Msanii wa Sauti Sol, Bien-Aimé Baraza, amefunguka baada ya shinikizo kutoka kwa baadhi ya wadau wa muziki waliohoji kwa nini wasanii wa Kenya hawakuandaa wimbo wa pamoja wa kumuomboleza hayati Raila Amolo Odinga.
Kupitia sehemu ya maoni kwenye video ya YY Comedian iliyoenea mitandaoni, Bien ameacha ujumbe uliovutia hisia mseto mtandaoni kwa kuandika, “Watu wengine labda Baba afufuke ndio niwork nao.”
Kauli hiyo imefafanuliwa na wengi kama ishara ya kuwepo kwa mgongano wa chini kwa chini kati yake na baadhi ya wasanii wa muziki nchini Kenya, ingawa wengine wameichukulia kama utani wa kawaida.
Mashabiki mitandaoni wamegawanyika, baadhi wakisema Bien alikuwa anatania tu, huku wengine wakihisi kwamba maneno yake yanaakisi hali halisi ya ukosefu wa umoja miongoni mwa wasanii wa Kenya.