Gossip

Dem wa Facebook Amkataa Hadharani Oga Obinna Wakati wa Mahojiano

Dem wa Facebook Amkataa Hadharani Oga Obinna Wakati wa Mahojiano

Msanii wa vichekesho kutoka Kenya, Dem wa Facebook, ameendelea kugonga vichwa vya habari baada ya kutoa kauli tata kumhusu Oga Obinna wakati wa mahojiano aliyofanya na mtangazaji mmoja.

Katika mahojiano hayo, mtangazaji alimuuliza kuhusu uhusiano wake na Obinna, lakini Dem wa Facebook alikatiza mjadala huo na kukataa kabisa kujibu maswali yoyote yanayomhusu.

Mrembo huyo, ameonyesha wazi kwamba hataki mambo yanayomhusu Obinna yawe sehemu ya mazungumzo yake, akiongeza kuwa hataki kubebeshwa mambo yanayohusiana naye.

Msimamo huo umeongeza mvutano uliokuwepo kati yake na Oga Obinna tangu aondoke Obinna TV, ambapo walikuwa wakifanya kipindi kimoja cha burudani.

Ingawa wawili hao hawajawahi kufichua hadharani chanzo cha tofauti zao, walimwengu wanadai kuwa huenda mahusiano ya kimapenzi yalisababisha umoja wao kazini kushindikana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *