Gossip

Lulu Diva Akanusha Taarifa za Kumnyang’anya Wema Sepetu Mume Wake Whozu

Lulu Diva Akanusha Taarifa za Kumnyang’anya Wema Sepetu Mume Wake Whozu

Msanii wa Bongo Fleva Lulu Diva ameweka wazi msimamo wake na kukanusha vikali taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa alimnyang’anya Wema Sepetu mume wake, msanii Whozu.

Kupitia waraka mrefu aliouandika Instagram, Lulu Diva amefafanua kuwa Whozu ni rafiki yake wa muda mrefu, na urafiki wao ulianza siku nyingi kabla hata ya Whozu kuanza mahusiano na Wema Sepetu. Ameongeza kuwa hakuwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Whozu, hivyo madai ya kumnyang’anya mtu mume wake ni ya uongo mtupu.

Kwa mujibu wa Lulu Diva, tofauti iliyojitokeza kati yake na Wema Sepetu haikuhusiana kabisa na Whozu, bali ilitokana na masuala mengine binafsi ambayo ameona hayapaswi kuwekwa hadharani.

Mrembo huyo, ameeleza kuwa katika kipindi ambacho Whozu na Wema walikuwa wakipitia changamoto katika mahusiano yao, kila mmoja alitarajia yeye achukue upande, jambo alilolikataa kwa kuwa wote ni marafiki zake.

Msanii huyo amesema taarifa zinazoendelea kusambazwa ni juhudi za makusudi za kumchafua mbele ya jamii, akisisitiza kuwa urafiki unaweza kufikia mwisho bila kugeuka kuwa uadui. Amehitimisha ujumbe kwa kutoa wito kwa umma kuacha kueneza fitina, akisema kila mtu aendelee na maisha yake kwa amani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *