Entertainment

Msanii Kings Music Mutima Akataa Kushiriki Mapenzi kwa Miaka 5

Msanii Kings Music Mutima Akataa Kushiriki Mapenzi kwa Miaka 5

Msanii mpya wa lebo ya Kings Music mwenye asili ya Rwanda, Mutima, amesema hataki kabisa kusikia masuala ya mapenzi katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Akizungumza katika kipindi cha Friday Night Live, Mutima amesema licha ya kuwa single, ameamua kuelekeza nguvu na muda wake wote katika muziki wake. Amefafanua kuwa mapenzi yanaweza kuvuruga umakini na kumchelewesha kufikia malengo aliyojiwekea.

Mrembo huyo, ameongeza kuwa anaamini mafanikio ya kweli yanahitaji umakini na kujitoa kikamilifu, jambo linalomfanya kwa sasa kuyaweka mapenzi kando ili kuhakikisha anatimiza ndoto zake za kimuzi.

Mutima ambaye anafanya poa single yake mpya “King’ang’anizi”, yupo chini ya Kings Music, lebo inayomilikiwa na Ali Kiba kwa mkataba wa miaka mitano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *