LifeStyle

Bahati Awataka Mashabiki Kuwa na Subira Kuhusu Matokeo ya DNA

Bahati Awataka Mashabiki Kuwa na Subira Kuhusu Matokeo ya DNA

Msanii nyota wa muziki, Bahati, amewataka mashabiki wake wawe na subira kufuatia shinikizo walilompa la kutaka atangaze matokeo ya vipimo vya DNA vinavyohusiana na mama mmoja aliyedai kuwa mzazi wake wa kumzaa.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Bahati amesema kuwa suala hilo ni nyeti na linahitaji muda kabla ya kuweka wazi matokeo hayo kwa umma. Amesema kuwa anafahamu hamu ya mashabiki wake kutaka kujua ukweli, lakini akawaomba faragha ya kushughulikia jambo hilo kwa utulivu.

Kauli ya Bahati imekuja baada ya kushindwa kutimiza ahadi yake ya kutangaza matokeo hapo jana, licha ya kuthibitisha wiki chache zilizopita kuwa angefanya hivyo Machi 3, kufuatia kukamilika kwa mchakato wa vipimo kati yake na mama aliyedai kuwa mzazi wake wa kumzaa.

Hali hii imezua mjadala mkubwa mitandaoni, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona mwelekeo wa matokeo hayo na namna yatakavyoweza kuathiri maisha yake binafsi na taswira yake katika muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *