Entertainment

Baba Levo Akanusha Taarifa za Kumkimbia Diamond Baada ya Kuteuliwa Mbunge

Baba Levo Akanusha Taarifa za Kumkimbia Diamond Baada ya Kuteuliwa Mbunge

Mbunge wa Kigoma Mjini, Baba Levo, amejitokeza kufafanua madai yaliyosambaa mtandaoni yakidai kuwa angekimbia msanii Diamond Platnumz mara tu baada ya kuteuliwa kuwa mbunge.

Akizungumza baada ya kukula kiapo nje ya majengo ya Bunge, Baba Levo amesema hajawahi na hatarajii kumkimbia Diamond, kwani ndiye mtu aliyemsaidia kupanda ngazi kutoka kudharauliwa na jamii hadi kuwa mtu mwenye heshima.

Msanii huyo aliyegeukia siasa, ameeleza kuwa uhusiano wake na Diamond bado upo imara na kwamba nafasi yake ya kisiasa haitabadilisha ukaribu wao.

Kauli yake imekuja kufuatia tetesi zilizodai kuwa kuteuliwa kwake kungekuwa chanzo cha yeye kujitenga na kundi la Wasafi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *