WILLY PAUL AWAJIA JUU WALIOTAKA KIMSHUSHA KIMUZIKI
Staa wa muziki nchini Willy Paul amerusha jiwe gizani kwa madalali waliotaka kumshusha kimuziki miaka ya hapo nyuma. Kupitia instagram yake Pozze amejitapa kuwa huu ndio muda wake wa kuwaaminisha wote waliomdharau kipindi hicho kuwa ana uwezo wa kuupeleka muziki wake kimataifa bila usaidizi wa mtu yeyote. Haikuishia hapo Hitmaker huyo wa “Toto” ameenda mbali zaidi na kutusanua kuwa kuna kipindi walimkatisha tamaa kuwa hatoweza kufanya project yeyote na ikafanikiwa kwa sababu hakuwa na mawazo ya kugeuza muziki wake kuwa biashara. “Walisema hatujiwezi, walisema hatuna akili ya bizz…lakini tables just turned.. watalilia kwa choo gui!!”, Aliandika kwa machungu. Utakumbuka kabla ya Willy Paul kugeukia muziki wa kidunia miaka kadhaa iliyopita, alikumbwa na kashfa nyingi kwenye kiwanda cha muziki wa injili nchini Kenya, kashfa alizozitaja kuwa zilitengenezwa na baadhi ya wadau wa muziki waliotaka kumshusha kimuziki.
Read More