Msanii wa Bongofleva kutoka Next Level Music (NLM), Rayvanny amekuwa msanii wa kwanza kutokea Afrika kuwahi kutumbuiza kwenye tuzo za MTV Europe Music Awards (MTV EMA) 2021.
Hafla ya tuzo hizo ambazo zimefanyika usiku wa kuamkia leo Novemba 15, 2021 nchini Hungary katika ukumbi wa Budapest Spotarena, Rayvanny alipanda jukwaani na staa wa Colombia aliyemshirikisha kwenye wimbo Mama Tetema, Maluma.
Maluma na Ray Vanny wametumbuiza ngoma hiyo kwa mara ya kwanza usiku wa kuamkia leo, na sasa tayari ngoma hiyo inapatikana kupitia majukwaa mbalimbali ya ku-stream muziki mtandaoni.