Entertainment

Bien Aachia Remix Nane Mpya za Wimbo Wake “All My Enemies Are Suffering”

Bien Aachia Remix Nane Mpya za Wimbo Wake “All My Enemies Are Suffering”

Mwanamuziki nyota Bien ameendeleza kasi ya mafanikio ya kibao chake “All My Enemies Are Suffering” baada ya kuachia rasmi remix nane mpya za wimbo huo.

Katika remixes hizo, Bien amewaleta pamoja mastaa wengi wakubwa kutoka maeneo mbalimbali ya Afrika, akiwemo Tobe Nwigwe, Breeder LW, Khaligraph Jones, Original Stinger, Yemi Alade na Jerau, miongoni mwa wengine. Ushirikiano huo umeupa mradi huo ladha tofauti tofauti, kuanzia rap kali, afro-fusion hadi mitindo ya Kisoul.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa burudani, hatua ya Bien ni mkakati wa kupanua wigo wa wimbo huo kimataifa na kuendeleza ushawishi wake katika muziki wa kizazi kipya barani Afrika.

Kuachiwa kwa remixes hizo pia imekuja mara baada ya toleo la asili la wimbo huo kutajwa na Spotify kama moja ya nyimbo bora barani Afrika mwaka 2025 kupitia playlist ya Best of African Heat, ambapo ilikamata nafasi ya tisa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *