononi ya OPPO. Willy Paul ameshare habari hiyo njema kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Instagram akieleza kwamba ana furaha kujiunga na familia ya Oppo. “Super excited to announce my partnership with the brand new OPPOReno8 series! We can’t wait to share this exciting new model with you guys!”. Ameandika. Kwa mafanikio hayo Hitmaker huyo wa “Lalala” atatakiwa kutangaza na kuwashawishi wafuasi wake wazinunue simu mpya aina ya OPPO Reno 8 series kupitia mitandao yake ya kijamii.

Read More
 Penzi la Willy Paul lampa Jovial umaarufu mtandaoni

Penzi la Willy Paul lampa Jovial umaarufu mtandaoni

Msanii nyota nchini Jovial amekiri kupata mashabiki wengi wanaofuatilia kazi zake tangu atangaze kuingia kwenye mahusiano na Willy Paul. Kupitia insta story mrembo huyo ameshindwa kuficha furaha yake kwa kusema kwa kipindi chote cha maisha ya muziki hajawahi pata idadi kubwa ya watu wanaotazama nyimbo zake pamoja na kutembelea mitandao yake ya kijamii licha ya kushirikiana na wasanii mbali mbali kwenye suala la kuachia nyimbo kali. Katika hatua nyingine Mrembo huyo amesema ameshangazwa namna watu wanavyomshambulia  na Willy Paul kwa kujihusisha na kiki mtandaoni ilhali hawaungi mkono kazi za wasanii wachanga wanaotoa muziki mzuri bila kutengeneza matukio. Hata hivyo amemaliza kwa kuachia Wakenya swali kama wanaunga mkono muziki mzuri au umbea ambapo mashabiki wengi wameonekana kusisitiza umuhimu wa wasanii kutoa muziki mzuri sambamba na kutengeneza matukio yatakayowafanya wazungumziwe mtandaoni kama njia ya kujitangaza kimuziki.

Read More
 Willy Paul afikisha subscribers milioni 1 Youtube

Willy Paul afikisha subscribers milioni 1 Youtube

Nyota wa muziki nchini Willy Paul amefanikiwa kufikisha idadi ya subscribers million moja kwenye mtandao wa Youtube Channel ya youtube ya Willy Paul ilifunguliwa rasmi Mei 21 mwaka 2010 na mpaka sasa imefikisha zaidi ya watazamaji millioni 193,063,998. Willy Paul sasa anajiunga na wanamuziki wenzake Otile Brown na Bahati ambao wana zaidi ya wafuatiliaji (subscribers) Milioni 1 kwenye mtandao Youtube nchini Kenya. Bosi huyo wa Saldido amepata mafanikio hayo mara baada ya video ya wimbo wake “Lalala” aliyomshirikisha Jovial kuondolewa kwenye mtandao wa Youtube kwa madai ya hakimiliki.

Read More
 Mwanaume wa makamu atishia kujitoa uhai kisa kuibiwa mpenzi na Willy Paul

Mwanaume wa makamu atishia kujitoa uhai kisa kuibiwa mpenzi na Willy Paul

Baada ya msala wa video ya wimbo wa “Lalala” kufutwa Youtube kwa madai ya hakimiliki na kisha kurejeshwa, sasa ni zamu ya mwanaume mmoja ambaye amejitokeza na kutishia kujitoa uhai kutokana na hatua ya Willy Paul kumnyang’anya mpenzi wake Jovial. Kwa mujibu wa video inayosambaa mtandaoni, mwanaume huyo anadai Jovial ni mpenzi wake wa muda mrefu ambapo ameenda mbali zaidi na kusisitiza kuwa wamebarikiwa kupata mtoto wa pamoja. Kauli ya mwanaume huyo imeibua hisia mseto miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ambapo wengi wameonekana kuzipuzilia mbali tetesi hizo wakidai ni kiki huku wengine wakiwa wamebaki na mashangao kwa kitendo cha mwanaume huyo kuangua kilio hadharani kisa mapenzi. Hata hivyo Willy Paul amepuzilia mbali tuhuma hizo kwa kusema kwamba  hazina ukweli wowote.

Read More
 Vdeo ya wimbo wa Willy Paul “Lalala” yafutwa Youtube

Vdeo ya wimbo wa Willy Paul “Lalala” yafutwa Youtube

Video ya wimbo wa Willy Paul ‘Lalala ambao amemshirikisha Jovial imeondolewa kwenye mtandao wa YouTube kutokana na malalamiko ya hakimiliki. Kwa sasa video hiyo ambayo ilikuwa na zaidi ya view laki 3 haipatikani kwenye mtandao huo kufuatia malalamiko ya hakimiliki kutoka kwa King Jones Official. Hata hivyo Willy Paul hajatoa tamko lolote kuhusu kufutwa kwa video ya wimbo wa mambo yote youtube. Ikumbukwe mtandao wa Youtube hauruhusu kutumia kazi au kionjo cha mtu mwengine bila makubaliano.

Read More
 ERIC OMONDI AKOSHWA NA MATUKIO YA WILLY PAUL NA JOVIAL, ATAKA WASANII WAFUATE NYAYO ZAO

ERIC OMONDI AKOSHWA NA MATUKIO YA WILLY PAUL NA JOVIAL, ATAKA WASANII WAFUATE NYAYO ZAO

Mchekeshaji kutoka Kenya Eric Omondi amekoshwa na kile kinachoendelea mtandaoni kati ya msanii Willy Paul na Jovial. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Omondi amewapongeza wawili hao kwa hatua ya kuhalalisha mahusiano mtandaoni kitendo ambacho amehoji ni ubunifu wa hali ya juu wa kutengeneza matukio yatakayowasaidia kutangaza muziki wao mtandaoni. Mchekeshaji huyo ambaye kwa muda mrefu amekuwa akipigana kwa udi na uvumba kutetea muziki wa Kenya, amesema kuwa kwa sasa ni vigumu kwa msanii kupata mafanikio makubwa pasi na kuwa na matukio yatakao mfanya awe gumzo kwa mashabiki zake. Hata hivyo amewapa changamoto wasanii kuwa wabunifu ili kutengeneza maudhui ya burudani yatakayo jenga gumzo kwa mashabiki wao na kupitia njia hiyo wataweza kushinda na wasanii wa kimataifa.

Read More
 WILLY PAUL AFUNGUKA SABABU ZA KUTOACHIA WIMBO WAKE NA GUCHI

WILLY PAUL AFUNGUKA SABABU ZA KUTOACHIA WIMBO WAKE NA GUCHI

Staa wa muziki nchini Willy Paul amefunguka sababu za kutoachia wimbo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki kati yake na msanii wa Nigeria Guchi. Kwenye mahojiano na Mungai Eve Willy Paul amesema video ya ngoma hiyo ilivuja mtandaoni, kitendo ambacho kilimkasirisha na kuamua kufutilia mbali mchakato wa kuachia wimbo huo. Lakini pia ameweka wazi chanzo cha kufuta video ya wimbo wake wa “Moyo” kwenye mtandao wa Youtube kwa kusema kuwa video ya wimbo huo haikuwa na ubora aliouhitaji, hivyo aliogopa itamshushia chapa au brand yake ya muziki. Willy paul ambaye amegonga vichwa vya habari kwa wiki moja sasa baada ya kuwekeza kwenye sekta ya matatu, anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao Kesho.

Read More
 CEO WA BONFIRE ADVENTURE AKIRI KUWA MMLIKI WA MATATU ILIYONUNULIWA NA WILLY PAUL

CEO WA BONFIRE ADVENTURE AKIRI KUWA MMLIKI WA MATATU ILIYONUNULIWA NA WILLY PAUL

Sakata la Willy Paul kudaiwa kununua matatu ambayo imetumika imechukua mkondo mpya baada ya bosi wa Bonfire Adventures Simon Kabu kukiri hadharini yeye ndio mmiliki halisi wa matatu hiyo. Kupitia posti ya msanii Willy Paul kwenye mtandao wa Instagram Kabu ameandika ujumbe wa kumpongeza msanii huyo kwa hatua ya kuwekeza kwenye biashara ya matatu ambapo ameenda mbali zaidi na kujinadi kuwa kabla ya Willy Paul kununua matatu hiyo yeye ndio alikuwa anamiliki. Ujumbe huo umezua hisia mseto mitandaoni ambapo baaadhi ya wakenya wameonekana kumkosoa Kabu kwa madai ya kumvunjia heshima Willy Paul huku wengine wakiendelea kumponda msanii huyo wakihoji kuwa walikuwa na fahamu kuwa matatu hiyo ishatumika.

Read More
 MASTERPIECE AMCHANA KIMTINDO WILLY PAUL KISA KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA MATATU

MASTERPIECE AMCHANA KIMTINDO WILLY PAUL KISA KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA MATATU

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Master Piece ameamua kufufua bifu yake na Bosi wa Saldido baada ya kuonekana kuponda hatua ya Willy Paul kuwekeza kwenye sekta ya matatu. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Masterpiece ameandika “Naskia kuna mtu amenunua mat ya ronga”, ujumbe ambao umetafsiriwa ni vijembe kwa Willy Paul ambaye juzi kati alitangaza kununua matatu. Sasa posti yake hiyo imeonekana kuwakera watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao wamemshushia kila aina matusi masterpiece wakidai kuwa muziki umemshinda ndio maana amegeukia maisha ya kulelewa na mwanamke anayemzidi kiumri. Hata hivyo wameenda mbali na kumtaka msanii huyo afurahie mafanikio ya wasanii wengine badala ya kudharau shughuli zao ambazo zinawaingizia kipato. Ikumbukwe Masterpiece na Willy Paul hajakuwa na maelewano mazuri kwa muda sasa, mwaka wa 2020 walirushiana maneno makali kwenye mitandao ya kijamii kisa uvaaji wa mavazi.

Read More
 WILLY PAUL AKIRI KUUMIZWA NA TUHUMA ZA KUMDHALILISHA MISS P KINGONO

WILLY PAUL AKIRI KUUMIZWA NA TUHUMA ZA KUMDHALILISHA MISS P KINGONO

Msanii nyota nchini Willy Paul ameendelea kutoa ushuhuda wa ndani kuhusu maisha yake,amefunguka kwamba alipitia kipindi kigumu mara baada ya kutuhumiwa kumnyanyasa kingono aliyekuwa msanii wake Miss P. Kwenye mahojiano na Munga Eve, Hitmaker huyo wa “Tamu Walahi” amedai kuwa tuhuma hizo ziliathiri afya yake ya akili kiasi cha kupatwa na msongo wa mawazo huku akiri kuwa tangu kipindi hicho hajawahi kurejea katika hali yake ya kawaida kwani amekuwa akiishi kwa hofu. Katika hatua nyingine amesema hatokuja kumsaini msanii yeyote kwenye lebo ya Saldido kwa kuwa wasanii aliowasajili kipindi cha nyuma walimshushia tuhuma za uongo ambazo karibu zimuharibie chapa yake ya muziki. Utakumbuka mwishoni mwa mwaka jana kipindi Miss P anaondoka kwenye lebo ya Saldido alimtuhumu Willy Paul kumdhulumu kijinsia kiasi cha kumlazimisha kutoka nae kimapenzi bila kutumia kinga.

Read More
 WILLY PAUL AWEKEZA KWENYE SEKTA YA MATATU

WILLY PAUL AWEKEZA KWENYE SEKTA YA MATATU

Nyota wa muziki nchini Willy Paul ameamua kuwekeza kwenye biashara ya uchukuzi maarufu matatu kama njia ya kutanua kitega uchumi chake. Akizungumza na wandishi wa habari, Willy Paul amesema kuwekeza kwenye sekta ya matatu ni moja kati ya ndoto ambazo amekuwa akitamani kufanikisha katika maisha. Hitmaker huyo wa toto ambaye kwa sasa amejikita zaidi kwenye masuala ya ujasirimali, amesema licha ya watu kumponda mtandaoni kuwa anapenda maisha ya starehe na anasa, amefarijika sana kutengeneza nafasi ya ajira kwa vijana wenzake kupitia uwekezaji wake huo. Licha ya mashabiki kumpongeza kwa mafanikio hayo, kuna baadhi ya walimwengu walimrushia vijembe mtandaoni wakidai kuwa Willy Paul ameishusha chapa yake (brand) kwa hatua ya kununua gari ambalo limetumika. “How does such a big brand in Kenya buys used car for business?” Shabiki ameandika kwenye posti ya Willy Paul Instagram. Tayari Willy Paul amenunua magari manne aina ya matatu na amezindua gari moja liitwalo Saldido Van ambayo itajihusisha na masuala ya kusafirisha watu kwenye shughuli zao za kibinafsi.

Read More