LifeStyle

Wahu Kagwi Azua Mjadala Kuhusu Mahari, Asema Hatadai Kwa Ndoa za Mabinti Zake

Wahu Kagwi Azua Mjadala Kuhusu Mahari, Asema Hatadai Kwa Ndoa za Mabinti Zake

Msanii mkongwe kutoka Kenya, Wahu Kagwi, amepuzilia mbali utamaduni unaowashinikiza wanaume kuwaliipia wake zao mahari pindi wanapoingia kwenye taasisi ya ndoa.

Wahu amesema kuwa wazo la wanaume kulipa mahari kwa wazazi kama fidia ya kumlea mtoto wa kike halimpendezi na halikai sawa na mtazamo wake kuhusu ndoa na thamani ya mwanamke.

Kwa mujibu wake, kumlea mtoto ni jukumu la mzazi na si jambo linalopaswa kulipwa au kufidiwa wakati wa ndoa. Wahu amethibitisha kuwa hatadai mahari siku itakapofika kwa mabinti zake kuolewa. Ameeleza kuwa anataka ndoa ya watoto wake ijengwe kwa upendo na heshima badala ya kuzingatia masharti ya kifedha.

Hata hivyo, Wahu amesisitiza kuwa heshima kwa tamaduni ya kiafrika ni muhimu, lakini pia ni vyema jamii kujitathmini na kujiuliza kama baadhi ya mila zinaendana na nyakati za sasa na misingi ya ndoa yenye furaha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *