LifeStyle

Ivy Trizah Muhenje Avikwa Rasmi Taji la Miss World Kenya 2026

Ivy Trizah Muhenje Avikwa Rasmi Taji la Miss World Kenya 2026

Mrembo Ivy Trizah Muhenje ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa taji la Miss World Kenya 2026, taarifa iliyothibitishwa na uongozi wa Mr and Miss World Kenya kupitia mitandao yao ya kijamii.

Katika taarifa yao, waandaaji hao wameeleza furaha yao wakisema kuwa wamefurahishwa kutawazwa kwa Ivy Trizah Muhenje kama Miss World Kenya 2026, hatua iliyopokelewa kwa shangwe na pongezi kutoka kwa wadau wa mashindano ya urembo nchini Kenya.

Kwa sasa, Ivy Trizah Muhenje anajiandaa kuanza safari yake mpya ya kuiwakilisha Kenya chini ya kaulimbiu ya #BeautyWithAPurpose, akitarajiwa kuwa balozi wa masuala ya kijamii na maendeleo, sambamba na kushiriki mashindano ya Miss World katika ngazi ya kimataifa.

Wakenya wameendelea kumpongeza Ivy kupitia mitandao ya kijamii, wakimtakia heri na mafanikio mema katika jukumu lake jipya la kuwa sura ya Kenya kwenye ulimwengu wa mashindano ya urembo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *