Entertainment

Guardian Angel Amtia Moyo Oga Obinna Baada ya Kukosolewa Mitandaoni

Guardian Angel Amtia Moyo Oga Obinna Baada ya Kukosolewa Mitandaoni

Staa wa nyimbo za injili nchini Kenya, Guardian Angel, amemtaka mtangazaji Oga Obinna kupuuza ukosoaji wa watu na kuendelea kusaidia vijana kupitia jukwaa lake, akisisitiza umuhimu wa kufanya mema bila kuathiriwa na maneno ya chuki.

Akizungumza katika hafla ya kumuaga marehemu Shalkido hapo jana, Guardian amemtia moyo mtangazaji huyo, akimhimiza kutokata tamaa licha ya wimbi la ukosoaji alioupokea mitandaoni

Hitmaker huyo wa Kimya, amempongeza Obinna kwa moyo wake wa kusaidia watu na kumtaka aendelee na juhudi zake za kuinua jamii licha ya upinzani na ukosoaji anaokutana nao.

Guardian ameongeza kuwa mara nyingi watu wanaojituma kufanya mazuri ndio hukosolewa zaidi, lakini kinachojalisha ni athari chanya wanayoacha katika jamii.

Guardian Angel, alikuwa miongoni mwa waombolezaji waliouthuria mazishi ya msanii wa miondoko ya Gengetone, Shalkidoh, yaliyofanyika jana katika kijiji cha Kimbo Matangi, Kaunti ya Kiambu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *