Sports news

Starlets Kukabiliana na Benin na Ivory Coast Katika Mechi za Kirafiki Abidjan

Starlets Kukabiliana na Benin na Ivory Coast Katika Mechi za Kirafiki Abidjan

Timu ya Harambee Starlets imepangiwa kucheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa nchini Ivory Coast kabla ya kuelekea Ufaransa kwa kambi ya mazoezi kuendelea na maandalizi yao ya kushiriki katika Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake WAFCON mwaka huu.

Timu hiyo inatarajiwa kuondoka Jumamosi kwenda Abidjan, ambapo itachuana na Benin tarehe 2 mweziujao na wenyeji Ivory Coast siku mbili baadaye katika uwanja wa Stade Olympique Alassane Ouattara d’Ebimpé. Mechi hizo zitawapa makocha wa timu hiyo fursa ya kuboresha mbinu zao na kutathmini utayari wa kikosi hicho dhidi ya wapinzani wenye ushindani mkubwa.

Fainali za kombe la WAFCON zitaanza tarehe 17 mwezi Machi na kukamilika tarehe 3 Aprili. Kenya itafungua kampeni yao ya Kundi A dhidi ya wenyeji Morocco mnamo tarehe 17 mwezi ujao, kisha itamenyana na Senegal siku tatu baadaye. Timu hiyo itahitimisha mechi za makundi dhidi ya Algeria tarehe 23 mwezi ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *