Serikali Kenya Kushirikiana na Waandalizi wa Nairobi Marathon Kuboresha Utalii wa Michezo

Serikali Kenya Kushirikiana na Waandalizi wa Nairobi Marathon Kuboresha Utalii wa Michezo

Waziri wa Utalii, Bi. Rebecca Miano, amesema serikali iko tayari kushirikiana na waandalizi wa mbio za kila mwaka za Nairobi Standard Chartered Marathon ili kuboresha hadhi ya mashindano hayo na kuyatumia kama nyenzo ya kukuza utalii wa michezo nchini. Akizungumza leo katika Bustani ya Uhuru, Nairobi, wakati wa makala ya 22 ya mbio hizo, Miano ameeleza kuwa sekta ya utalii na michezo zina uhusiano wa karibu unaoweza kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa. Amesema serikali inapanga kuanzisha ushirikiano wa kimkakati na washikadau katika sekta ya michezo, utalii na masoko ya kimataifa, ili kuhakikisha Kenya inatambulika duniani kama kitovu cha utalii wa michezo. Waziri Miano pia amepongeza ufanisi wa waandalizi na washiriki, akibainisha kuwa takribani wanariadha 32,000 walijitokeza kushiriki katika mbio za mwaka huu idadi ambayo inaonyesha mvuto mkubwa wa mashindano hayo kitaifa na kimataifa. Hata hivyo, amesema wizara yake itaendelea kuunga mkono matukio kama haya yanayochangia ustawi wa michezo, utalii na uchumi wa nchi kwa ujumla

Read More
 Apple Kuongeza Chaguo la Transparency Katika Mfumo Mpya wa iPhone

Apple Kuongeza Chaguo la Transparency Katika Mfumo Mpya wa iPhone

Kampuni ya teknolojia ya Apple imetangaza kuwa itaanzisha chaguo jipya litakaloruhusu watumiaji kuchagua kiwango cha transparency katika muonekano wa mfumo mpya wa iPhone. Hatua hii inakuja baada ya kuzinduliwa kwa design mpya inayojulikana kama Liquid Glass, ambayo inachanganya mwonekano wa kioo na maji, ikitoa hisia ya kisasa zaidi katika muundo wa iOS. Hata hivyo, Apple imekiri kuwa baadhi ya watumiaji, hasa wenye changamoto za kuona, wamekuwa wakipata ugumu kutofautisha icons na buttons kutokana na kiwango kikubwa cha uwazi katika muonekano huo. Kupitia maboresho hayo, Apple imepanga kuweka sehemu maalum ya kuchagua kiwango cha uwazi (transparency level) kulingana na mapendeleo ya mtumiaji. Watumiaji wataweza kuchagua kati ya mitindo miwili ambazo ni Clear na Tinted. Chaguo la Clear litaonyesha mandhari ya nyuma ya icons kwa uwazi zaidi, huku Tinted likiongeza opacity na contrast ili kufanya icons na buttons ziweze kuonekana kwa urahisi zaidi, hasa kwa watu wenye matatizo ya kuona. Maboresho haya yanatarajiwa kujumuishwa katika toleo jipya la iOS litakalotolewa mwaka huu, hatua ambayo inalenga kuboresha matumizi na kupanua wigo wa upatikanaji kwa watumiaji wote.

Read More
 Nina Roz Apuuzilia Mbali Kauli ya Daddy Andre Kuhusu Kampeni Zake

Nina Roz Apuuzilia Mbali Kauli ya Daddy Andre Kuhusu Kampeni Zake

Msanii wa Uganda Nina Roz amepuzilia mbali kauli ya aliyekuwa mpenzi wake, Daddy Andre, aliyedai hatatoa msaada wowote katika kampeni zake za kisiasa iwapo hatalipwa. Kwenye mahojiano ya hivi karibuni, Nina Roz amesema kuwa Andre hana mchango wowote katika safari yake ya kisiasa na kwamba hahitaji msaada wake kwa njia yoyote. Msanii huyo ameonyesha kutopendezwa na kauli hiyo na kueleza kuwa hana muda wa kujibizana na mtu ambaye hana nafasi katika mipango yake. Ameongeza kuwa kuingia kwake katika siasa hakutamzuia kuendelea na kazi ya muziki, akibainisha kuwa ataendeleza vipaji vyake vyote viwili, kama alivyofanya Bobi Wine, ambaye pia alianza kama msanii kabla ya kuingia katika siasa. Wikiendi iliyopita, Daddy Andre alieleza kuwa anaendesha muziki kama biashara na hatokuwa tayari kutumbuiza au kumpigia debe Nina Roz katika kampeni zake za Wilaya ya Sembabule bila malipo, akisisitiza kuwa anafanya kazi kwa misingi ya kibiashara. Nina Roz, anayefahamika kwa wimbo wake maarufu “Billboard (Oliwa)”, aliteuliwa rasmi kuwa mgombea wa kiti cha Mbunge wa Wanawake wa Wilaya ya Sembabule katika uchaguzi mkuu ujao kupitia chama cha NUP chake Bobi Wine.

Read More
 Kelechi Africana Awataka DJs Waheshimu Kazi za Wasanii Kenya

Kelechi Africana Awataka DJs Waheshimu Kazi za Wasanii Kenya

Msanii wa muziki kutoka Pwani, Kelechi Africana, ameonyesha kutoridhishwa na tabia ya baadhi ya madj wanaodhibiti sauti za nyimbo wakati wasanii wanatoa burudani kwa mashabiki zao jukwaani. Kupitia ujumbe wake mitandaoni, Kelechi amesema madj wengi wamekuwa wakipunguza sauti ya playback mara tu msanii anapopanda jukwaani, hali inayowafanya mashabiki kupoteza hamasa. Ameeleza kuwa mara nyingi muziki huwa na sauti kubwa kabla msanii hajaanza kutumbuiza, lakini inapungua ghafla msanii anapoanza kuimba, kisha kurejea juu pindi msanii anaposhuka jukwaani. Kelechi amesema hali hiyo inawadhalilisha wasanii na kuathiri ubora wa maonesho, akisisitiza kuwa yeye na wasanii wengine hulipwa kufanya kazi yao kwa ubora, hivyo madj wanapaswa kuwa waangalifu na kuhakikisha usawa wa sauti wakati wote wa onyesho. Aidha, amehoji kama tatizo hilo linatokana na vifaa vya madj au makusudi, akiwataka kuwa na ushirikiano zaidi na wasanii ili kuinua kiwango cha maonesho ya muziki nchini Kenya.

Read More
 Bifu Kati ya VJ Patelo na Toxic Lyrikali Yapamba Moto Mtandaoni

Bifu Kati ya VJ Patelo na Toxic Lyrikali Yapamba Moto Mtandaoni

Vita vya maneno kati ya VJ Patelo na rapa Toxic Lyrikali vimechacha tena mtandaoni, safari hii vikihusisha majigambo ya fedha na vito vya thamani. Toxic Lyrikali ndiye alianza mashambulizi kupitia Instagram Live kwa kudai kuwa Patelo anaishi kwa kutegemea pesa za mke wake, Dee, jambo lililozua mjadala mkali kati ya mashabiki wao. Hata hivyo, Patelo hakusita kujibu. Kupitia mitandao ya kijamii, ameonyesha maisha yake ya kifahari na misururu ya minyororo ya thamani, huku akimkejeli Toxic kwa kusema kuwa minyororo yake ni “miyoo” (bandia). Mashabiki wa pande zote mbili wameendelea kutoa maoni tofauti, wengine wakimtetea Patelo kwa kudai anajitegemea, huku wengine wakisema Toxic Lyrikali alikuwa anasema ukweli kuhusu maisha ya VJ huyo. Vita hivyo vya maneno vinaonekana kuendelea, huku kila upande ukijaribu kuthibitisha nani ni “boss” halisi katika maisha ya kifahari.

Read More
 Octopizzo Azuru Nyumbani kwa Odinga Kutoa Pole kwa Familia

Octopizzo Azuru Nyumbani kwa Odinga Kutoa Pole kwa Familia

Msanii wa hip hop nchini Kenya, Octopizzo, amezuru nyumbani kwa familia ya hayati Baba Raila Odinga ili kutoa heshima zake za mwisho na kushiriki majonzi pamoja nao. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Octopizzo amechapisha picha akiwa na familia ya Odinga na kueleza kuwa ilikuwa fahari kubwa kwake kuonyesha heshima kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Raila Odinga. Ametoa shukrani zake za dhati kwa Raila Junior na Mama Ida Odinga kwa mapokezi ya kifamilia na ukarimu waliomuonyesha wakati wa ziara hiyo. Octopizzo pia ametuma salamu za rambirambi akiwatakia familia hiyo faraja, nguvu na neema katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, huku akihimiza umoja na upendo miongoni mwa Wakenya wakati wa msiba huo.

Read More
 Msanii Iyanii Afichua Kiasi cha Pesa Anachompa Mpenzi Wake Kila Mwezi

Msanii Iyanii Afichua Kiasi cha Pesa Anachompa Mpenzi Wake Kila Mwezi

Mwanamuziki Iyanii amefichua kuwa amekuwa akimpa mpenzi wake, anayejulikana kama Shes Kemunto, posho ya kila mwezi inayokadiriwa kuwa kati ya KSh150,000 hadi KSh200,000. Akizungumza kwenye mahojiano, Iyani alisema hatua hiyo ni sehemu ya kumtunza na kumthamini mpenzi wake kwa mchango wake katika maisha yake ya kila siku. Mkali huyo wa ngoma ya Donjo Maber, amesema kwamba anapenda kuhakikisha Kemunto anaishi kwa starehe bila kuwa na wasiwasi wa kifedha. Hata hivyo, Iyanii amesisitiza kuwa mapenzi sio maneno bali ni vitendo vinavyoonyesha kujali. Kauli hiyo imezua maoni mseto miongoni mwa mashabiki mitandaoni, wengine wakimsifu kwa ukarimu wake huku wengine wakidai ni matumizi ya kupindukia.

Read More
 Eric Omondi Aanza Harakati za Kumtafuta Jamaa Anayefanana Naye

Eric Omondi Aanza Harakati za Kumtafuta Jamaa Anayefanana Naye

Mchekeshaji na mwanaharakati, Eric Omondi, ameomba msaada wa kumtafuta kijana anayefanana naye, ambaye video yake imesambaa mtandaoni nchini Kenya. Kupitia kipande cha video alichopakia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Eric ameeleza kuwa anataka kumpata kijana huyo ili wawe wawili, akitania kwamba mmoja wao anaweza kushiriki kwenye maandamano huku mwingine akiendelea na kazi zake za kawaida. Kijana huyo ambaye anadaiwa kutoka Githurai, Kenya, alipata umaarufu ghafla baada ya video yake kusambaa ambapo alinukuliwa akisema kuwa anatamani kukutana na Eric Omondi. Wafuasi wengi mitandaoni wamekuwa wakimtag Eric kwenye video hiyo wakimtaka atimize ombi hilo. Hadi sasa Eric Omondi hajaweka wazi kama amepata mawasiliano ya kijana huyo, lakini mashabiki wanatarajia kuona mkutano wao, ambao wengi wanaamini utazua kicheko na kufunika mitandao

Read More
 Stevo Simple Boy Akanusha Kutoka Kimapenzi na Pritty Vishy

Stevo Simple Boy Akanusha Kutoka Kimapenzi na Pritty Vishy

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Stevo Simple Boy, amekanusha madai kwamba aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mrembo aitwaye Pritty Vishy, akieleza kuwa mahusiano yao yaliishia katika hatua ya mazungumzo (talking stage). Akizungumza kwenye podcast ya AM, Stevo amesema kuwa licha ya kuwa mwaminifu katika mapenzi, aligundua kuwa Pritty hakuwa na nia njema katika uhusiano huo, bali alikuwa na malengo yake binafsi. Stevo ambaye anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao Fanana, ameeleza kuwa baada ya kutengana, Pritty alianza kuzungumza mambo mabaya kumhusu, lakini yeye alichagua kubaki kimya ili kuepuka kuendeleza mizozo ya mtandaoni. Stevo ameongeza kuwa anamshukuru Mungu kwa kuhifadhi ubikra wake hadi alipompata mke anayempenda na kumjali kwa dhati. Msanii huyo pia amefichua kuwa wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza hivi karibuni, hatua anayosema ni baraka kubwa katika maisha yake.

Read More
 Amber Ray Asema Uhusiano Wake na Rapudo Ulivunjika kisa Chai

Amber Ray Asema Uhusiano Wake na Rapudo Ulivunjika kisa Chai

Sociliate kutoka Kenya, Amber Ray, ameibua gumzo mtandaoni baada ya kufunguka chanzo cha kuvunjika kwa uhusiano wake na mchumba wake, Kennedy Rapudo. Akizungumza kwenye mahojiano na Obinna TV, Amber amesema uhusiano wao uliingia doa baada ya Rapudo kumlazimisha kupika chai wakati yeye alikuwa na hangover kali. Amesema ingawa huwa mnyenyekevu kwa baba wa mtoto wake, alikasirishwa na kitendo hicho kwa sababu hapendi kufanya jambo lolote kwa kulazimishwa. Mama huyo wa mtoto mmoja, amesema baada ya kisa hicho, walikaa bila kuwasiliana kwa takriban mwezi mmoja kabla ya Rapudo kumtafuta ili kusuluhisha tofauti zao. Hata hivyo, amekiri kuwa hadi sasa wameachana mara tatu na kurudiana, akionyesha kuwa uhusiano wao umekuwa na changamoto kadhaa lakini pia maelewano.

Read More
 Akothee Aeleza Namna Magonjwa Yalivyobadilisha Maisha Yake

Akothee Aeleza Namna Magonjwa Yalivyobadilisha Maisha Yake

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya, Akothee, amefunguka kuhusu mabadiliko makubwa kwenye maisha yake baada ya kugunduliwa na matatizo ya kiafya yakiwemo mashambulizi makali ya kichwa (migraine), damu kuganda, na fibroids. Kupitia ujumbe mrefu kwenye ukurasa wake wa Instagram, Anasema hali hizo zimemlazimisha kupunguza kasi na kubadili mtazamo wake kuhusu maana ya nguvu na maisha. Akothee amesema changamoto hizo zimemfundisha kuwa nguvu ya kweli si kupambana kila wakati, bali ni kujipa nafasi ya kupumzika na kupona. Ameeleza kuwa sasa anaheshimu mwili wake zaidi, anaepuka presha zisizo za lazima, na kutilia mkazo amani na utulivu kama tiba yake kuu. Aidha, amewatia moyo wanawake wengine wanaopitia changamoto za kiafya kimyakimya, akisema hawapaswi kuona hali hizo kama udhaifu, bali kama safari ya mabadiliko na ukuaji.. Ameongeza kuwa sasa anaheshimu zaidi mwili wake na kuepuka presha zisizo za lazima. Kwa ucheshi wake wa kawaida, Akothee ametaniana na wafuasi wake akisema wanaweza kumuita “Fibroids, Migraines, Bloodclot Akoth Kokeyo,” huku akisisitiza kwamba upendo wa kweli ni ule unaoonyeshwa mtu akiwa hai, na kwamba huu ni wakati wake wa kuthamini utulivu.

Read More
 OpenAI Yazindua Browser Mpya Inayotumia Akili Bandia

OpenAI Yazindua Browser Mpya Inayotumia Akili Bandia

Kampuni ya OpenAI, inayojulikana kwa kutengeneza programu maarufu ya ChatGPT, imezindua browser mpya ya kisasa inayoitwa Atlas, ambayo inatarajiwa kushindana na Google Chrome na browsers zingine kubwa duniani. Atlas ni browser inayotumia akili bandia (AI) kufanya kazi mbalimbali za mtandaoni kwa ufanisi na kwa kasi zaidi. Tofauti na browsers za kawaida, Atlas inaweza kusoma kurasa za wavuti, kufupisha habari, kusaidia kuandika maudhui, na hata kutoa uchambuzi wa taarifa ulizofungua mtandaoni. Kipengele cha kipekee zaidi cha Atlas ni kwamba imeunganishwa moja kwa moja na ChatGPT, jambo linaloiwezesha kutoa msaada wa papo kwa papo kwa watumiaji. Kwa mfano, mtumiaji anaweza kuomba browser imsaidie kujibu maoni kwenye mitandao ya kijamii, kuelewa maana ya ukurasa fulani, au kupata muhtasari wa taarifa ndefu bila kutoka kwenye ukurasa husika. Ujio wa Atlas unachukuliwa kama hatua kubwa katika mageuzi ya teknolojia ya AI, kwani unaleta mchanganyiko kamili kati ya ufahamu wa lugha asilia na uzoefu wa kutumia mtandao. Wataalamu wa teknolojia wanasema Atlas inaweza kubadilisha namna watu wanavyotumia intaneti, hasa kwa wale wanaotegemea AI katika kazi zao za kila siku. Kwa sasa, OpenAI haijatangaza rasmi tarehe ya uzinduzi kamili wa Atlas kwa umma, lakini browser hiyo imeanza kuvutia hisia nyingi mtandaoni kutokana na uwezo wake wa kipekee.

Read More